Ni mjinga pekee ndo anayo mawazo ya kijinga kama hayo,utakuta msomi mzima anatumia kitabu Cha Water Rodney ku-justify kuto endelea kwa Waafrika,kumbe mchawi wa maendeleo ya bara la Afrika ni mwafrika mwenyewe.
Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania BWM. kwenye kitabu chake,anakiri wazi kutumia pesa ya umma kugharamia kampeni za uchaguzi za CCM ,sasa hizi ni akili au ujinga wa mtu mweusi au alishauri na wazungu?
Hivi ni mzungu ndo huwa anawashauri watawala wa kiafrika kuiba pesa za umma na kupeleka kwenye ma-bank ya ughaibuni,kama alivyofanya San Abacha wa Nigeria,hapa kwetu tu ni shida mara Tegeta-Esrow,EPA, Richmond nk.
Hivi ni mzungu ndo hutoa ushauri kwa watawala wa kiafrika kuandaa maigizo na ujinga wa kisiasa wa kuandaa chaguzi za marudio,ambapo pesa nyingi hupotea uko, mfano ni kipindi cha JPM katika ile hatua ya "kuunga mkono juhudi".
Hivi mzungu ndo huingia mikataba ya hovyo ya kuuza rasilimali hovyo za taifa,mfano Mzee Mwinyi na kashfa ya kuuza Loliondo,Kikwete- gesi na Samia-bandari.
NB: wazungu hujenga matundu ya vyoo katika shule za waafrika ambapo watawala wameshindwa,lakini muda huo huo watawa wa kiafrika wanaagiza magari ya kifahari ya V8 ,toka Japan.