Kwanini ijengwe Sanamu ya Hayati Rais Magufuli peke yake na si Marais wengine?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Nimeshtushwa Sana na Tangazo la kuwa kuna ujenzi wa sanamu ya Magufuli Uwanja Wa Maonesho ya Sabasaba kwa Gharama ya Tsh. milioni 420.

Sikatai ila nina hoja:
Kwanini Magufuli?
Mwinyi je?
Mkapa je?
Kikwete je?

Hao Wote Walikuwa ni MARAIS wa NCHI na Kuna MAMBO MAKUBWA hata NAO WALIIFANYIA NCHI hii.

Kama Tunataka Kujenga SANAMU ya MAGUFULI Basi TUJENGE na SANAMU za MWINYI, MKAPA na KIKWETE.

Pia soma
- Sanamu la Magufuli na ukarabati wa kumbi za kisasa kujengwa kwa Tsh milioni 420 viwanja vya Sabasaba
 
Hii nchi ina mambo ya ajabu sana... Pata picha kila rais mstaafu au mwendazake akijengewa sanamu? Hivi Nyerere hastahili sanamu?
Nyerere si alishajengwa na Magu
 
Ulishawahi kujiuliza kwa nini huwa kuna maazimisho ya waziri mkuu Moringe Sokoine tu?

Ili ukumbukwe lazima uwe na outstanding performance
Maadhimisho ya kumbukizi ya Hayati Moringe huwa yanafanywa na SUA tu sio Kitaifa...lakini pia huwa kuna Nyerere day na Karume day pia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…