Kwanini huolewi? Au una kasoro?


Maswali yako ni mazuri sana na yanajenga.
Ninaishi maisha ya kawaida sana kama binti mwenye Kumjua Mungu, nina kabila na nina wazazi pia.
Suala sio kutaka kuolewa, kikubwa ni hili swali "kwanini huolewi?" ndio linanikwaza.
 
labda na wewe utuambie kwa nini hujaolewa, hupendi au hujapata muoaji mnaeendana?
Ongeza au kwa vile sijaamua kwa sasa (Inawezekana napenda ila sijawa tayari)

Tunarudi palepale!
Lazima jibu lipo kati ya hayo lakini kwanini jamii isielewe au isisikilize kwanza wahisi ni tatizo au kasoro?
 
Naomba nieleweke.
Suala la kwa nini sijaolewa haliniumizi kichwa.
Tatizo kuulizwa na jamii kuona ni tatizo mimi kutoolewa.
Ningekua na hamu sana ya kuolewa ili niifurahishe jamii wala nisingepata tabu
Ni suala la kutafuta kijana yeyota na kumshawishi hata kwa pesa ili tukafunge ndoa jamii ijue nina mume
matatizo katika ndoa ni suala jingine ambalo kwa mimi ambae nitakua nimeolewa kufurahisha jamii suluhisho ni jepesi sana
TALAKA.
Na hili swali halipo kwangu tu, kuna rafiki yangu nae anaulizwa sana tena yeye ana hali mbaya maana hamu ya kuolewa kweli anayo sana.
 
Kuolewa sio issue sana ila kwa jamii yetu eti usipoolewa may una matatizo sio kweli bana.

Pole ila usijali watu wanaolewa na 40yrs wala isikutishe my dear

Hadithi hadithi ? Hadithi njoo, uwongo njoo, utam kolea.
 
Nakubaliana na wewe. Human being is a social animal. It matters what the society is perceiving you. Kusema usijali watu wanasemaje nakataa kabisa. Piga maombi Mungu atakupatia mume mwema. Hata hao westerners kutokuolewa au kuolewa late ni culture yao na si lazima kila cha mzungu ni kizuri. Wewe mwenyewe umesema unajisikia vibaya unavyoulizwa na watu kwa nini huolewi. Kwa sababu unahisi umepungukiwa na kama ungehisi its okay usingeleta hii mada hapa. Jamii yetu haikubaliani na mtu kuchelewa kuoa au kuolewa. As long as uko Tz tegemea maswali kama hayo kila siku.

Ushauri wangu, stop hanging out with wrong guys. Wa kukuoa utamjua tu hao wengine wanakuzehesha tu.

 
Ogopa sana ushauri wa watu ambao hawana evidence nikiwa na maana hawana ushuhuda. The effect of not getting married or marrying late utaijua 20 years to come not now. Pale ambapo umestaafu watoto wanadai school fees. Au pale ambapo umezaa na mume wa mtu watoto kakunyang'anya na hawakutambui kama wewe ndo uliwazaa. Wadada wengi hawaliangalii ili la kunyang'anywa watoto wanaozaa na wame za watu. Na sheria inasema mtoto ni wa baba. Kuna dada alizaa na lawyer tajiri sana watoto wanasoma UK na walichukuliwa kwa mama yao wakiwa wadogo sana baba akawaficha boarding, wanamuona mama yao kama kinyago kwani hajawalea na wao ni matawi ya juu.
 
Kuna mtu niliona anashauri kama unataka kuwa single parent ununue mbegu. I think that could be a solution kuepuka kunyang'anywa mtoto. Tabu inakuja pale mtoto atakapokusumbua baba yangu yu wapi. Pili ni immoral hasa kwa mtu wa dini.
 

...pole sana, hii inatokana na matarajio ya jamii inayokuzunguka.
Tamaduni, mila na desturi zina "wasuta" ndugu, jamaa, na marafiki zako
kiasi kwamba wanashindwa kujizuia kukuuliza kwanini huolewi.
Kwa wengi wetu (wabantu), mfumo wa maisha unakutarajia uolewe na uzae kabla hujavuka miaka 30 - 35.

Umri unavyokimbia ni viashiria bahati ya kupatikana waoaji inapungua, na hata afya ya uzazi inapungua.
Wanapohoji kwanini huolewi, indirectly wanahoji kwanini "hutaki" kuolewa. Umegusia kwamba

Ongeza au kwa vile sijaamua kwa sasa (Inawezekana napenda ila sijawa tayari)
Tunarudi palepale!
Lazima jibu lipo kati ya hayo lakini kwanini jamii isielewe au isisikilize kwanza wahisi ni tatizo au kasoro?

Je, hao wanaokuuliza pia unawajibu hivyo -HUJAWA TAYARI?
 
<p> </p>
<p>&nbsp;</p>

dada sijakuelewa unavyosema wengine wanalazimisha, Nani kakudanganya ukimlazimisha men akuoe anakuoa pole. msipende kujifariji kupitia ndoa za watu sio kila mtu anaeteseka ndoani kwahiyo kisa ndoa za watu wengine zinavunjika ndio kigezo cha wewe na dada Pretty kutokuolewa?
 


Dah,tatizo hatuna ID za ukweli humu!

Kuna mtoto wa ant yangu,yuko 30 saivi na mdogo wake wa mwisho 23 kaolewa ila yeye bado!

Huwa natamani kujua kwanini ila ni swali ambalo anajua mtu mwenyewe!

Na kwako pia,unajua mwenyewe kwanini haujaolewa ,....maybe kila unae mpata anaona ni "gharama" kuishi na wewe,.....au labda "huoneshi kuwa na upendo kwa wandugu"......

Kwa mfano,huyu sis angu hata ningekuwa mimi ndo muoaji nisinge muoa,maana ni mtu wa yeye kama yeye tu,...sidhani kuoa mtu kama huyo atataka hata kumuona mamako akikutembelea achilia mbali wadogo zako!

Vitu kama hivyo vina repel waoaji ila vina attract wachezeaji kwa wingi na wengi tukishajua unataka kuolewa kwa ham kweli basi tunaingia na gia ya kuoa,kukisha cheza kimtindo tunaondoka!

Ila sister,Mungu peke yake ndo anaijua kesho yako,...kama uko single leo na umejiheshimu all that way (kiimani,kama hukuwahi kuiba waume za watu au kama uliiba basi repent) basi Mungu atakupa mume kwa mda anao ona unafaa maana anajua spear ya kila kiungo chako (na nani anakufaa kama mume pia)

Salute
 

Endelea tu kumdanganya mwenzako....na wewe pia subiria ifike hiyo miaka kama utatafutwa...hao watoto uzae lini na uolewe lini????mshaurini mwenzenu vizuri na sio kumpa mawazo ambayo hayata msaidia....miaka 30 unasema mda bado......au hata 40 nani kakuambia bana???miaka 40 na watoto lini???
 

Barikiwa sana!!! Nimepata furaha ya ziada kwa haya maneno yaliyotoka kwenye moyo wako. Namshukuru Mungu kwa ajili yako pia. Endelea kusonga Mbele.
Thanks again!!!
 

Kila mtu ameitwa hapa duniani kwa jinsi yake. Sio lazima kila mtu apite hapa duniani kama utaratibu wa dunia ulivyo. Cha msingi ni kutulia na kutengeneza uhusiano wako na Mungu tu. Ikiwa Mungu amekuandikia kuolewa utaolewa tu, kama hajakuandikia atakupa furaha na Neema ya kupita hapa dunia kwa njia hiyo aliyokuandikia pia.

Kumbuka sio kweli kwamba Ndoa ndiyo furaha ya mwanadamu asilimia mia moja, wakati mwingine nikujitoa sadaka tu, kuna watu wanajuta kuolewa. Kwa hiyo hapo hakuna kulazimisha mambo wala kuolewa kwa sababu fulani kasema. Ishi maisha yako mheshimu Mungu wakati ukifika itakuwa.

We unajua je bwana, yawezekana yeye ameitwa kuishi maisha kama hayo hapa duniani. Tunasahau kama sisi ni wasafiri na wapitaji tu hapa??? Yani tunadhani kila mtu lazima apite hapa kama wewe na mwingine walivyopita?? Nooooo kila mtu ana njia yake.

Dada usife moyo wala usikate tamaa, songa mbele, fanya kazi kwa bidii. Maisha yaendelee!!
 

Loly,naongea from what i've seen.kuna rafiki yangu alilazimisha kuolewa mwanaume hataki ye anatumia kigezo wamekaa muda mrefu,mwanaume akaoa akaweka ndani akaendelea na mambo yake..matokeo yake dada wa watu hakuweza kuvimilia viroja alivyokuwa anafanyiwa akaomba divorce..sasa hapo imesaidia nini?au kwa kuwa itabaki historia kuwa aliolewa..acheni kudanganyana jamani.kuolewa ama kutoolewa kumepangwa na Mwenyezi Mungu..
 
Omba Mungu akusadie utapata tu usikate tamaa
 

Ok sawa nimekueelwa vizuri kabisa na wala hamna tatizo wangu....kwa hiyo labda aendelee kusubiria mpaka atakapo pata mwanaume mwema.....ila zaidi ushauri wako nimeupenda.......
 
<p> </p>
<p>&nbsp;</p>

ndio maana nilimshauri akemee .... mahaba likishatoka atapata mchumba muoaji sio Kama wale wa zamani, sijamshauri ang'ang'anie wanaume mimi, namkizidi kuwa wabishi mtagonga 40yrs
 

Kumbe jeuri hivyo, kaa hivyo hivyo usije sababisha pressure kwa mme atakayekuoa, na ni vema uhamie Ulaya kabisa ili usionekane wa ajabu kwani kwa Afrika haikwepeki kuonwa wa ajabu. Ni vugumu kuwa anti-social halafu utarajie kuchekewa. Ulaya wenzio mpaka anazeeka ana faili la talaka nane au zaidi kwani wao kuolewa ni kama kununua soda tu, haina thamani, fanya hima ukajiunge nao.

Nimefuatilia mchango yako hapa kwenye thread yako na hii ndio conclusions yangu, I am sorry!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…