Kwanini inatokea ligi kuu tu na haitokei ligi ya mabingwa Afrika

Kwanini inatokea ligi kuu tu na haitokei ligi ya mabingwa Afrika

Wapenzi wa michezo naomba mnijuze, kuna hii klabu inaitwa Yanga katika mechi zake 8 za mwisho za ligi kuu bara 2016, nne kati ya hizo wachezaji wa timu pinzani wanapewa kadi nyekundu na hatimaye Yanga inatumia fursa hiyo kupata ushindi, lakini kinachonishangaza katika ligi ya mabingwa Afrika, Yanga imeshacheza mechi 5 (2 na timu dhaifu ya Mauritius Cercle de Joachim, 2 na APR ya Rwanda na 1 Al Ahly ya Misri) hakuna kadi nyekundu timu ya upinzani imepewa na sasa dhahiri baada ya wiki moja inatolewa katika mashindano hayo na timu ya Al Ahly. Kwa nini ligi ya bara tu na sio ligi ya mabingwa Afrika?
Timu ya Malinzi mwenyekiti anaitwa YUSUF MANJI...unategemea nini.?
 
Mtoa mada umeuliza swali gumu kuliko upeo wa wachangaiaji wengi humu ambao unazi na ushabiki maandazi unapunguza uwezo wao wa kuona mambo kwa macho yote. Majibu na posts unazopata ni matokeo ya makengeza ya kiushabiki. Mimi nami nitajaribu kujibu kwa kadiri ya uelewa wangu.

Zipo sababu nyingi kwa nini Yanga ni mnufaika mkubwa wa penati na kadi nyekundu nyingi kwa wapinzani wao;

1. Yanga ina foward kali pengine kuliko zote kwa Ligi Kuu sasa. Nguvu na usumbufu wa Ngoma, ujanja wa Tambwe na kasi na usumbufu wa Msuva ni wazi timu pinzani zinatumia nguvu kubwa kuwatuliza washambuliaji hawa, au kwa lugha rahisi wanapaniwa sana, na Ngoma anajua sana 'kuomba kuchezewa faulo kwa kujiingiza kwenye njia mara kwa mara na kugongana na walinzi wa timu pinzani. Na hapa lazima tukubaliane, wabongo wanapania sana mechi!!

2. Aina ya mpira wa Yanga ni wa matokeo zaidi, yaani direct football.. Ktk mechi kubwa wanacheza mpira wa kushambulia kwa kushtukiza kwa kuingia ktk eneo la penati kwa haraka hata kwa pasi moja tu, ambapo lolote laweza kutokea. Timu nyingine, na hasa Simba zinacheza mpira mwingi kabla ya kuingia eneo la hatari na hivyo kutumia muda mrefu kidogo kufikia eneo la timu pinzani hadi defence zinakuwa zimejipanga kuokoa kabla ya faulo.

3. Katika miaka ya hivi karibuni Yanga waliwahi kupiga refa live bila chenga. Shughuli hii ya kusulubu refa ilifanywa na wachezaji wenyewe chini ya Nadir Haroub na kuungwa mkono na mashabiki wao. Kabla ya hapo Yanga walikuwa walalamishi sana kuhusu marefa na baada ya kumpiga Israel Mujuni Nkongo, na kupewa adhabu kubwa, coincidentally, kiukweli marefa wengi wanakuwa ktk pressure kubwa kuchezesha Yanga. Na kwa sasa Yanga ni timu pekee isiyolalamikia sana marefa hapa Tanzania lkn pia ikiwa ndiyo inayoongoza kulalamikiwa na timu pinzani. Ni ngumu kuona kuwa kile kipigo kimesababisha Yanga kuogopwa, lkn ni ukweli pia kusema, baada ya kipigo, ghafla Yanga hailalamikii, isipokuwa inalalamikiwa zaidi!!!!

Mchanganyiko wa sababu hizi, unaifanya Yanga iwe na kila sababu ya kupata hizo penati na kadi nyekundu kwa wapinzani wake, na kuna kila dalili hali hii itaendelea zaidi.
 
Hili kombe wawape Yanga tu,halafu ndo wamalizie viporo!Wanabebwa sana hawa jamaa ndo maana ligi ya mabingwa Africa hawawezi enda popote.Bila hizi red card mbona Yanga ya kawaida tu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kama siyo kadi nyekundu lazima watatafutiwa penati,na hii ndo maana mpira hauendelei,haiwezekani kadi nyekundu kwa wapinzani tena zinatolewa kwenye dk kuanzia 70
Mechi ya baselona na athletic madird tores alipewa kadi nyekundu na baka alishinda ndo tuseme baka alibebwa au?……jana usiku dk za majeruhi athletic madrid wanapata penati nao tuseme walibebwa au? Kafanye tathimini upya
 
Wadau leo Yanga wamecheza na Coastal Union katika michuano ya Azam Confederation Cup, kama kawaida red card zimeendelea kutolewa kwa timu pinzani inayocheza na Yanga, na hapa chini ni baadhi ya post katika thread nyingine inayoendelea;


KikulachoChako said:
Hakuna sababu ya vodacom kudhamini ligi kama hii ambayo bingwa anapangwa na chama cha soka......

Nashauri TFF msimu ujao wamkabidhi tu Yanga ubingwa wake maana kuendelea na ligi ambayo bingwa ameshapangwa na TFF ni kuwapotezea watu muda wao na nguvu zao.....

danya said:
Mbna mwamuzi wa pembeni anatofautiana na mwamuzi wa kati?

Julio alisema wanaoshinda hawastahili kushindaa ndo maana nje ya nchi hawafanyi vizuri

Mbojo JF-Expert Member
#104
33 minutes ago

Joined:May 31, 2011
Messages:461
Likes Received:81
Trophy Points:28
Hata maamzi ya TFF yataipa yanga ushindi.Nimeona yafuatayo 1.Ngoma kafunga kwa offside
2.Yule babu alipaswa apewe red lakini kapewa yellow.
3.Tambwe kafunga na kiwiko.
Kwa hali hii washabiki wanyamaze tuu watani.

danya JF-Expert Member
#107
33 minutes ago

Joined:Sep 6, 2014
Messages:1,736
Likes Received:341
Trophy Points:83
libeva said:
Mashabiki wa mikia wameleta fujo
Hivi ile faulo ya makusudi ya mchezaji wa yangaa na hajapewa hata njano anapewa nyekundu mtu mwinginee! Yaani kifupi mwamuziiii wa Leo kachemka game imemshindaaaa mbayaaaa kama kweli hakupokea pesa

Mbona yanga waliifunga costal goli 8 na walikubali coz mpira ulikuwa Fare kwanini leo

Kifupi MWAMUZI WA LEO KAZINGUA GOLI LA NGOMA ILE NI OFFSIDE YA WAZI KABISAAAAAA

MWAMUZI ALITUMWA HUYU

danya JF-Expert Member
#111
28 minutes ago

Joined:Sep 6, 2014
Messages:1,736
Likes Received:341
Trophy Points:83
DR.CYPRIAN said:
Ongeeni yote...referee wa leo hakua makini
Bora hilo Refa leo Ameshikishwa Pesaaa huyooooo

Lakini kwa TFF YA MALINZI SINA WASI WASI NA MAAMUZI HAPO COSTAL WATAAMBIWA NDO WENYE VURUGU HIVYO YANGA IMEPITA!

NITAMKUMBUKA SANA TENGA


chilonge JF-Expert Member
#114
26 minutes ago

Joined😀ec 23, 2014
Messages:221
Likes Received:28
Trophy Points:28
Nahisi leo ningekuwa uwanjani ningepata kesi ya jinai..!
Dhahiri bin Shahri leo kuna namna imefanyika asee! Yanga wamebebwa sana kupita maelezo dah..!
Kwa hali hii soka letu haliwezi kusonga na kamwe tutaendelea kutolewa kwenye michuano ya Kimataifa



Katavi Platinum Member
#119
24 minutes ago

Joined:Aug 31, 2009
Messages:34,558
Likes Received:1,090
Trophy Points:113
MANI said:
Wanatia aibu ndio maana hawawezi kucheza nje ya nchi
Yanga full kubebwa.!

simanyane JF-Expert Member
#123
22 minutes ago

Joined:Apr 10, 2015
Messages:1,812
Likes Received:139
Trophy Points:63
Mnataka haki hameni nchi mbona Jecha alitangaza matokeo na mpaka sasa hali imetulia hakuna cha vulugu hii ndo Tz bwana

Kafman JF-Expert Member
#125
20 minutes ago

Joined:Feb 3, 2012
Messages:782
Likes Received:32
Trophy Points:28
Mi huwa nawaambia kila siku kushabikia mpira wa Tz ni upuuzi wa kiwango cha juu,huyo Malinzi alishawahi hata kuongoza mpira shuleni? mtu kaja tu from no where anapewa uongozi wa mpira. Tutamkumbuka sana Wambura alihujumiwa vya kutosha!!
 
Ndo tatizo la kufuatilia mpira kupitia radio hlo, kadi zote nyekundu haikuepo mtu alo onewa, na ubora wa tim ya yanga una fahamika lazma ayo mambo yawepo, barca hazipit mech tatu wapinzani hawajala red kwa pia hata uko hispania washabik wengne hulala mika
 
Haya tena, ripoti ya Salehe Jembe kuhusu mechi ya Yanga na Coast ni kama ifuatayo;

UTATA WAIGUBIKA MECHI YA COASTAL VS YANGA, WACHEZAJI YANGA WAPIGWA CHUPA






Hauijulikani kama Yanga imesonga fainali ya Kombe la FA au itakuwa tofauti.


Mechi yake dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga imeisha ikiwa Yanga inaongoza kwa mabao 2-1. Lakini mwamuzi alimaliza baada ya kuzuka kwa tafrani na kipa wa Yanga Deogratius Munish ‘Dida’ kushambuliwa na mashabiki.


Pia beki Oscar Joshua akapigwa chupa kichwani. Mashabiki hao walionekana walikuwa wakipinga Yanga kupewa bao.


Amissi Tambwe aliyeingia kuchukua nafasi ya Donald Ngoma alifunga bao la pili kwa mkono.


Kabla ya hapo, Ngoma alifunga bao ambalo wachezaji wa Coastal Union walilalamika ni off Side.


Sasa haikujulikana mechi ilikuwa imeisha, au mwamuzi amemaliza kabla na suala hilo litakuwaje.


Lakini taratibu na kanuni zinaonyesha Yanga inaweza kupewa ushindi ikibainika mashabiki waliofanya vurugu ni wa Coastal Union lakini pia mchezo unaweza kuchezwa kwa dakika zilizobaki kama mashabiki waliofanya vurugu hawatakuwa wa Yanga au Coastal.
 
Wanampango muache nanyie kushabikia ligi za tz
Mimi siku nyingi sina muda huo
 
Leo Salehe Amemaliza kabisa, angalia hii hapa chini;

NAONA AIBU KUKUMBUKA, NAOGOPA HATA KUOTA MAMBO YA TANGA-COASTAL VS YANGA



Na Saleh Ally
HAKUNA kitu Watanzania wengi hawakipendi kama ukweli. Ukikisimamia, basi wewe ndiye adui namna moja wa wengi, lakini mimi naendelea tu na leo nipo Tanga.
Kwanza nianze kulaani kitendo cha mashabiki waliokua kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakati Coastal Union ikipambana na Yanga katika nusu fainali ya Kombe la FA kumpiga mwamuzi msaidizi hadi akazimia.
Hakika ameumizwa na mara nyingi nimekuwa nikilalama kuhusiana na vurugu za uwanja huo, hadi imefikia sipendi hata kuangalia mpira hapo.
Ingawa safari hii, unaweza ukasema ni kama nyuki waliochokozwa, si kama siku nyingine. Mwamuzi msaidizi aliyekuwa ameshika kibendera upande wa mashariki ya uwanja. Alifanya mambo mawili makubwa na mabaya katika mpira wa nchi hii.
Hakuna anayeweza kukataa hata kidogo kama Coastal Union waliutawala hasa mchezo huo. Walikuwa bora mara mbili ya Yanga, wachezaji vijana na wazalendo walikuwa bora mara tatu zaidi ya wakongwe na wageni wanaolipwa mamilioni ya fedha ukilinganisha na wao.
Coastal Union wenyewe wanapaswa kujilaumu kushindwa “kuua” mchezo mapema kabisa. Walikuwa na uwezo wa kwenda mapumziko na bao tatu na Yanga, walikubali kabisa. Lakini hawakuwa makini na mambo yakawa magumu kabisa.

Bao la Coastal Union lililofungwa na Yossouf Sabo raia wa Cameroon lilikuwa bora na bomba kweli. Lakini mabao yote mawili ya Yanga yalijaa utata na lile la pili linaonyesha ni uonevu wa dhati, dhahiri shahiri kwamba mwamuzi huyo alipanga kuona Yanga inashinda. Huu ni upuuzi wa hali ya juu ambao tunataka tukae kimya na kuuachia upite kwa kuwa kila mmoja anahofia kulaumiwa na mashabiki wa Yanga kama atasema ukweli.
Yanga ilikuwa na mabao 2-1 hadi mwamuzi anavunja mchezo baada ya vurugu. Lakini uhalisia unaonyesha “hapana”. Bao la kwanza alilofunga Donald Ngoma, lina utata mkubwa wa kuotea, Ngoma anafunga lakini hata yeye anaonyesha hajiamini kama anapaswa kushangilia au la.
Bao la pili la Tambwe, dhahiri anausukuma mpira kwa mkono kila mmoja akiona wazi. Lakini mwamuzi anaamua kusema bao. Hakika hii ni aibu na Wanayanga wanaochukia watu kusema ukweli watakuwa ni wanaojidanganya kwa kuwa bingwa wa michuano hiyo atashiriki michuano ya kimataifa ambako hakuwezi kuwa na waamuzi wazembe kama hao wa mechi kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

Mwisho wa hili. Adhabu inaweza kuangukia kwa Coastal Union na Yanga ikasonga ikionekana haina hatia. Lakini macho yetu yanapeleka ujumbe ndani ya mioyo yetu kwamba Coastal Union wameonewa au wamedhulumiwa.
Dhuluma hiyo unaweza kuikataa kinafiki, lakini kama ni muungwana. Kamwe hauwezi kuwaza hilo, badala yake utakasirishwa kabisa hata kama utakuwa Yanga wa kulialia.
Lazima kuwe na “fea” game. Kama Coastal waliitoa Simba, mwamuzi akatoa penalti dakika ya mwisho kwa kuwa yalikuwa ni maamuzi sahihi, hicho ndicho kinachotakiwa kwa kuwa tunahitaji bingwa halali.
Angalia mechi ya Mwadui FC dhidi ya Azam FC ilivyokuwa tamu. Angalia ushindani wa juu na mshindi mwisho kapatikana kwa mikwaju ya penalti.

Mechi ya Tanga; gumzo lake sasa ni uamuzi mbovu. Hakika hili ni jambo baya katika soka nchini kwetu na haitakuwa ni kuisaidia Yanga, pia uzembe wa mwamuzi huyo hauwezi kuwa na faida katika mchezo wa soka na TFF wanapaswa kuchukua hatua kali pamoja na maumivu ya kipigo alichopata, lakini apumzishwe kabisa.
Sitaki hata kukumbuka kilichotokea, naona aibu. Jana usiku, nimejitahidi nikilala nisiote ndoto ya mechi hiyo, naogopa!
 
Mtoa mada haya nenda kwa Kaburu akupe ujira wako,na kama imekuuma sana saga chupa unywe. Yanga mbele Daima nyuma mwiko.
 
Mbereko hizi ndio zinazotugharimu Kama Taifa tuwe na mafanikio ya Juu kabisa kila mara kutolewa 'kiume' katika raundi za AWALI kimataifa!very sad!
 
Mwenye video za goal za yanga zidi ya coast atupie hapa tumalize ubishi
 
Mbereko hizi ndio zinazotugharimu Kama Taifa tuwe na mafanikio ya Juu kabisa kila mara kutolewa 'kiume' katika raundi za AWALI kimataifa!very sad!
Hahahaaa mtu anatolewa raundi ya awali,halaf anajitapa ametolewa"kiume"!Very fun!
 
kinacho waponza simba ni kutumia mda mwingi kufatilia ya yanga na kusahau yao, wametumia mda mwingi kuhakikisha yanga inatolewa na Alialy na kusahau game yao ya coastal Union
 
Kuna viumbe mwaka wakustaafu umefika(Zaidi ya miaka 7)hawajafika hiyo nafasi.
 
Wapenzi wa michezo naomba mnijuze, kuna hii klabu inaitwa Yanga katika mechi zake 8 za mwisho za ligi kuu bara 2016, nne kati ya hizo wachezaji wa timu pinzani wanapewa kadi nyekundu na hatimaye Yanga inatumia fursa hiyo kupata ushindi, lakini kinachonishangaza katika ligi ya mabingwa Afrika, Yanga imeshacheza mechi 5 (2 na timu dhaifu ya Mauritius Cercle de Joachim, 2 na APR ya Rwanda na 1 Al Ahly ya Misri) hakuna kadi nyekundu timu ya upinzani imepewa na sasa dhahiri baada ya wiki moja inatolewa katika mashindano hayo na timu ya Al Ahly. Kwa nini ligi ya bara tu na sio ligi ya mabingwa Afrika?
Wale ni wa kimataifa wenzao kwahiyo full maufundi...
 
Back
Top Bottom