Kwanini Hayati Magufuli alikuwa hapendwi jimboni kwake?

Pascal kusema kweli nimezaliwa enzi za Nyerere ila huyu mwamba sitamsahau kwa visa vyake,ana mazuri mengi na mapungufu mengi pia ila yote juu ya yote mwamba alikuwa mpambanaji,atakumbukwa kuliko marais wote ndio maana anaandikwa sana karibu JS
Nikiwa pande zile huwa nalala pale kwake, kuna siku nilikuja na wazungu 3, kwa assignment ya 10 days Bimulo, wazungu wakataka scrambled eggs for breakfast, wakaletewa omelettes!, nikampandia chef, hajui kuandaa scrambled!. Wazungu waka complain, kumbe Maza yupo!, huwezi amini, Maza mwenyewe in person aliingia jikoni kuandaa scrambled!.

Ni kweli mwanzoni huyu mwamba alianza vibaya ila mwishoni alikuja kubadilika na kuwa ni mtu poa wa ajabu!. Hata mimi baada ya kumpiga lile swali siku ile, cha moto nilikipata!, nikadhani ni yeye ndio alinimaind!, nikampandia!, kumbe sio yeye ni yale majinga fulani tuu kule 'sehemu'. Usikute hata Ben Saanane, Azory Gwanda au Lissu wala sio yeye ni yale yale majinga kule!.

Angalia zile siku za mwisho mwisho alivyokuja kubadilika... "Mimi ni Mwenzenu Hapa, Sijabadilika ni Yule Yule "KaJoni" - Ni Maneno Simple, Humble and Down to Earth Yenye Maana Kubwa! na Rais Magufuli, so far, is the best president this country has ever had. Msikivu, ana upendo na huruma. Atabarikiwa sana. Tanzania itabarikiwa! na Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana! hata la katiba ilikuwa amalizane halo Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!.

Hivyo baada ya kuitwa ni amekwenda straight moja kwa moja Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

RIP JPM
P
 
Kama alibadilika mbona alinajisi ule uchaguzi wa 2022 na watu wengi kufungwa na kujeruhiwa?
Kiburi chake kuhusu kukataa chanjo Covid kikagharimu maisha ya wengi?
 
Kama alibadilika mbona alinajisi ule uchaguzi wa 2022 na watu wengi kufungwa na kujeruhiwa?
Kiburi chake kuhusu kukataa chanjo Covid kikagharimu maisha ya wengi?
Uchaguzi gani wa 2022?!, aliunajisia wapi wakati alikuwa tayari yuko 6ft under?!.
I know you ment uchaguzi wa 2020!, kiukweli sio yeye ni yale majinga kule 'sehemu' yalimponza!.
P.
 
Uchaguzi gani wa 2022?!, aliunajisia wapi wakati alikuwa tayari yuko 6ft under?!.
I know you ment uchaguzi wa 2020!, kiukweli sio yeye ni yale majinga kule 'sehemu' yalimponza!.
P.
Sasa hayo majinga si alikuwa na uwezo wa kuyadhibiti?

Magufuli alikuwa akiingia kanisani na kuwakejeli wazi wazi viongozi wa dini waliokuwa wakihimiza waumini wajikinge na Covid
Huku akijua kabisa Covid ilikuwepo na iliua viongozi kadhaa ndani ya serikali yake
Hapa ilikuwa ni hao wajinga au kiburi chake!?
 
Sass ilikuwaje lissu akapigwa mawe ,acha ujinga
 
Mjifunze kupokea taarifa hata msizozipenda sasa wewe ukivimbisha domo lako hapa na ukweli wa mambo ndo huo itasaidia nini? Au unadhani unaweza kufuta historia. Magufuli alikua binadamu siyo malaika yule useme alifanya mazuri tu hakuwa na mabaya .mwandishi Hapa amejaribu kumwelezea anavyomfahamu kwa undani we na we anzisha andiko lako utuwambie unavomjua magufuli tutakuja kuchangia.
 
Vipi kwani Ile Brevis yako Bado unayo? Mbona ulikuwa unapewa laki 3 Kila siku na mzee kwenda kukusanya data watu wanamsemaje kitaa, ulikuwa kimya Leo unadiriki kusema alikuwa na roho mbaya
 
Vipi kwani Ile Brevis yako Bado unayo? Mbona ulikuwa unapewa laki 3 Kila siku na mzee kwenda kukusanya data watu wanamsemaje kitaa, ulikuwa kimya Leo unadiriki kusema alikuwa na roho mbaya
Dah we jamaa wewe
 
Pascal uko sahihi kuna majinga yamefanya aonekane mkatili,kuna vitu yalifanya bila yeye kushirikishwa,na alikuwa anabadilika kuwa mwema kadri siku zinavyoenda.
 
Pascal uko sahihi kuna majinga yamefanya aonekane mkatili,kuna vitu yalifanya bila yeye kushirikishwa,na alikuwa anabadilika kuwa mwema kadri siku zinavyoenda.
Sure, JPM alikuwa anabadilika kuwa mwema, nadhani zile zilikua pressure za awamu ya kwanza tu,, hakulisemea swala la wasiojulikana, lakini kimya kimya akamtoa kipilimba na kumweka Afande Diwani,, tangu hapo suala hilo likatoweka🤷‍♂️
 
Nabii hakubaliki nyumbani.

Niliwahi shuhudia ktk mkutano ambao Mwl Nyerere alikuwa akimnadi Mr Mkapa uwanja wa mkendo musoma mjini,

Umma ulikuwa ukimzomea mara Kwa mara na akalazimika kukatisha hotuba yake mara Kwa mara,

Watu walipoona anawapuuzia na kuendelea kuongea, wahuni walirnda kumleta mtu aliyefahamika Kwa Jina la KIBOKO aliyekuwa ndugu wa Nyerere ambaye nati zote hazikuwa zimekaza,

Alipofika mkutano I, Mwl Nyerere ikamlazimu kukatisha mkutano wake.

All in all Magu anakubalika na wengi kuliko wasiomkubali.

Tunamshukuru Mungu Kwa zawadi ya Magu.

Aamen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…