Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nipo mupenzi mbona umenitupa hivyo ?upo we mtu?
Habari wanajamvi.
Kwa kweli hilo swali huwa linanisononesha sana.
Nina umri wa miaka 30, sijaolewa, sina mchumba wala mpenzi yapata mwaka na miezi kadhaa sasa.
Mdogo wangu anayenifuatia ana miaka 27 aliolewa akiwa na miaka 24 na ana watoto wawili sasa.
Familia yangu na jamii inayonizunguka hainielewi na mara nyingi nakutana na hilo swali
"Mbona wenzako wanaolewa wewe huolewi, au una tatizo?"
Kiukweli hua napata ugumu sana kujibu hilo swali kwa sababu sina cha kuwajibu.
Labda ningesema nina tatizo au kasoro lakini kati ya niliowahi kuwa nao kimahusiano hakuna alieoa hadi sasa japo wote walinizidi umri na kuna wawili walikua na watoto tayari na mpaka sasa hawajaoa.
Hivi kwa jamii yetu mwanamke kutoolewa ni kasoro?
Maana kuna rafiki yangu naye anapata usumbufu kama wangu kutoka kwa familia yake.
Vipi kama mwanaume ninayempata yeye hana wazo la kuoa nifanyeje?
Na wanaume huwa wanaulizwa na kuonekana wana matatizo kama wanawake?
Kuolewa sio issue sana ila kwa jamii yetu eti usipoolewa may una matatizo sio kweli bana.
Pole ila usijali watu wanaolewa na 40yrs wala isikutishe my dear
Chwechwe unasambaza mbegu tu,malezi watahangaika nayo wenyewe we kiboko...cku hiz kuolewa cyo inshu tafuta m2 au ntafute mimi nikutie mimba ukishajifungua lea mtoto wako mwenyewe .....maisha yanaendelea
Nipo mupenzi mbona umenitupa hivyo ?
Dada angu pole sana kwa mawazo mabaya ulojiwekea na unawaza sana sababu wewe mwenyewe unapenda upate mchumba uolewe lakini inakuwa sivyo, embu jiulize maswali kwanza kwa nini unaokuwa nao hawakukuuliza swali hilo? pengine kuna kitu kinawakwaza bila ya wewe mwenyewe kujua, relax kila kitu kitakuja chenyewe wakati ukifika wala usiumie roho kuona mdogo wako alishaolewa, pia siku hizi kutaka kusoma kwanza wasichana wengi wamejikuta wana madegree kibao then wanatafuta wachumba wa kuwaoa miaka inakuwa imeenda sana mwishoni unajikuta kwenye situation ambayo unajiona umechelewa. mimi naona umri wako bado upo freshutapata tu mchumba
not in africa
usijilazimishie kuolewa tena hiyo miaka sio tishio kiivyo.
Mwombe Mungu utapata wa kukufaa.