Kwanini Hayati Magufuli alikuwa hapendwi jimboni kwake?

Nabii hakubaliki nyumbani.

Niliwahi shuhudia ktk mkutano ambao Mwl Nyerere alikuwa akimnadi Mr Mkapa uwanja wa mkendo musoma mjini,

Umma ulikuwa ukimzomea mara Kwa mara na akalazimika kukatisha hotuba yake mara Kwa mara,

Watu walipoona anawapuuzia na kuendelea kuongea, wahuni walirnda kumleta mtu aliyefahamika Kwa Jina la KIBOKO aliyekuwa ndugu wa Nyerere ambaye nati zote hazikuwa zimekaza,

Alipofika mkutano I, Mwl Nyerere ikamlazimu kukatisha mkutano wake.

All in all Magu anakubalika na wengi kuliko wasiomkubali.

Tunamshukuru Mungu Kwa zawadi ya Magu.

Aamen.
Nyerere aliwasahau watu wa kwao,hakupeleka huduma muhimu za jamii
 
Huenda hili likakushangaza lakini ukweli ndio huu, zaidi ya nusu ya watu wa jimboni kwake hawakumpenda.
Ila wale waliompenda walimpenda sana tena sana.

Visa vyote ninavyoandika kumuhusu Hayati Magufuli ni vya kweli sababu nilikuwa nae karibu kwa kazi fulani ambayo sitaitaja humu,nimeishi jimboni kwake Chato nikifanya kazi hiyo,nimeingia Ikulu bila appointment nikifanya kazi hiyo.haikuwa kazi ya serikali bali nikiwa kibarua kwenye mradi fulani wilayani Chato,mradi wake binafsi

Naifahamu Chato kama ninavyoifahamu Dar na Dodoma

Kwa wasiofahamu jimbo hili ngoja niwape muhtasari kidogo,nimezunguka Tanzania hii sijawahi kuona jimbo lina makabila mengi kama jimbo la Chato,huwezi kujua kabila kipi ni dominant na lipi predominant,

Chato kuna
Wahangaza,wanyambo,watutsi,
warundi,waha,wazinza,wasubi,wahaya,wazinza,wasumbwa,wasukuma,na kila mmoja hujiona hapo ni kwao kwa asili.watu wa huko hufahamu lugha hizo zote,hata hayati JPM alijua hizo lugha zote japo kihistoria baba yake alihamia.

Miaka ya nyuma Chato ilikuwa tarafa ndani ya wilaya ya Biharamulo mkoa wa Kagera ,Sasa mwaka 1990 hayati JPM akagombea ubunge na mzee Phares Kabuye,alishindwa vibaya sana kura za maoni unajua kwa nini?

Jpm alikuwa akienda vijiji vyenye wasukuma anajifanya msukuma na kuwaponda wasubi kuwa ni wakulima wa migomba mbunge wao hawezi kuwasaidia wao wakulima wa pamba,hivyo wamchague yeye.

Meanwhile akienda Biharamulo anajifanya ni Msubi na kuongea Kisubi na anawaambia yeye ni ukoo wa Wayango wazilankende,ukoo ambao hauko usukumani bali kigoma ,butundi,rwanda,uganda na makabila yanayosikilizana na wahaya.hapo atajifanya msubi orijino na kuwaponda wasukuma kuwa ni wanyamahanga yaani wavamizi wa mkoa wa Kagera,

Akienda maeneo yenye waha wengi atajifanya muha na kuongea kiha na kirundi,siasa za ukabila zikamponza akadondokea pua.

Mizimu ya kwao ikamsaidia jimbo likagawanywa mashariki na magharibi 1995 akagombea mashariki ilipo kata ya Chato akajibatiza usukuma ila kuna wakati alikuwa akijisahau na kurudia kusema yeye ni myango ukoo ambao hauko usukumani,

Akagombea kwa style ileile ya kutumia vernacular languages kulingana na audience.
Akajikuta anachukiwa na makabila mengine jimboni kwake isipokuwa wasukuma.

Uwekezaji alioufanya jimboni kwake baada ya kuwa Rais ilikuwa ni kutafuta huruma na kufuta makovu ya makabila mengine na alifanikiwa maana makabila yote yalifaidi uwekezaji ule.

Lakini watu wa Biharamulo magharibi hawatamsahau kwa maana barabara ya lami oliyotakiwa kupita mjini kwao kuelekea Bukoba ilipofika kata ya Bwanga akaichepusha kuelekea Chato,Muleba kama adhabu ya kumnyima kura 1990.
Barabara hiyo ilikuja kuwekwa lami baadae baadae sana.

Utajiuliza mbona alikuwa anashinda ubunge kila mara
kama hakuwa anapendwa?
Ni kwamba ulitumika umafia na hadaa kwa washindani wake,wengine wakitishwa au kutekwa au kuahidiwa vyeo na pesa ili wajitoe kugombea nae

Hitimisho;
Ukabila upo na Hayati JPM alichukiwa jimboni kwake sababu ya mbegu ya ukabila iliyopandwa na........
Mizimu ya kwao ikamsaidia,lakini mizimu hiyo hiyo ikamkataa 2021 kwa sababu ya ubaguzi ubaguzi.
 
Kwa hiyo ndio hizi ndio sera za siasa za majukwaani mnazijiandaa nazo?
 
Wakina wewe nlioruhusiwa juzi huko Ikulu!

Wakati tunataka Sera,wewe bado una personal attacks na Mizimu [emoji22]

Kuwa na adabu basi,malaika unamuitaje mzimu
 
Kwa siasa hizi ni ushahidi tosha kwamba mmeishiwa sera!

Na amini nakuambia huko majukwaani mnaenda kuangukia pua.

Labda mjitambuwe na kujirekebisha!
Majukwaa gani mbona hueleweki,
 
Majukwaa gani mbona hueleweki,
Mkuu Mdukuzii Kwani mmeruhusiwa kufanya siasa kwenye majukwaa gani zaidi ya kwenye siasa za mikutano ya hadhara!
JamiiForums-1181595203.jpg
 
Una asili ya kaubishi MHA kaijua biashara miaka ya kalibuni kazi ya MHA ni vibalua vya kulima na kuchunga ng'ombe wa wasukuma hicho neicho kimefanya KUWA wengi ukanda huo hata baba yake magufuli kafika huko kufanya vibalua vya kulima na kuchunga ng'ombe wa wasukuma

Kwani Baba yake Magufuli ni Muha??
 
Mkuu Mdukuzii Kwani mmeruhusiwa kufanya siasa kwenye majukwaa gani zaidi ya kwenye siasa za mikutano ya hadhara!View attachment 2472056
Nikwambie kitu ndugu yangu,kwenye maswala ya kujenga miundombinu magufuli hana mpinzani,sio tanzania tu bali hata nchi nyingi za afrika,ila kwenye demokrasia na haki za binadamu alifeli sana
 
Back
Top Bottom