Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Huyu ni kiongozi wa pili kutoka CCM ambaye anatoa kauli tatanishi kuhusu kupoteza watu pamoja na watu wasiyojulikana, lakini wanaishia kutenguliwa na kuonywa tu na hakuna hatua nyingine inachukuliwa dhidi yao.
Wa kwanza alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Kagera, akasema wakiwapoteza watu polisi wala wasijisumbue kuwatafuta, zaidi kwenye hilo soma hapa: Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute
Polisi wala hawakufanya lolote, tukaishia kupata kauli tu za viongozi CCM ooh ni kijana tu ameteleza, mara hatukubaliani na alichosema, ikaisha hivyo, na sasa tunaona kweli watu wanapotezwa kama alivyosema na polisi wala hawajisumbui mpaka wanaagizwa na mahakama kufanya kazi yao!
Leo mwingine karudia yaleyale sema kwa lugha nyingine tu, kuwa kipindi kile walifanya na sasa wamejipanga kufanya tena. Kikubwa wanachofanya ni kutengua, kuonya kishkaji na kuja na matamko yao ya maigizo kuwa alichosema siyo msimamo wa chama!
Zaidi soma hapa: Kuelekea 2025 - DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!
Wahalifu wanasema waziwazi ushiriki wao kwenye matukio hayo kwanini hawachukuliwi hatua kwenda kulisaidia polisi? Au mpaka wawe wapinzani ndio wanastahili kuchukuliwa hatua?
Polisi/Serikali mtaendelea kufumbia macho hayo mpaka lini? Mpaka wananchi wanaanze kushungulika na watu hawa kwa namna wanayoona inafaa kwakuwa nyie mmewaangusha?