Kwanini IMF na Benki ya Dunia wameitenga Tanzania katika mgao wa fedha za Corona? Au ule utani kwamba sisi matajiri, wao wametuibia, uliwachukiza?

Wameituibia sana. Ukiuliza wakati unaibiwa wewe ulikuwa wapi?? Wakati alikuwemo
 
Naomba waziri wa utamaduni awaambie,tunapotaja majina kama mabeberu,tumeibiwa sana,ni chachandu ya siasa za ndani tu jamani,
Mmezidisha siasa wanaogopa mkipewa pesa mtaenda kununua Midege kwa keshi mmje muwakoge wenzenu
 
Msaada!? Kutoka Word Bank na IMF?!!! Sio charity organisations zile. Ndio mambo Magufuli aliyoyakataa. Wanakupa mkopo wa harakaharaka halafu unafurahia eti umesaidiwa. Kama ni msaada wasamehe walizokupa maana kwao ndio ingekua rahisi zaidi
Mbona ule wa world bank alimtuma Hadi kabudi Kama alikua auhitaji
 
Hivi ARvs sio msaada ni mkopo
 
Mbona ule wa world bank alimtuma Hadi kabudi Kama alikua auhitaji
Nikweli ule mkopo alikua anauhitaji sana ili kusukuma agenda fulani ya maendeleo na WB wakawa wanaleta vikwazo vingi.

Na ndio hapo msingi wa shaka kuhusu mkopo huu wanaoitiwa unapojengeka. Kwamba kwa wema gani hao WB na IMF waliokua nao kwetu hadi watuite twende kukopa tena wenyewe wakiita msaada hyku kwa wakibembeleza?
 
Hata wewe unapompa mwanamke hela hawez kukupangia, Bali we ndo unaompangia

Jiulize kwanin serekali ilisema tayari Ina njia mbadala kwa wanafunz waliopata mimba ndo ikapewa mkopo

Kama ilikua aihuitaji isingehangaika kutafuta njia mbadala

Kwa hiyo world bank na IMF ndo inayoipigia magoti Tanzania ama kweli Ujinga haujawah kutuacha salama waafrika
 
You
You are missing the point. Mkopo wa elimu serikali ilikua inauhitaji ndio maana wame comply na hayo masharti ya mabeberu ya kua na njia mbadala kwa hao mabinti wenye viherehere mpaka wakawa wazazi wakiwa bado wanafunzi .Kwenye mkopo wa corona Magufuli amekataa pamoja na kwamba hao mabeberu walikua tayari kutoa

Logic yake ni kwamba kwanini kama hivyo vyombo vya mabeberu wanazipenda saana nchi zetu wasifute au kusimamisha ulipaji wa mikopo iliyokwishatolewa ili hela za marejesho nchi zitumie kujijengea uwezo wa kupambana na corona kwa kutumia mapato yao ya ndani. Kwanini WB na IMF wanadanganya ili kuzidi kuziingiza nchi masikini kwenye shimo la madeni zaidi? Hiyo ndio hoja ya Rais na mimi naiona ina mantiki
 
Narudia Tena huwez ipangia bank masharti nawakati wao ndo wanaokupa mkopo, lazima ufuate masharti yao mbona ni simple logic
 
Wala hawajatutenga.
Wale wanataka kuwa unapoomba pesa usema kuwa utaitumia kama wanvyotaka. Wanataka itumike kupunguza makali ya ugonjwa na pi itumike kwa wananchi ambao wapo affected zaidi. Wananchi wa hali ya chini.
Ila kiuhalisia Jiwe anataka kuila hii pesa na wao wameshtuka.
Watampa hio pesa ila haitakusaidia chochote kwa sababu jiwe roho mbaya ataila
 
Mbona waziri wa fedha aliandika barua kuomba fedha ila akanyimwa. Alionyesha tu matumizi ya kupambana na korona, wao wanataka kuoungza makali ya masikini pia.
Jiwe kakataa..
 
Narudia Tena huwez ipangia bank masharti nawakati wao ndo wanaokupa mkopo, lazima ufuate masharti yao mbona ni simple logic
And this is how they have always been strangling nations over the years. Wanakupa mkopo utumie katika sekta ambazo hazizalishi then utumie mapato yako kutoka kwenye vyanzo vingine kulipa deni. Unabaki mtumwa wa madeni miaka yote

Kwenye hili wameshtukiwa. Walitaka kutumia corona kama chambo ili tuiume ndoano yao tuzidi kuzama kwenye madeni. Kwa taarifa yako katika mambo yaliyopelekea kuivamia Libya ni nia ya Marehemu Ghadafi kutaka kuiondoa Afrika kwenye utumwa huo wa madeni ya kinyonyaji. Kwenye hili la kukataa huo mkopo (eti wengine wanaita msaasa!!!) Magufuli alikua sahihi kabisa
 
Mwenye hekima, na hasa akiwa kiongozi, kabla hajatamka neno, hujiuliza:
1) kuna ulazima wa kusema?
2) Niseme nini?
3) Nikisema kuna hasara gani au faida gani?
4) Nikiacha kusema, kuna hasara yoyote?

Aliyekosa hekima, hutangulia kusema kabla ya kujiuliza maswali hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M
Taarifa za kweli za idadi ya wagonjwa na vifo ndiyo zitasaidia tupewe msaada.

Ukipika report hupewi msaada.

Msaada huo ni bure au tutalipa? Kama ni bure sawa lakini kama si bure hauna maana,
Kama wana huruma na sisi watukopeshe pesa za mitaji kwa wafanya biashara wetu waongeze mitaji nchi ipate uchumi, lakini suo misaada ya magonjwa kisha kuna riba.
Tukiwa na pesa tutajitibu wenyewe.
 
Mikopo ya biashara ipo nenda CRDB utapewa mkopo wa biashara kama unataka.

Hapa tunazungumzia misaada ya kupambana na Korona.
 
Hizo ni hadithi.

Bank ya Dunia imewahi kukopesha mataifa mbalimbali kwaajili ya miradi ya maendeleo.

"The World Bank provides low-interest loans, zero to low-interest credits, and grants to developing countries. These support a wide array of investments in such areas as education, health, public administration, infrastructure, financial and private sector development, agriculture, and environmental and natural resource management. Some of our projects are cofinanced with governments, other multilateral institutions, commercial banks, export credit agencies, and private sector investors."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatutaki watuongezee mzigo wa mabenki.Wakiweza wafute au watupunguzie madeni ili hela tulizokuwa tunalipa madeni tutumie kupambana na Corona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…