Kwanini Hela imekuwa ngumu mtaani?

Unajua wapi tungeanzia? Bwawa la Nyerere lingalitoa umeme wa uhakika lakini kwa bei ndogo ili bidhaa tutakazotengeneza hapa nchini ziwe rahisi. Usafirishaji wa Malighafi (SGR) kama nayo isingechakachuliwa ili uwe wa bei ndogo.
 
Hali ya maisha mtaani imekuwa ni tete kwa kweli. Mzunguko wa biashara uko chini sana.

Fedha kwa sasa haina thamani kutokana na bei ya bidhaa nyingi muhimu kupanda bei kupitiliza kiwango cha kawaida. Halafu kibaya zaidi haipatikani kirahisi! Ukiipata, inaisha kirahisi rahisi tu!!

Ukiondoa hiyo vita ya Urusi na Ukraine, kwa mtazamo wangu naona pia kitendo cha hii serikali ya huyu mama kuja na hi mitozo yao isiyo na kichwa wala miguu! Na yenyewe imechangia pakubwa sana kuyafanya maisha ya wananchi wa kawaida kuwa magumu.
 
Bongo inflation rate 4.7% na US rate 8.2%, hizi number mnazorushiwa na Kina Mwigulu sijui wanazitoa wapi, idara za serikali au viongozi bongo hawajui hata wanaongea nini, sitashangaa inflation rate kwa bongo inazidi 40%
 
Mimi siamini pesa hipo kwa wanao tafuta na hakuna hali nzuri wala mbaya kwa nchi yetu hii tangu enzi za nyerere mpaka sasa walikuwepo na pia hata sasa wapo walalamishi lakini wanao fanikiwa wapo pia tena wengi cha msingi ni kuzidi kutafuta bila kukata tamaa, hali aitakuja badilika ata aje nani.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi
 
Hiv Deng Xiaoping aliwezaje
 
Hatari sana
 
Unajua wapi tungeanzia? Bwawa la Nyerere lingalitoa umeme wa uhakika lakini kwa bei ndogo ili bidhaa tutakazotengeneza hapa nchini ziwe rahisi. Usafirishaji wa Malighafi (SGR) kama nayo isingechakachuliwa ili uwe wa bei ndogo.
Bwawa la Nyerere lingekamilika kama ilivyopangwa, kisha SGR nayo ikawa networked kama ilivyokuwa imepangwa ingekuwa ni hatua kubwa sana za mwanzo mwanzo kujinasua kaa taifa.

Maana production ingekuwa na gharama ndogo, mizigo ingekuwa inatembea harakahaka within a country, nchi ambazo zinaingiza mizigo yake kupotia bandari ya Dar ingeongeza kiwango cha mizigo inayopita nchini....daah ngoja niishie hapa tu, kiufupi uchukuzi na uzalishaji vingelipuka kwa kiwango kikubwa sana.
 
Kweli mzunguko hamna, watu na vibiashara vyao huku mtaani utawaonea huruma, kila siku wanafungua na zinakufa ndan ya muda mfupi.
Juzi nikawasikia et mtaa huu una laana [emoji3][emoji3]
Akili ya mtu mweusi huwa ikikosa majibu inawazia muujiza kutoka katika matatizo.

Mfano biashara imekuwa ngumu au imekwama, wazo lake la kwanza ni kuwa amelogwa badala ya kusema atafute mbinu ya kusurvive.
 
Na kwa idadi ya wamachinga iliyopo ni wazi wanategemea uagizwaji wa bidhaa ziwe ni za kitumba au mpya toka viwandani kuja kuziuza.
 
Kinachotusaidia watz sehemu kubwa ya bidhaa kama chakula tunapata direct kutoka shamba na hiyo inasaidia kushusha sehemu kubwa ya gharama za matumizi kama manunuzi ya bidhaa za matumizi ya familia.

Ila tungekuwa tunatumia 100% bidhaa za viwandani kama chakula kununuliwa supermarket nadhani by sasa watu wasiweza ku escape chochote na maisha yangekuwa magumu sana.

Kwa sasa life ni ngumu sana especially kwa watu wenye familia kubwa. Chakula kipo ila kimepanda bei kumaanisha mzigo wa kulisha familia unaongezeka kila siku.

Bidhaa za chakula cha msingi kama unga, maharage, mchele, mafuta ya kupikia, vinapopanda bei watu wanakuwa katika hali mbaya sana.

Kama jamii ya watanzania hebu tuje na wazo zuri la kuweza kutoka hapa kwa namna yoyote na kuweka mbinu kinga za kuzuia upumbavu na ushenzi kama huu kufanyika tena kwenye taifa letu pendwa.
 
No 3 ni hatari. January inakuja. wenye watoto schools hata mshtuko hatuuoni
 
Kupanda vitu bei, ina maana vitu vimeadimika au vimekuwa vichache na mahitaji ni makubwa; cha kufanya kwa sasa kwa upande wa kilimo, kila mmoja ajitahidi angalau kulima ekari mbili za nafaka ili kuongeza wingi wa chakula.
 
Kupanda vitu bei, ina maana vitu vimeadimika au vimekuwa vichache na mahitaji ni makubwa; cha kufanya kwa sasa kwa upande wa kilimo, kila mmoja ajitahidi angalau kulima ekari mbili za nafaka ili kuongeza wingi wa chakula.
Shida ni kuexport kiwango kikubwa cha mazao kuliko uwezo wetu wa kuzalisha.
 
Hela ikiwa ngumu ktk taifa ndy uchumi utapanda .sababu watu watazidi kuzalisha maradufu jli kuitafuta pesa .lkn kwa Tz naona tuna relax kabc .hizi pigo zakutafuta hatuna !! [emoji848] sielewi vijana tunakwama wp
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…