Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
uchumi unaporomoka kwa kasi na kushusha soko kwa spidi mbaya...............note that am not mtaalamu
Mbona NMB na KCB hazishuki hivyo why CRDB tu?
Ni kweli hisa za CRDB na za TWIGA zimeshuka,kwa twiga najua sales yao imeshuka sana
kutokana na other competitors wamekuja na price za chini kdg.Kwa crdb labda kimei aje atuambie
It's all about their financial strategy in terms of mix of debt,earnings and payment of dividend
Dar es Salaam Stock Exchange (DSE),ipo Jubilee House karibu na PPF tower!Hisa za crdb zinauzwa WAP
Kushuka kwa dhamani ya hisa za CRDB zimesababishwa na kuongezeka kwa hisa zilipelekwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa,ukilinganisha na mahitaji halisi ya hisa zinazohitajika sokoni!(Refer to the law of demand and supply in determination of price)!Hili ni zao tu,cha kujiuliza hapa ni kwamba,kwanini watu wengi wamepeleka hisa zao sokoni?
Kulingana na utafiti mdogo nilioufanya (As financial analyst) ni kwamba hivi karibuni CRDB wametoa taarifa zake za fedha kwa robo ya pili ya mwaka,ambazo kwa upande wa faida ,benki imepata faida ya Tshs 20.04 bilioni ukilinganisha na Tshs 16.51 bilioni iliyoipata kwa robo ya mwaka iliyotangulia,hii ni sawa na ongezeko la aslimia 24.Ukija kuangalia suala la mikopo ambayo hailipwi kumekuwa na ongezeko kubwa kutoka Tshs 124.169 bilioni mpaka 139.307 bilioni jambo ambalo si zuri kwa kampuni (Source:CRDB published information for second quarter).
Kwa kuwa wanahisa kwa kushirikiana na financial analysts na brokers, huwa wapo very sensitive na hizi taarifa za kifedha wengi wameshauriwa kuuza hiza zao kwa kuwa benki imeonyesha uzembe mkubwa katika ukusanyaji wa madeni,na hivyo kuhatarisha its going concern(Uwepo wake kwa siku zijazo).
Naomba kuwasilisha wanabodi!
Nashukuru mkuu,tupo pamoja!Nashukuru kwa malezo ya kina mkurugenzi TUKUTUKU.
Mi nilijua kua yawezekana benki imepata hasara na ndio mana hisa zimeshuka kumbe faida imepatikana isipokuwa bad debts zimeongezeka.
Technically you have unlocked the puzzle.