Kwanini huwa tunaamini kuwa wazungu ndiyo wametudumaza tusiendelee?

Kwanini huwa tunaamini kuwa wazungu ndiyo wametudumaza tusiendelee?

... kwanza ni kwa sababu tuna udumavu; na kwa kuwa viongozi ni sehemu yetu nao wana udumavu; na kwa udumavu huo hawawezi kufikiri nje ya box; wanatuaminisha hivyo na kwa udumavu huo tunaamini and the vicious cycle continuous over and over!
 
Mchina katawaliwa lini na mzungu?
Zama zetu kupata taarifa kama hii ilikuwa ni kama haiwezekani kabisa, Lakini Kwa Sasa swali kama hili halistahili kuulizwa!!


Nenda kagugo!!
 
Kwa sababu ni kweli!!….
Dhana nzima ipo kwene ukoloni mamboleo! Ni rahis sana mtu kubeza hili kama hajui ukoloni mambo leo!!….
-Usione kuna mapinduzi ya kijeshi ( fatilia utakuta aliyepindua alipata mafunzo USA, sijui Europe-Je bado una hisi ni coincedence)

-Mikataba mibovu isiyo na masilahi-(Economic Hitman)
-Madikteta wa muda mrefu ambao wanasave maslah ya wazungu ( kwa kigezo cha kuachwa madarakani muda mrefu)

-kuuliwa kwa viongozi wenye maono na watetezi wa raia wa nchi zao ie Patric Lumumba,Thomas sankara etc

-Kutumia organization kubwa kucontrol uchumi ie IMF,World bank
-Mikopo yenye mashart magumu ie IMF nk

INGAWA KUNA PART AMBAYO VIONGOZI WETU NAO WANAHUSIKA,,, lakin pia na jamaa wametukalia pabaya
OK tuseme hii ni kweli usemavyo, swali ni je baada ya miaka mingapi sasa ndiyo tutaachana na hizi lawama? Mbona tuliopata nao uhuru huko Asia na America kusini wametoboa?
 
Dhana nzima ya waafrika kudumaa katika kuleta maendeleo kunaenda sambamba na kuendelea kuwa tegemezi kwa mataifa ya magharibi na Marekani.

Misaada au ufadhili tunaopata Africa ni sumu na ndio sababu kubwa inavyofanya tuendelee kudumaa. Wenyewe kwa wenyewe tungeweza kusaidiana na kuinuana kwa kutumia rasilimali tulizojaliwa.

Tunazo rasilimali za kutosha ila tunahitaji sisi wenyewe tuwe na rasilimali watu wenye upendo, utu, utii, umoja, ubunifu, uaminifu, uadilifu, uvumilivu na utimamu wa kusimamia dira na malengo yetu ili tuweze kutumia rasilima zilizopo kwa maendeleo endelevu. Tunazo resources ila bara linahitaji watu ambao ni resourceful.
 
Dhana nzima ya waafrika kudumaa katika kuleta maendeleo kunaenda sambamba na kuendelea kuwa tegemezi kwa mataifa ya magharibi na Marekani.

Misaada au ufadhili tunaopata Africa ni sumu na ndio sababu kubwa inavyofanya tuendelee kudumaa.
Hii hoja ya nchi za Magharibi ni kichaka cha wanasiasa Wa Afrika wanachojifichia kukwepa wajibu wa wao kuidumaza Afrika kimaendeleo.

Uchina, Urusi, Brazil, India, Afrika ya kusini zote zimewahi au Bado zinapokea mikopo toka nchi za Magharibi lakini zinapiga hatua za kimaendeleo.

Tatizo siyo misaada toka nchi za Magharibi bali ufujaji wa misaada hiyo kunakofanywa na wanasiasa Wa Afrika.

Asilimia tisini ya wanasiasa wa Afrika ni majizi mabobevu.

Umewahi kujiuliza ni kwa nini Afrika huwezi kuwa tajiri bila ya kushirikiana na wanasiasa waliopo madarakani? Bila ya KUIBA na KUFISADI mali ya umma huwezi kuwa tajiri Afrika.
 
Swala la maendleo pia lina uhusiano mkubwa na tamaduni za sehemu usika
 
Swali lako linaweza pia kifanana na swali hili. Kwanini watu wengi wanaamini umasikini wa waafrika unasabisbwa na viongozi wake.
Lazima tutambue kunakikundi Fulani kushikilia nyanja za kiuchumi kama ilivyo viongozi wa kiafrika anaweza kuamua kukukandamiza kiuchumi like kuweka Kodi zisizolipika, mfumuko wa bei, mzunguko mdogo wa fedha nk
Kukupangi bei ya mazao. Wakuuzie mbolea ghali then mazao uuze wanavyotaka, Sasa hapo utamlaumu mwananchi au kiongozi.
All in all naweza kusema pia mabeberu yamechangia kiasi kikubwa nchi za Kiafrika kuwa masikini
 
Victim hood mindset kutafuta sehemu ya kutupia lawama.

Waafrika adui yetu ni uvivu, ulalamikaji, ulafi na umimi hasa ukabila

Hata wachina na wahindi waliwahi kutawaliwa na wazungu, Leo wahindi ndio kundi linaloongoza kwa kuwa na jamii yenye familia zenye kipato cha juu zaidi Marekani, Wachina wameipigisha nchi yao hatua kwa spidi ya radi
Wahindi wachina walitawaliwa kulimwili tu sisi tumetawaliwa kimwili , kifikra na kiimani.
 
Kwa kuwa walipuuza mila zetu na kutulazimisha kuamini zao. Mfano mzuri ni hizi dini. Hakika wamedumaza akili zetu, mtu unajifungia siku nzima ukiomba. Kumbuka kuwa Yesu ni mzungu.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Mpaka Leo Bado Kwa sehemu kubwa wanasiasa wetu wanaonesha kwa maneno na matendo yao kuwa wazungu ndiyo ama wanasababisha tusiendelee au wao ndiyo walisababisha tusiendelee.

Kwa nini tunaamini hivyo??
Ni kwa sababu hatuna viongozi wenye uwezo wa kuongoza!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mpaka Leo Bado Kwa sehemu kubwa wanasiasa wetu wanaonesha kwa maneno na matendo yao kuwa wazungu ndiyo ama wanasababisha tusiendelee au wao ndiyo walisababisha tusiendelee.

Kwa nini tunaamini hivyo??
Niger coup ni jibu.
 
Back
Top Bottom