Washawasha
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 16,717
- 13,176
Wabongo msumari,viongozi nyundo.Jamaa ninawakubali kuhusu uwezo wao wa akili. Kufinance viwanda na ubunifu. Pia nchi yao ni jangwa kabisa. Hawana mto, kisima, bwawa wala ziwa,inawabidi wachukue maji ya chumvi toka baharini kisha watoe chumvi kwenye desalination plants halafu watu wakitumia wanakusanya maji taka wanayarecycle kwa ajili ya kilimo. Ila wana maji ya kutosha kutumia mpaka kwenye umwagiliaji. Nchi yao ni jangwa kabisa hakuna mvua wala umande na wanalima na wanavuna sana. Na bado wanaendelea na utafiti wa kuboresha technology yao. Kiufupi wanasema technology waliyogundua ni ndogo mno na wanataka kuboresha zaidi
Ingekuwa bongo hela ya kujenga desalination plants watu wangezilamba zote na hakuna kitu kingefanyika. Au desalination plants zinafanya kazi kwa miezi 3 halafu wanazima kwa ajili ya matengenezo miezi 9 na maposho makubwa ya vikao wangekula . Hapo bado hatujazungumzia upigaji wa hela ya service ya mitambo na bado hawajaiba hela ya umwagiliaji kwenye kibbutz.
Nalog off Z