Ukiwa na shiling elfu kumi Tanzania utanunua vitu vingi lakini ukichukua hiyohiyo elfu kumi ukaenda nayo kenya hautonunua vitu vingi kama ulivyonunua Tz so thamani ya shiling ikiwa ndogo kuna faida saana (hasa kwa nchi zinazozalisha bidhaa nyingi)
Ndugu yangu, thamani 'halisi' humtegemea zaidi muhitaji wa pesa yako, ili akapate 'vile' anavyohitaji yeye kwa wakati huo.
Kuna wakati BAADA ya uhuru nchi zetu EA (Ke,Tz,Ug) zilitumia hela moja, SHILLING.
Hata baada ya kutengana kwa muda mfupi hali ilikuwa muzuri, Ushs =Kshs =Tshs.
Soko letu kuu kwa nchi zetu lilikuwa moja. Viwanda katika nchi zetu vilianzishwa kimikakati ya kuimarisha umoja/ushirikiano na sio migongano/mipambano.
Migogoro mingi ambayo baadae ilikua na kukuzwa sana, hatimae ilikuja sababisha kuvunjika kwa EAC na ndio iliyotufikisha hapa.
Kutokana na historia viwanda vingi vya mahitaji muhimu ya kila siku kama sabuni, dawa ya meno, mafuta ya kupikia etc vilikuwa Kenya. Hivyo basi Kshs ikawa ndo yahitajika zaidi kwetu na hata kwa Uganda, ili kupata hayo mahitaji (muhimu).
Pamoja na Tz kuamua kufunga mipaka na
kukimbizana kuanzisha viwanda mbadala na kuingiza baadhi ya bidhaa hasa kutokea China, ili kuziba mapengo, bado biashara ya kuingiza mahitaji kutoka Kenya kimagendo ilishamiri na kuifikisha thamani ya Tsh hapa ilipo.