Dada Pretty miaka 30 ni mingi ndugu yangu mtu asikudanganye na anekuambia kuolewa sio issue inamaana anataka uwe malaya au utembee na wanaume za watu? kutokana na maelezo yako Kama unavyodai majamaa zako wa nyuma wote bado hawajaoa mimi navyoona huo ni mkosi au nuksi shost kukutana na mijinaume ambayo sio mioaji mfululizo mhh! sasa fata ushauri naokwambia Kama nikuomba mungu omba mungu akuondolee nuksi ya kutokuolewa kwanza ikishatoka ndio uombe mungu akuchagulie mume, pili nina wasiwasi una jini mahaba lina kupeleka kwa wanaume wasiofaa ambao pia wao wana hayo majini shost piga vizuri Kama wewe ni mkristo kemea jini mahaba kwa kwenda mbele mama la sivyo unazeeka kumbuka kuna kuna kuzaa na watoto ni hazina maishani usijidanganye ukazaa bila kuolewa huko nikujidhalilisha yaani ukae miaka yote hiyo 30 halafu uje uzae bila kuolewa usikubali wanaume wapo kibao wanatafuta wanawake wa kuoa hawawaoni kwani una kasoro gani chakarika mwaka huu usiishe shost
Nimerudi.
Loly mpenzi,
1. miaka 30 ni mingi ukimaanisha nini?ni wapi imeandikwa mtu aolewe kabla hajafika 30 years?hapo naona umekosea kidogo
watu wanaolewa wakiwa hata na miaka 40 na kupitiliza, binafsi nadhani hakuna umri maalum ambao mwanamke anapaswa awe amekwisha olewa.
2. kuwa na majamaa ambao wao pia hawajaoa haimaanishi una nuksi...wao wana maisha yao na wewe una maisha yako..ni kama kufananisha kifo na usingizi.
3. kwa uelewa wangu,muanzapo mahusiano hamuanzi kwa kuambiana 'oo nitakuoa''au 'oo nioe'...hell no...kuoa kunakuja kama mmeridhiana,kama mnapatana,je mnaweza kuvumiliana and all that..mi sijaolewa so siwezi kuweka list ndefu hapa...kwahiyo yawezekana Da Pretty hao aliokutana nao huko nyuma (i) hawakuwa na nia ya kuoa na ndo mana mpaka leo hawajaoa (wapo wanaume wa hivyo na ninawafahamu,wao wanajiita senior bachelors)...au (ii) hawakuridhia mpaka kufikishana kuoana and vice versa its true
4. Imeandikwa kuwa 'Mume bora hupewa na Mungu'..kwa hiyo kumshirikisha Mungu kwenye maombi ni jambo la muhimu na busara pia, ingawaje sidhani kama majini sijui mahaba have nothing to do with ndoa
5. Kama usemavyo 'watoto ni hazina'..na hii kumbuka haijalishi kama umeolewa au haujaolewa,hazina ni hazina tu with or without marriage so hata akiamua kuzaa sasa hivi hatojidhalilisha kama ulivyosema (ingawaje jamii itaona amejidhalilisha)
6. Mbona wanawake wa kuoa wengi tuu,kwanza wanawake ni wengi kuliko wanaume iweje wanaume wasione wa kuoa.Mi naona hao wasioona ni kwamba hawako tayari kuoa na kujisingizia hawajaona hawana lolote
Angalizo
Yatupasa tuishi bila kujali jamii inasemaje,jamii inaonaje au jamii itakuchukulia vipi.
Da Pretty, miaka 30 sio mingi, usiharakishe kuolewa kama hauko tayari au kama hajatokea the right person to marry you just because jamii inakuonaje..Waache waulize,waseme, watajijua wenyewe,yao yanawashinda kwa nini wakuulize wewe? Kama ni mama zako,wakalishe kitako waambie bado hauko tayari au hujapata unaedhani anakufaa.kwani tatizo liko wapi hapo? at the end of the day wewe ndio utakayeishi na huyo mume,wacha upate anaefaa bwana hee!!take your time dada,chagua if u have to pembua upate unayemtaka..usiforce mambo kisa watu wanasemaje..wama maisha yao yanawasubiri kuishi ukute yameshawashinda..eboo..achana nao.