Kwanini Hayati Magufuli alikuwa hapendwi jimboni kwake?

Huenda hili likakushangaza lakini ukweli ndio huu,zaidi ya nusu ya watu wa jimboni kwake hawakumpenda.
Ila wale waliompenda walimpenda sana tena sana

Visa vyote ninavyoandika kumuhusu Hayati Magufuli ni vya kweli sababu nilikuwa nae karibu kwa kazi fulani ambayo sitaitaja humu,nimeishi jimboni kwake Chato nikifanya kazi hiyo,nimeingia Ikulu bila appointment nikifanya kazi hiyo.

Naifahamu Chato kama ninavyoifahamu Dar na Dodoma

Kwa wasiofahamu jimbo hili ngoja niwape muhtasari kidogo,nimezunguka Tanzania hii sijawahi kuona jimbo lina makabila mengi kama jimbo la Chato,huwezi kujua kabila kipi ni dominant na lipi predominant,

Chato kuna warundi,waha,wazinza,wasubi,wahaya,wazinza,wasumbwa,wasukuma,na kila mmoja hujiona hapo ni kwao kwa asili.watu wa huko hufahamu lugha hizo zote,hata hayati JPM alijua hizo lugha zote japo kihistoria baba yake alihamia.

Miaka ya nyuma Chato ilikuwa tarafa ndani ya wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera ,Sasa mwaka 1990 hayati JPM akagombea ubunge na mzee Phares Kabuye,alishindwa vibaya sana kura za maoni unajua kwa nini?

Jpm alikuwa akienda vijiji vyenye wasukuma anajifanya msukuma na kuwaponda wasubi kuwa ni wakulima wa migomba mbunge wao hawezi kuwasaidia wao wakulima wa pamba,hivyo wamchague yeye.

Meanwhile akienda Biharamulo anajifanya ni Msubi na kuongea Kisubi na anawaambia yeye ni ukoo wa Wayango wazilankende,ukoo ambao hauko usukumani bali kigoma ,butundi,rwanda,uganda na makabila yanayosikilizana na wahaya.hapo atajifanya msubi orijino na kuwaponda wasukuma kuwa ni wanyamahanga yaani wavamizi wa mkoa wa Kagera,

Akienda maeneo yenye waha wengi atajifanya muha na kuongea kiha na kirundi,siasa za ukabila zikamponza akadondokea pua.

Mizimu ya kwao ikamsaidia jimbo likagawanywa mashariki na magharibi 1995 akagombea mashariki ilipo kata ya Chato akajibatiza usukuma ila kuna wakati alikuwa akijisahau na kurudia kusema yeye ni myango ukoo ambao hauko usukumani,

Akagombea kwa style ileile ya kutumia vernacular languages kulingana na audience.
Akajikuta anachukiwa na makabila mengine jimboni kwake isipokuwa wasukuma.

Uwekezaji alioufanya jimboni kwake baada ya kuwa Rais ilikuwa ni kutafuta huruma na kufuta makovu ya makabila mengine na alifanikiwa maana makabila yote yalifaidi uwekezaji ule.

Lakini watu wa Biharamulo magharibi hawatamsahau kwa maana barabara ya lami oliyotakiwa kupita mjini kwao kuelekea Bukoba ilipofika kata ya Bwanga akaichepusha kuelekea Chato,Muleba kama adhabu ya kumnyima kura 1990.
Barabara hiyo ilikuja kuwekwa lami baadae baadae sana.

Utajiuliza mbona alikuwa anashinda ubunge kila mara
kama hakuwa anapendwa?
Ni kwamba ulitumika umafia na hadaa kwa washindani wake,wengine wakitishwa au kutekwa au kuahidiwa vyeo na pesa ili wajitoe kugombea nae

Hitimisho;
Ukabila upo na Hayati JPM alichukiwa jimboni kwake sababu ya mbegu ya ukabila iliyopandwa na........
Nonsense!.
 
Alishindwa Ubunge kila mwaka! Kwani uchaguzi ukifanyika kila mwaka huko Chato? 1990 ndiyo kila mwaka? 1995 vip? 2000, 2005, 2010 vip alishindwa pia?

Alikuwa mbunge vipindi vitatu 1995 hadi 2010 (jimbo la Chato) kwa kupita bila kupingwa baada ya kuwanunua washindani wake. Mara mbili, alianguka kwenye kura za maoni (jimbo la Biharamulo).
 
Alikuwa mbunge vipindi viwili 2005 na 2010 (jimbo la Chato) kwa kupita bila kupingwa baada ya kuwanunua washindani wake. Mara mbili, 1995 na 2000 alianguka kwenye kura za maoni (jimbo la Biharamulo).
Uko serious?
 
Kiburi na dharau dhidi ya wazee wake wa Chato ni moja ya vitu vilivyomuangusha sana .

Wakati mmoja akiwa na ziara jimboni Chato , Wazee walimuomba awawekee lami kwenye barabara yao , wakati huo alikuwa waziri wa ujenzi , lakini pia alikuwa mbunge wao , Magufuli aliwashambulia wazi wazi wazee wale kwamba yeye siyo Waziri wa Chato bali ni waziri wa Tanzania nzima , hivyo hawezi kuwapendelea wao ili wapate lami , na kwamba KAMA WANATAKA LAMI WANYE MAVI YAO WAYASILIBE BARABARANI IWE LAMI .

Watu wote walishangazwa na kauli ile na hiyo ni moja ya kauli iliyomfanya achukiwe kwao , huyu mahusiano yake na wananchi yalirejea baada ya kuteuliwa kugombea Urais baaasi , hakuwa na ushawishi wowote kabla ya hapo

Alikua na kauli za hovyo sana utadhani sio kiongozi.
 
Alikuwa mbunge vipindi viwili 2005 na 2010 (jimbo la Chato) kwa kupita bila kupingwa baada ya kuwanunua washindani wake. Mara mbili, 1995 na 2000 alianguka kwenye kura za maoni (jimbo la Biharamulo).
Wewe ni mwongo. Magu kawa mbunge kuanzia 1995. Hizo alizoanguka ni kabla ya hapo.
 
Ndio maana uchaguzi wa 2020 aliharibu kabisa. Hana historia ya kushinda kihalali.
Hana ushawishi zaidi ya ubabe tu
Kilichofanyika 2020 kwa nchi zingine ilikuwa ni machafuko LIVE. Majirani walishangaa sana kwa utulivu wetu. Mungu atuepushe isitokee tena. Nina imani mama hatafanya kama mtangulizi wake.
 
Huenda hili likakushangaza lakini ukweli ndio huu,zaidi ya nusu ya watu wa jimboni kwake hawakumpenda.
Ila wale waliompenda walimpenda sana tena sana

Visa vyote ninavyoandika kumuhusu Hayati Magufuli ni vya kweli sababu nilikuwa nae karibu kwa kazi fulani ambayo sitaitaja humu,nimeishi jimboni kwake Chato nikifanya kazi hiyo,nimeingia Ikulu bila appointment nikifanya kazi hiyo.

Naifahamu Chato kama ninavyoifahamu Dar na Dodoma

Kwa wasiofahamu jimbo hili ngoja niwape muhtasari kidogo,nimezunguka Tanzania hii sijawahi kuona jimbo lina makabila mengi kama jimbo la Chato,huwezi kujua kabila kipi ni dominant na lipi predominant,

Chato kuna warundi,waha,wazinza,wasubi,wahaya,wazinza,wasumbwa,wasukuma,na kila mmoja hujiona hapo ni kwao kwa asili.watu wa huko hufahamu lugha hizo zote,hata hayati JPM alijua hizo lugha zote japo kihistoria baba yake alihamia.

Miaka ya nyuma Chato ilikuwa tarafa ndani ya wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera ,Sasa mwaka 1990 hayati JPM akagombea ubunge na mzee Phares Kabuye,alishindwa vibaya sana kura za maoni unajua kwa nini?

Jpm alikuwa akienda vijiji vyenye wasukuma anajifanya msukuma na kuwaponda wasubi kuwa ni wakulima wa migomba mbunge wao hawezi kuwasaidia wao wakulima wa pamba,hivyo wamchague yeye.

Meanwhile akienda Biharamulo anajifanya ni Msubi na kuongea Kisubi na anawaambia yeye ni ukoo wa Wayango wazilankende,ukoo ambao hauko usukumani bali kigoma ,butundi,rwanda,uganda na makabila yanayosikilizana na wahaya.hapo atajifanya msubi orijino na kuwaponda wasukuma kuwa ni wanyamahanga yaani wavamizi wa mkoa wa Kagera,

Akienda maeneo yenye waha wengi atajifanya muha na kuongea kiha na kirundi,siasa za ukabila zikamponza akadondokea pua.

Mizimu ya kwao ikamsaidia jimbo likagawanywa mashariki na magharibi 1995 akagombea mashariki ilipo kata ya Chato akajibatiza usukuma ila kuna wakati alikuwa akijisahau na kurudia kusema yeye ni myango ukoo ambao hauko usukumani,

Akagombea kwa style ileile ya kutumia vernacular languages kulingana na audience.
Akajikuta anachukiwa na makabila mengine jimboni kwake isipokuwa wasukuma.

Uwekezaji alioufanya jimboni kwake baada ya kuwa Rais ilikuwa ni kutafuta huruma na kufuta makovu ya makabila mengine na alifanikiwa maana makabila yote yalifaidi uwekezaji ule.

Lakini watu wa Biharamulo magharibi hawatamsahau kwa maana barabara ya lami oliyotakiwa kupita mjini kwao kuelekea Bukoba ilipofika kata ya Bwanga akaichepusha kuelekea Chato,Muleba kama adhabu ya kumnyima kura 1990.
Barabara hiyo ilikuja kuwekwa lami baadae baadae sana.

Utajiuliza mbona alikuwa anashinda ubunge kila mara
kama hakuwa anapendwa?
Ni kwamba ulitumika umafia na hadaa kwa washindani wake,wengine wakitishwa au kutekwa au kuahidiwa vyeo na pesa ili wajitoe kugombea nae

Hitimisho;
Ukabila upo na Hayati JPM alichukiwa jimboni kwake sababu ya mbegu ya ukabila iliyopandwa na........
Cc: Erythrocyte
 
Back
Top Bottom