Kwanini IMF na Benki ya Dunia wameitenga Tanzania katika mgao wa fedha za Corona? Au ule utani kwamba sisi matajiri, wao wametuibia, uliwachukiza?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nashangaa,nchi zote zinazopakana na sisi zimepewa msaada wa haraka na benki ya dunia,IMF,na kuweka kidonda chumvi. Trump kaongea na marais wa nchi tunazopakana nazo na kuahidi misaada kedekede.

Je ule utani wa kuwaita mabeberu wao walijua tunawachukia?sisi watanzania ni watu wa utani kimakabila na ndio asili yetu,japo sijui kwamba kabila gani linautani nao au kama nchi ndio tuna utani nao.

Naomba waziri wa utamaduni awaambie,tunapotaja majina kama mabeberu,tumeibiwa sana,ni chachandu ya siasa za ndani tu jamani,

Watupe na sisi kamsaada
 
Umeshamaliza Kujifukiza ili usiambukizwe Janga hili baya la CORONA kama ulivyoelekezwa na Kiongozi wako Mkuu Ndugu?
 
Tumetoka kupewa zile zilizokuwazimekwama .......

So kupewa tena utakuwa upendeleo pia

Japo wametoa nafasi ya kuomba mikopo ya dharula .. mkuu kakataa anataka watusimashie repayment ili anachokusanya kitumike katika kupambana na hii covid- 19
 
Hakuna utani kwenye pesa.
IMF sio chombo cha waswahili kwamba wana operate kwenye mananeno... na blah blah. Hawa jamaa wako serious. No games likija suala la pesa
 
Nashangaa,nchi zote zinazopakana na sisi zimepewa msaada wa haraka na benki ya dunia,IMF,na kuweka kidonda chumvi. Trump kaongea na marais wa nchi tunazopakana nazo na kuahidi misaada kedekede.

Je ule utani wa kuwaita mabeberu wao walijua tunawachukia?sisi watanzania ni watu wa utani kimakabila na ndio asili yetu,japo sijui kwamba kabila gani linautani nao au kama nchi ndio tuna utani nao.

Naomba waziri wa utamaduni awaambie,tunapotaja majina kama mabeberu,tumeibiwa sana,ni chachandu ya siasa za ndani tu jamani,

Watupe na sisi kamsaada
Sisi dona, siyo sembe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unadhani hiyo misaada inatoka bure bure tu, lazima ilipwe, japo inaitwa misaada lakini sio misaada ni mapatano yakibiashara na faida lazima iwepo kwa mtoa mtonyo
 
M
Taarifa za kweli za idadi ya wagonjwa na vifo ndiyo zitasaidia tupewe msaada.

Ukipika report hupewi msaada.

Msaada huo ni bure au tutalipa? Kama ni bure sawa lakini kama si bure hauna maana,
Kama wana huruma na sisi watukopeshe pesa za mitaji kwa wafanya biashara wetu waongeze mitaji nchi ipate uchumi, lakini suo misaada ya magonjwa kisha kuna riba.
Tukiwa na pesa tutajitibu wenyewe.
 
Mitaji ya biashara za barakoa au?
 
Back
Top Bottom