Kwanini Hayati Magufuli aliogopwa sana na Waandamanaji tofauti na Ruto anavyoonewa huko Kenya?

Kwanini Hayati Magufuli aliogopwa sana na Waandamanaji tofauti na Ruto anavyoonewa huko Kenya?

Ni kwasababu ya ukatili wake uliokithiri na watu walimjua huyu jamaa ni katili na hata anaweza kukupoteza katika mazingira ya kutatanisha kama akina Saanane. Ruto ni muungwana, mcha Mungu na pia Kenya kuna demokrasia iliyokomaa zaidi ya hii hapa kwetu.
Kama demonskrasia ndo hizo vurugu haifai
 
Magufuli hakuogopwa Bali alifanya kazi nzuri ambayo iliwafanya wtz wasiwe na sababu ya kuandamana.kipindi hicho mambo yalikuwa mazuri tofauti na Sasa Kila siku Nchi inaharibiwa na huyu mama
 
Maandamano ya CHADEMA yaliyoitwa UKUTA kama yangefanikiwa yangekuwa zaidi ya haya ya Gen Z.

Nakumbuka Shujaa Magufuli alitoa Kauli Moja tu " atakayeandamana asije akanilaumu" kauli hii ilitosha kuwafanya CHADEMA waufyate

Lakini hapo Kenya kila wiki Rais Ruto anatoa Vitisho vipya lakini Gen Z hawaogopi wala nini

Ahsanteni Sana 😂
Yule alikuwa mwehu!
 
Ubovu wa katiba pia ni sababu kubwa. Kenya wana katiba imara na bora kabisa inayowapa wananchi haki ya kuandamana pasipo vibali uchwara vya polisi kama ilivyo hapo Tz.

Ndiyo maana utaona kabla ya katiba mpya wananchi wa Kenya hawakuwa na uhuru kama ilivyo sasa maana utawala wa Moi ulikumbatia likatiba la tangu KANU ambalo lilikuwa bovu kabisa.
 
K
Ni kwasababu ya ukatili wake uliokithiri na watu walimjua huyu jamaa ni katili na hata anaweza kukupoteza katika mazingira ya kutatanisha kama akina Saanane. Ruto ni muungwana, mcha Mungu na pia Kenya kuna demokrasia iliyokomaa zaidi ya hii hapa kwetu.
Kwa maana hiyo JPM aliwaweza 😅😅😅🙌
 
Magufuli alikuwa real sana ndiyo maana wananchi wanyonge walimpenda.

Kumbuka masikini ndiyo hutumika kuandamanishwa
John Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania, aliogopwa sana na waandamanaji kutokana na mtindo wake wa uongozi ambao ulijulikana kwa kuwa mkali na wa kijasiri. Alikuwa na sera kali za kudhibiti upinzani na maandamano, na alitumia vyombo vya dola kama polisi na jeshi kwa nguvu kubwa kudhibiti wapinzani na waandamanaji. Pia, alijulikana kwa kutokubaliana na ukosoaji na mara nyingi alichukua hatua za haraka dhidi ya wale waliomkosoa, ikiwemo kuwakamata na kuwafunga gerezani.

Kwa upande mwingine, William Ruto, Rais wa Kenya, anaonekana kuwa na mtazamo tofauti wa uongozi. Ingawa kuna changamoto na maandamano nchini Kenya, Ruto ameonyesha utayari wa kushirikisha upinzani na kufanya mazungumzo, jambo ambalo linaweza kupunguza hofu na kuogopwa kwake na waandamanaji. Pia, mfumo wa kidemokrasia nchini Kenya unatoa nafasi kubwa zaidi kwa wananchi na wapinzani kuonyesha maoni yao na kufanya maandamano kwa njia za amani.

Tofauti hizi katika mitindo ya uongozi na sera za kudhibiti upinzani zinaweza kuelezea ni kwa nini Magufuli aliogopwa zaidi na waandamanaji ikilinganishwa na Ruto.
 
Magufuli hakuwa shujaa bali alikuwa mtu mwoga sana kuliko hata kunguru. Kwa ajili ya uwoga wake ndiyo maana kila mkutano na kila ziara alikuwa anezungukwa na IGP Sirro, CDF Mabeyo, DG IS Diwani Athman.

Halafu alikuwa na ulinzi mzito sana wa banadamu, mitambo, askari kanzu, askari wenye laptop ba helicopter

Lakini pamoja na vyote hivyo COVID-19 ikamfagia kinyama
Hauoni hivyo vyote alifanya kujilinda na mafisadi!? Na mnasingizia COVID 19 while you killed our Man ,STUPID.
 
Ruto dhaifu anachezewa sana. Hata Maza hawezi chezewa hivyo.
 
Ruto amezungukwa na watu wasioweza kuipambanua falsafa yake + wazee wa dili kama yeye, baraza lake lote la mawaziri plus timu ya mawasiliano serikalini inaendeshwa na watu wenye majigambo/dharau kwa umma, ni timu isiyo na masikio ya kusikiliza 'ground' inasema/inataka nini, mtu kama Isaack mwaura anaulizwa kuhusu safari ya president US anaishia kutukana, mkanganyiko wa maelezo kutoka kwa Ruto na Mohammed hussein kuhusu ndege iliyotumika kwenye safari ya US, wapambe walio na majivuno mfano Oscar Sudi na Kipchumba murkomen, wandani wenye lugha chafu kwa wananchi wenye mrengo wa tofauti mfano Kimani ichungwa, Dismus Barasa etc, ni mambo mengi sana yanamkwamisha Ruto. Inawezekana ana nia njema na Kenya ila amekuwa 'hostage' kwa wandani wake.
 
Back
Top Bottom