Kwanini iitwe Tanganyika law society na sio Tanzania law society?

Kwanini iitwe Tanganyika law society na sio Tanzania law society?

Wakuu kwa Sasa masikio yote yapo Dodoma kwenye mkutano wa mawakili na katika mkutano huo umefanyika uchaguzi ambao matokeo yake yanasubiriwa kwa hamu sana.
Maswali yangu kwa wajuzi:

1.Kwanini hii inaitwa Tanganyika law society na sio Tanzania law society??
2. Je Zanzibar napo huwa kuna Zanzibar law society??
3. Kuna wakati ndugu Fatma Karume kutoka Tanzania visiwani alokuwa mwenyekiti wa Tanganyika law society, je bila shaka hii ni kumaanisha hata mawakili kutoka Zanzibar ni wanachama na ndo MAANA bi Fatma alipata nafasi ya uongozi?

4. If that is the case, kwanini sasa haibadilishwi jina ikaitwa Tanzania law society Ili kumaanisha ni jumuiya ya mawakili pande zote mbili bara na visiwani?

Ngaiwoye
Kumbuka hiki chama mpaka sasa 2024 kina umri wa miaka 70, Muungano haujafika umri huo. Kwahiyo kilianzishwa kipindi cha TANGANYIKA!
 
Kumbuka hiki chama mpaka sasa 2024 kina umri wa miaka 70, Muungano haujafika umri huo. Kwahiyo kilianzishwa kipindi cha TANGANYIKA!
Hata Tanganyika nchi ilimpata uhuru kabla ya muungano, baada ya muungano ilibadilika na kuwa Tanzania.
Msingi wa SWALI langu ni huu...Fatuma Karume anatokea Zanzibar ni mwanachama na ALIWAHI kuwa mwenyekiti wa TLS...na hapo juu nimeambiwa Zanzibar pia ipo society kama hii...Sasa hainingii akilini why iitwe Tanganyika na sio Tanzania...
Je katika Zanzibar law society mtu kutoka Bara anaweza kuwa president??
Je Ili uwe kiongozi wa TLS ni LAZMA uwe na ubishani na serikali na ndo mana bi Fatma alishinda?
 
Back
Top Bottom