Kwanini hatuwazi kama Japan, Korea, Singapore na Ulaya?

Kwanini hatuwazi kama Japan, Korea, Singapore na Ulaya?

Mwafrika mmoja

Senior Member
Joined
Mar 15, 2019
Posts
104
Reaction score
234
Mwaka 2026 dunia sasa inakimbia sana, mambo yanabadilika kila baada ya sekunde 30 lakini kwa nchi nyingi za Afrika. Inawezekana kabisa mambo yanabadilika.Kila baada ya wiki 30.

Huwa inaumiza sana na kushangaza, katika karne ya 21 mwaka 2026 unakuta binadamu wanagombania usafiri kituoni mpaka wanachaniana mashati.

Wamama wanapoteza viatu vyao, mikoba yao na wengine wanapata ulemavu. Kwa kukanyagwa kwenye purukushani za kupanda daladala.

Ukiwa mtumiaji wa usafiri huu wa umma utakuwa unaelewa kila kitu ninachozungumza hapa. Wengi wana maumivu sana ukikaa nao kwenye usafiri huu, hawaoni dalili ni lini maisha yatakuwa afadhani. Kwamba na wao watakuwa na furaha kutumia usafiri wa umma.

Kwamba na wao watatumia treni za kisasa za mjini (Tram) ambazo zinapita kwenye njia zake tu, hakuna foleni, hakuna ugomvi wala kubanana kama ng'ombe zizini. Bara la Afrika, Tanzania ikiwemo ina kila kitu cha kutufanya tuishi kama Ulaya, Japan, China na South Korea wanavyoishi. Kwa ustaarabu wa hali ya juu.

Natambua juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuboresha usafiri wa umma Tanzania, lakini kwenye hizo sehemu ambazo miundominu ya kisasa ya usafiri wa umma inatumika.Zinatakiwa juhudi kubwa zingine kuboresha uendeshaji na usimamizi wake.

Mabasi yanatakiwa kuwa mengi, kila baada ya dakika 10 basi liwe linaingia kituoni na basi liwe linasimamisha watu wachache sana siyo kama ilivyo sasa. Lakini tusiishie kwenye mwendokasi pekee. Majiji kama Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya yanatakiwa kuwa na miundombinu ya treni za mjini.

Treni za mjini zitasaidia kupunguza sana magari barabarani kwasababu Watu hawataona haja ya kununua magari wakati wanaweza kutumia dakika 30 tu kufika kazini.

Afrika inapaswa kufikiri sawasawa na Ulaya, Singapore, Dubai, Hong Kong na Marekani zinavyofikiri. Sisi siyo wanyonge, tuna kila kitu kuliko wao KWANINI TUFELI?
 
Back
Top Bottom