Kwanini Herod Antipas aliitwa Mbweha na kwanini watu wa Mataifa wanaitwa Mbwa?

Kwanini Herod Antipas aliitwa Mbweha na kwanini watu wa Mataifa wanaitwa Mbwa?

lugha katika masuala ya dini imejaa kauli za kiubaguzi. hili linanikera sana. utasikia wakristo wanawaita wengine wapagani mara waislamu wanawaita wnzao makafiri.
Biblia hai-support ubaguzi wala maneno ya dharau. Katika maandiko yafuatayo tunafundishwa jinsi ya kutumia lugha au ndimi zetu vizuri:
Waefeso 4:29 (BHN)
Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na yanayojenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.

Wakolosai 4:6 (BHN)
Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.
 
Majina ya wanyama katika Biblia ni lugha ya picha iliyotumiwa kama kielelezo cha tabia, nafasi, au hali ya kiroho. Ni muhimu kuyasoma kwa muktadha sahihi wa kitamaduni na wa kimaandiko. Hii inasaidia kuelewa vizuri mafundisho ya Biblia na jinsi Mungu anavyowasiliana na watu kwa lugha inayoeleweka kwa wakati huo.

Mara nyingi katika tamaduni za Mashariki ya Kati, watu walipoitwa kwa majina ya wanyama, lengo halikuwa kutukana, bali kuelezea tabia, uwezo, nafasi au hali fulani ya kiroho ya mtu. Hii ni tofauti na nchi nyingine ambapo majina ya wanyama hutumiwa na watu kama matusi.

Hii hapa baadhi ya mifano katika Biblia inayoonyesha jinsi majina ya wanyama yalivyotumika kwa namna ya heshima au ya kiakili, kulingana na muktadha:

1. Yesu anaitwa "Simba wa kabila la Yuda" (Ufunuo 5:5). Hili ni jina linaloonesha mamlaka, ujasiri, nguvu na uongozi. Simba alijulikana kuwa mnyama mwenye nguvu na anayeheshimiwa sana katika jamii. Kwa hiyo, jina hili linamtambulisha Yesu kuwa ni Mfalme mwenye nguvu.

2. Herod Antipas aliitwa Mbweha
Yesu aliposema, “Mwambieni mbweha huyo…” (Luka 13:32), hakumtukana Herode bali alimtaja kwa sifa yake ya hila na ujanja ujanja. Katika jamii za Mashariki ya Kati, mbweha alionekana ni mnyama mjanja, asiye na nguvu na ujasiri wa kweli kama simba. Kwahiyo, watu waliokuwa wakifikiri kwamba Yesu alimtukana Herod Antipas, nadhani wamepata jibu hapa.

3. Shetani anaitwa nyoka kwa sababu alijivika umbo la nyoka ili kumjaribu Eva katika bustani ya Edeni. Katika Biblia, nyoka anawakilisha hila, udanganyifu na uovu — sifa alizo nazo shetani.

4. Yesu alipomwambia mama Mkananayo, “Si vema kuwapa mbwa chakula cha watoto,” (Mathayo 15:26), hakumtukana. Katika muktadha huo, ‘mbwa’ ni jina lililowakilisha watu wa Mataifa (wasio Wayahudi), waliokuwa nje ya agano la Israeli kwa wakati huo.

5. Katika Mathayo 25:31–46 Watakatifu wanaitwa Kondoo na wenye dhambi wanaitwa Mbuzi. Nadhani hakuna asiyejua sifa au tabia za kondoo na mbuzi.
Ni mbwa kwa sababu walipwakia vitu visivyo vyao kama mbwa. Ndiyo maana waarabu na wayahudi wanatubagua sana ukiachia mbali wazungu waliotumia biblia kuitawala dunia.
 
Biblia hai-support ubaguzi wala maneno ya dharau. Katika maandiko yafuatayo tunafundishwa jinsi ya kutumia lugha au ndimi zetu vizuri:
Waefeso 4:29 (BHN)
Maneno mabaya hata yasisikike kamwe miongoni mwenu; kila mara maneno yenu yawe ya kufaa na yanayojenga na kuwasaidia wengine, ili yawaneemeshe wasikilizaji wenu.

Wakolosai 4:6 (BHN)
Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa daima mema na yaliyokolezwa kwa chumvi na ya kuvutia, na mnapaswa kujua jinsi ya kumjibu vizuri kila mmoja.

Dini zote za kigeni zinaendeshwa kwa misingi ya kibaguzi na kinyonyaji. Yesu anaonyeshwa akiwa mweupe hata kama hakuwa au hata sijui kama alikuwapo. Muhammad anasema watakaoingia peponi nyuso zao zitakuwa nyeupe wakati watakaoingia motoni nyuso zao zitakuwa nyeusiوَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱبْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِى رَحْمَةِ ٱللَّهِ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ ١٠٧ tafsiri​

As for the bright-faced, they will be in Allah’s mercy, where they will remain forever.​

Narrated 'Abdullah: The Prophet said, "I saw (in a dream) a black woman with unkempt hair going out of Medina and settling at Mahai'a, i.e., Al-Juhfa. I interpreted that as a symbol of epidemic of Medina being transferred to that place (Al-Juhfa)."​

Mbona umesema Dini zote lakini umenukuu maneno ya Dini moja!
 
Duh, poleni sana. Inaonekana Mungu hayuko upande wenu. Vinginevyo kwanini mambo yenu hayafanikiwi? Angalieni ni wapi mlipoanguka, mkatubu(Ufunuo 2:5)
Si Kweli. Usitafsiri maandiko vibaya
 
Si Kweli. Usitafsiri maandiko vibaya
Maandiko yanasema: "ombeni nanyi mtapewa." Sasa ninyi mbona mnaomba lakini hampati? Kikwazo kimojawapo cha kutokujibiwa maombi ni dhambi.
 
Ni mbwa kwa sababu walipwakia vitu visivyo vyao kama mbwa. Ndiyo maana waarabu na wayahudi wanatubagua sana ukiachia mbali wazungu waliotumia biblia kuitawala dunia.
Biblia ni kitabu muhimu sana. Kingekuwa hakina maana, baada ya ukoloni watu wasingeendelea kukitumia. USA mauzo ya Biblia yameongezeka sana nyakati hizi.
 
Back
Top Bottom