Kwanini Hela imekuwa ngumu mtaani?

Kwanini Hela imekuwa ngumu mtaani?

I agree with you, everything is imported mpaka bahasha[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ni aibuView attachment 2420328
😂
Bado hatujapata Kiongozi wa kutegua huo mtego. Wapo bize na kulamba asali na v8. China walipata bahati ya kuwa na Deng Xiaping ndio aliutegua huo mtego na ndio maana mpaka leo China ni taifa tajiri. Huko ulaya usa huo mtego waliutegua toka miaka ya 1700-1800 ndio maana mpaka leo hao jamaa ni matajiri kutokana na capitalism ideology.
 
Trade imbalance ni tatizo kubwa sana , huwezi kuwa na taifa la wachuuzi na machinga na madalali bila kuwa na real productivity ya bidhaa kuuza nje ya nchi na kusatisfy soko la ndani ukadhani unajenga uchumi hata siku moja , miaka bilioni Tz itabaki hii huu ,hakuna kutoboa kwa mwendo huu
Hata mifumo ya kiserikali au hata ya kifedha na mabenki yamekaa kimfumo wa kulazimisha watu kuwa waagizaji na umachinga kuliko kuzalisha bidhaa na huduma.
 
Systematic poverty hii daah
alie kwenye mtumo kama kifaa lazima akione, wanaoendesha mfumo vipofu na Wana injoi.
Umaskini ni ukosefu wa mtu kuwa mzalishaji yaani ubunifu zero na sio kwamba rasilimali ndio shida...hiki KITU ni maksudi kipo ili kumaintain dominion over us.
 
Hata mifumo ya kiserikali au hata ya kifedha na mabenki yamekaa kimfumo wa kulazimisha watu kuwa waagizaji na umachinga kuliko kuzalisha bidhaa na huduma.
Na ndio kazi ipo hapo ,sasa .Akili inabidi itumike kufanya transformation hapo .
Ni nashangaa sana miaka 60 hii yote tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele
 
Hata mifumo ya kiserikali au hata ya kifedha na mabenki yamekaa kimfumo wa kulazimisha watu kuwa waagizaji na umachinga kuliko kuzalisha bidhaa na huduma.
Si ndio hapo , yaani resources ya ardhi ,maji iliyopo nchi hii ilitakiwa iwe ni fursa tosha ya kuondoa tatizo za ukosefu wa ajira na hiyo trade imbalance lakini zimebaki siasa tu ,miaka na miaka ,no real action .
Badala ya mabenki kutoa mikopo ya ununuzi wa mitambo ya uzalishaji wa bidhaa kwenye viwanda na kwenye kilimo .
Eti rais anahamasisha machinga kupewa mikopo , hii akili ya mtu mweusi ni giza kabisa
Hivi nchi
 
[emoji23][emoji23]
Ngoja nikwambie ukweli. Tanzania tuna mzunguko mdogo sana wa hela. Halafu kila kitu tunaagiza. Kwa hiyo biashara tunazofanya zinafanana na zinakuwa nyingi kuliko wateja. Na purchasing power ipo chini. Kwa hiyo raia wataishia kununua daily consumables (bidhaa ambazo kila siku lazima utumie/ulipie)

Ndio maana matajiri wengi wa Bongo wanawekeza kwenye biashara ambazo kila siku mtu lazima utumie
1. Mafuta ya magari(diesel/petrol)
2. Sukari
3. Chumvi
4. Kiberiti
5. Ngano
6. Mafuta ya kula
7. Sabuni za kipande
8. Sabuni za unga
9. Usafiri na usafirishaji
10. Pedi na pampers
11. Juisi, beverages na maji
12. Pombe
13. Mitandao ya simu/bando

Nadhani umenipata. Chanzo ni mzunguko mdogo sana wa hela hivyo hela kuwa ngumu na watu kutumia hela kwa ajili ya vitu vinavyo hitajika kila siku. Unadhani kwanini bakhresa kawekeza kwenye ngano, azamtv bagamoyo sugar? Au kwa nini mo yupo bize na mafuta ya kula, sabuni za unga? Unadhani kwanini azania wamehamia kwenye sabuni ya kipande na unga? Maana yake huko kwenye sabuni za kipande na sabuni za unga ndio kuna hela [emoji23]
fact
 
Watu wako bize na kulamba asali na v8.[emoji23][emoji23]
Yaani hizo pesa wanazotumia kununua hayo magari na kufanya upumbavu wote ambao ni unnecessary huko serikalini ingekuwa ni mtaji wa kununua mitambo na kujenga miundo mbinu ya mamia ya viwanda na hata kuanzisha viwanda vya kuzalisha mitambo na vipuri
 
Kwa mara ya kwanza tangu 2017 inflation rate imefikia 4.8% and expected to reach 4.9% at the end of this year. Hii ina maana gani

1. Nguvu ya manunuzi imepungua sana kwahiyo hakuna mzunguko mkubwa wa pesa
2. Tsh itaendelea ku-depreciate against other currencies
3. Nguvu za kiume itakuwa ni changamoto sababu ya ugumu wa maisha kwa vijana[emoji3]
4. Magonjwa ya akili yataongezeka sababu ya challenge za mfuko na lindi la majukumu
5. Unemployment rate itaendelea kuwa kubwa
6. Bidhaa za vyakula, usafiri na vinywaji hazitakamatika

Mungu tuvushe salama

Picha ya kwanza ni dollar against Tsh since year 2000

Picha ya pili ni inflation rate this yearView attachment 2420326View attachment 2420327
We acha tu nahivi maji hamna inazidi kuwa ngumu zaidi yaani sio poa.
 
Systematic poverty hii daah
alie kwenye mtumo kama kifaa lazima akione, wanaoendesha mfumo vipofu na Wana injoi.
Umaskini ni ukosefu wa mtu kuwa mzalishaji yaani ubunifu zero na sio kwamba rasilimali ndio shida...hiki KITU ni maksudi kipo ili kumaintain dominion over us.
kuna ukweli hapa
 
Yaani hizo pesa wanazotumia kununua hayo magari na kufanya upumbavu wote ambao ni unnecessary huko serikalini ingekuwa ni mtaji wa kununua mitambo na kujenga miundo mbinu ya mamia ya viwanda na hata kuanzisha viwanda vya kuzalisha mitambo na vipuri
Hii kitu hapa
images%20(57).jpg
 
Back
Top Bottom