hekimatele
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 9,890
- 2,795
TUKUTUKU naomba jibu na wanabodi wengine tafadhali.Kushuka kwa dhamani ya hisa za CRDB zimesababishwa na kuongezeka kwa hisa zilipelekwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa,ukilinganisha na mahitaji halisi ya hisa zinazohitajika sokoni!(Refer to the law of demand and supply in determination of price)!Hili ni zao tu,cha kujiuliza hapa ni kwamba,kwanini watu wengi wamepeleka hisa zao sokoni?
Kulingana na utafiti mdogo nilioufanya (As financial analyst) ni kwamba hivi karibuni CRDB wametoa taarifa zake za fedha kwa robo ya pili ya mwaka,ambazo kwa upande wa faida ,benki imepata faida ya Tshs 20.04 bilioni ukilinganisha na Tshs 16.51 bilioni iliyoipata kwa robo ya mwaka iliyotangulia,hii ni sawa na ongezeko la aslimia 24.Ukija kuangalia suala la mikopo ambayo hailipwi kumekuwa na ongezeko kubwa kutoka Tshs 124.169 bilioni mpaka 139.307 bilioni jambo ambalo si zuri kwa kampuni (Source:CRDB published information for second quarter).
Kwa kuwa wanahisa kwa kushirikiana na financial analysts na brokers, huwa wapo very sensitive na hizi taarifa za kifedha wengi wameshauriwa kuuza hiza zao kwa kuwa benki imeonyesha uzembe mkubwa katika ukusanyaji wa madeni,na hivyo kuhatarisha its going concern(Uwepo wake kwa siku zijazo).
Naomba kuwasilisha wanabodi!
Kama mikopo ambayo hailipwi imeongezeka na still benki imepata faida, hiyo faida imetoka wapi ukizingatia one of the core business and income ya any bank ni interests from loans?
Last edited by a moderator: