Huenda hili likakushangaza lakini ukweli ndio huu,zaidi ya nusu ya watu wa jimboni kwake hawakumpenda.
Ila wale waliompenda walimpenda sana tena sana
Visa vyote ninavyoandika kumuhusu Hayati Magufuli ni vya kweli sababu nilikuwa nae karibu kwa kazi fulani ambayo sitaitaja humu,nimeishi jimboni kwake Chato nikifanya kazi hiyo,nimeingia Ikulu bila appointment nikifanya kazi hiyo.
Naifahamu Chato kama ninavyoifahamu Dar na Dodoma
Kwa wasiofahamu jimbo hili ngoja niwape muhtasari kidogo,nimezunguka Tanzania hii sijawahi kuona jimbo lina makabila mengi kama jimbo la Chato,huwezi kujua kabila kipi ni dominant na lipi predominant,
Chato kuna warundi,waha,wazinza,wasubi,wahaya,wazinza,wasumbwa,wasukuma,na kila mmoja hujiona hapo ni kwao kwa asili.watu wa huko hufahamu lugha hizo zote,hata hayati JPM alijua hizo lugha zote japo kihistoria baba yake alihamia.
Miaka ya nyuma Chato ilikuwa tarafa ndani ya wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera ,Sasa mwaka 1990 hayati JPM akagombea ubunge na mzee Phares Kabuye,alishindwa vibaya sana kura za maoni unajua kwa nini?
Jpm alikuwa akienda vijiji vyenye wasukuma anajifanya msukuma na kuwaponda wasubi kuwa ni wakulima wa migomba mbunge wao hawezi kuwasaidia wao wakulima wa pamba,hivyo wamchague yeye.
Meanwhile akienda Biharamulo anajifanya ni Msubi na kuongea Kisubi na anawaambia yeye ni ukoo wa Wayango wazilankende,ukoo ambao hauko usukumani bali kigoma ,butundi,rwanda,uganda na makabila yanayosikilizana na wahaya.hapo atajifanya msubi orijino na kuwaponda wasukuma kuwa ni wanyamahanga yaani wavamizi wa mkoa wa Kagera,
Akienda maeneo yenye waha wengi atajifanya muha na kuongea kiha na kirundi,siasa za ukabila zikamponza akadondokea pua.
Mizimu ya kwao ikamsaidia jimbo likagawanywa mashariki na magharibi 1995 akagombea mashariki ilipo kata ya Chato akajibatiza usukuma ila kuna wakati alikuwa akijisahau na kurudia kusema yeye ni myango ukoo ambao hauko usukumani,
Akagombea kwa style ileile ya kutumia vernacular languages kulingana na audience.
Akajikuta anachukiwa na makabila mengine jimboni kwake isipokuwa wasukuma.
Uwekezaji alioufanya jimboni kwake baada ya kuwa Rais ilikuwa ni kutafuta huruma na kufuta makovu ya makabila mengine na alifanikiwa maana makabila yote yalifaidi uwekezaji ule.
Lakini watu wa Biharamulo magharibi hawatamsahau kwa maana barabara ya lami oliyotakiwa kupita mjini kwao kuelekea Bukoba ilipofika kata ya Bwanga akaichepusha kuelekea Chato,Muleba kama adhabu ya kumnyima kura 1990.
Barabara hiyo ilikuja kuwekwa lami baadae baadae sana.
Utajiuliza mbona alikuwa anashinda ubunge kila mara
kama hakuwa anapendwa?
Ni kwamba ulitumika umafia na hadaa kwa washindani wake,wengine wakitishwa au kutekwa au kuahidiwa vyeo na pesa ili wajitoe kugombea nae
Hitimisho;
Ukabila upo na Hayati JPM alichukiwa jimboni kwake sababu ya mbegu ya ukabila iliyopandwa na........
Pale alipojenga ni ardhi ya baba yake, hii ilizua ugomvi na mdogo wake kwa nini ajenge katika ardhi ya familia kabla hawajagawana, wakati huo dogo alikuwa mwanasheria musoma, JPM (akianza ukatiki na dhulma zamani) akamtumia difenda la polisi likamtoa musoma mpaka Chato, hapo ndio wanachato walipomchukia zaidi kwa kuwa walijua anamuonea. Hakuishia hapo, alimbania sana katika mambo mengi.
Pale rubambangwe Kuna mlima, pale palijengwa makazi ya mkuu wa wilaya, lakini tangu yajengwe, hapajawahi kukaliwa na mkuu wa wilaya, baadae JPM akawapa PCCB.
Ukweli ni kwamba maeneo yale ni gambushi(Kijiji Cha wachawi). Kuna habari kwamba zamani enzi ya shida ya usafiri, watu kuamka usiku wa manane kusubiri mabasi, kuna mabasi ya kichawi yalikuwa yanapita pale yakifanana kwa Kila kitu na mabasi ya kawaida na makondakta wale wale wakiita abiria wa mwanza/bukoba, ukipanda tu, unajikuta uko gambushi.
Chato Ina gambushi zaidi ya tano, moja iko makurugusi, hiyo ni kitongoji kabisa, na Serikali imekisajili, kinaitwa gambushi.
JPM enzi ya kampeni ya ubunge alikuwa lazima aende na mama yake mzazi katika kampeni, inasemekana mama yake ni "master sana" kwenye yale mambo yetu. Wengine wanasema ndio maana afya ya mama ilipoyumba, mwamba aliyumba sana kiakili, akabeba mashine za oksijeni za serikali popote zilipo mama akawekewa nyumbani, na daktari bingwa kabisa. Kwa hiyo akawa hawezi kuupiga u-master, yaani beki zikawa hazikabi, fowadi zikawa zinatumbukiza magoli tu kumlenga JPM.
Mara sister naye, nadhani alikuwa kaimu master akadanja, mwamba ilabidi acheze mpira peke yake dhidi ya timu ya watu 11. Kuna video moja ilitembea ya JPM akilia sana, wataalamu walielewa maana yake nini, kwamba Sasa ukuta wa Berlin umevunjika, na wanyama wakali waleee wanaunguruma kwa hasira wakisubiri chakula yao
Mwanzoni alikiwa hakosi kwenda Chato, jioni anazama ndani ya Ile midude mi V8, faster kibirizi, anageuka, kazi ikawa mingi, ikashindikana........basi ndio hivyo tena.
Aliwahi kuwashusha watu na maiti katika gari hoteli yake. Mdogo wake Gordian aliwapa msaada wa usafiri kwe da kuzika, wanaanza safari, wakafika mbali, mwamba akapata taarifa, akawaambia shusha hao watu hapohapo gari zirudi nyumbani.
Alikuwa anawachapa viboko dada zake wakubwa wameolewa kabisaa.
..............