Kwanini Hayati Magufuli alikuwa hapendwi jimboni kwake?

Kwanini Hayati Magufuli alikuwa hapendwi jimboni kwake?

Kiburi na dharau dhidi ya wazee wake wa Chato ni moja ya vitu vilivyomuangusha sana .

Wakati mmoja akiwa na ziara jimboni Chato , Wazee walimuomba awawekee lami kwenye barabara yao , wakati huo alikuwa waziri wa ujenzi , lakini pia alikuwa mbunge wao , Magufuli aliwashambulia wazi wazi wazee wale kwamba yeye siyo Waziri wa Chato bali ni waziri wa Tanzania nzima , hivyo hawezi kuwapendelea wao ili wapate lami , na kwamba KAMA WANATAKA LAMI WANYE MAVI YAO WAYASILIBE BARABARANI IWE LAMI .

Watu wote walishangazwa na kauli ile na hiyo ni moja ya kauli iliyomfanya achukiwe kwao , huyu mahusiano yake na wananchi yalirejea baada ya kuteuliwa kugombea Urais baaasi , hakuwa na ushawishi wowote kabla ya hapo
Hata vijana wa chadema nao walimtukana sana daktar Slaa na kumpenda mno Mzee Lowasa hivi ndivyo siasa ilivyo
 
Mimi sijazungumzia wenyeji wa chato jamii nyingi hata geita katoro na Kahama sio ya wasukuma kwa asili ila majority kwa sasa ni wasukuma!
Mimi nakushangaa Kusema Chato waha ni wengi lakini ukweli ni kwamba waha chato ni wachache sana maana shughuli nyingi za waha hasa wanapokuwa wahamiaji ni biashara ndogo ndogo sio uvuvi wala kilimo!
Waha wengi wapo mjini wakifanya biashara hasa ya maduka na masokoni!
Kwa chato wapo ila sio wengi wakuweza Kusema ni majority!
Nadhani hakumaanisha Chato mjini,alimaanisha chato kama wilaya,nilikuwa bwanga,buziku na kuna mji unaitwa nyakayondwa ni kama upo kigoma,waha wengi sana kwenye hizo kata
 
Tunaweza share ata audio akiwaambia wanye mavi yao?

Binafsi naona magufuli alikuwa na ushawishi ila ushawishi wake ulibebwa na utendaji wake wa kazi sio maneno kama walivyokuwa wengine! Binafsi sikuhitaji kampeni kumpigia magufuli kura 2015 ila aliyoyatenda huko nyuma kabla 2015 October ndiyo yalipelekea nione sehemu sahihi ya kura yangu ni kwa Magufuli.
Huna akili
 
Huenda hili likakushangaza lakini ukweli ndio huu, zaidi ya nusu ya watu wa jimboni kwake hawakumpenda.
Ila wale waliompenda walimpenda sana tena sana.

Visa vyote ninavyoandika kumuhusu Hayati Magufuli ni vya kweli sababu nilikuwa nae karibu kwa kazi fulani ambayo sitaitaja humu,nimeishi jimboni kwake Chato nikifanya kazi hiyo,nimeingia Ikulu bila appointment nikifanya kazi hiyo.

Naifahamu Chato kama ninavyoifahamu Dar na Dodoma

Kwa wasiofahamu jimbo hili ngoja niwape muhtasari kidogo,nimezunguka Tanzania hii sijawahi kuona jimbo lina makabila mengi kama jimbo la Chato,huwezi kujua kabila kipi ni dominant na lipi predominant,

Chato kuna
Wahangaza,wanyambo,watutsi,
warundi,waha,wazinza,wasubi,wahaya,wazinza,wasumbwa,wasukuma,na kila mmoja hujiona hapo ni kwao kwa asili.watu wa huko hufahamu lugha hizo zote,hata hayati JPM alijua hizo lugha zote japo kihistoria baba yake alihamia.

Miaka ya nyuma Chato ilikuwa tarafa ndani ya wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera ,Sasa mwaka 1990 hayati JPM akagombea ubunge na mzee Phares Kabuye,alishindwa vibaya sana kura za maoni unajua kwa nini?

Jpm alikuwa akienda vijiji vyenye wasukuma anajifanya msukuma na kuwaponda wasubi kuwa ni wakulima wa migomba mbunge wao hawezi kuwasaidia wao wakulima wa pamba,hivyo wamchague yeye.

Meanwhile akienda Biharamulo anajifanya ni Msubi na kuongea Kisubi na anawaambia yeye ni ukoo wa Wayango wazilankende,ukoo ambao hauko usukumani bali kigoma ,butundi,rwanda,uganda na makabila yanayosikilizana na wahaya.hapo atajifanya msubi orijino na kuwaponda wasukuma kuwa ni wanyamahanga yaani wavamizi wa mkoa wa Kagera,

Akienda maeneo yenye waha wengi atajifanya muha na kuongea kiha na kirundi,siasa za ukabila zikamponza akadondokea pua.

Mizimu ya kwao ikamsaidia jimbo likagawanywa mashariki na magharibi 1995 akagombea mashariki ilipo kata ya Chato akajibatiza usukuma ila kuna wakati alikuwa akijisahau na kurudia kusema yeye ni myango ukoo ambao hauko usukumani,

Akagombea kwa style ileile ya kutumia vernacular languages kulingana na audience.
Akajikuta anachukiwa na makabila mengine jimboni kwake isipokuwa wasukuma.

Uwekezaji alioufanya jimboni kwake baada ya kuwa Rais ilikuwa ni kutafuta huruma na kufuta makovu ya makabila mengine na alifanikiwa maana makabila yote yalifaidi uwekezaji ule.

Lakini watu wa Biharamulo magharibi hawatamsahau kwa maana barabara ya lami oliyotakiwa kupita mjini kwao kuelekea Bukoba ilipofika kata ya Bwanga akaichepusha kuelekea Chato,Muleba kama adhabu ya kumnyima kura 1990.
Barabara hiyo ilikuja kuwekwa lami baadae baadae sana.

Utajiuliza mbona alikuwa anashinda ubunge kila mara
kama hakuwa anapendwa?
Ni kwamba ulitumika umafia na hadaa kwa washindani wake,wengine wakitishwa au kutekwa au kuahidiwa vyeo na pesa ili wajitoe kugombea nae

Hitimisho;
Ukabila upo na Hayati JPM alichukiwa jimboni kwake sababu ya mbegu ya ukabila iliyopandwa na........
Noma sana ,Push Gang watakuvamia.
 
Mimi sijazungumzia wenyeji wa chato jamii nyingi hata geita katoro na Kahama sio ya wasukuma kwa asili ila majority kwa sasa ni wasukuma!
Mimi nakushangaa Kusema Chato waha ni wengi lakini ukweli ni kwamba waha chato ni wachache sana maana shughuli nyingi za waha hasa wanapokuwa wahamiaji ni biashara ndogo ndogo sio uvuvi wala kilimo!
Waha wengi wapo mjini wakifanya biashara hasa ya maduka na masokoni!
Kwa chato wapo ila sio wengi wakuweza Kusema ni majority!
tembelea kata ya busere, kasenga, bwana na nyarutembo uone waha.
 
Kiburi na dharau dhidi ya wazee wake wa Chato ni moja ya vitu vilivyomuangusha sana .

Wakati mmoja akiwa na ziara jimboni Chato , Wazee walimuomba awawekee lami kwenye barabara yao , wakati huo alikuwa waziri wa ujenzi , lakini pia alikuwa mbunge wao , Magufuli aliwashambulia wazi wazi wazee wale kwamba yeye siyo Waziri wa Chato bali ni waziri wa Tanzania nzima , hivyo hawezi kuwapendelea wao ili wapate lami , na kwamba KAMA WANATAKA LAMI WANYE MAVI YAO WAYASILIBE BARABARANI IWE LAMI .

Watu wote walishangazwa na kauli ile na hiyo ni moja ya kauli iliyomfanya achukiwe kwao , huyu mahusiano yake na wananchi yalirejea baada ya kuteuliwa kugombea Urais baaasi , hakuwa na ushawishi wowote kabla ya hapo
Kwahiyo walimchukia kwasababu hakutaka kutumia nafasi yake ya uwaziri wa ujenzi kuwapendelea wanachato!?...
 
Back
Top Bottom