Ni tatizo akiandika barnaba tu au hata wakiandika wengine?
Injiri ya Barnaba ni tofauti kabisa na Injiri za kwanye biblia kwakuwa Injiri zote za kwenye biblia zinakubaliana kwa pamoja kuwa.
Yesu wa Nazaleti ndiye-
[emoji116]
-Pekee Kristo na Masihi.
-Bwana na Mwokozi wa watu wote wa ulimwenguni.
-Njia, Kweli na Uzima.
-Alitoka Mbinguni, akauvaa mwili wa binadamu, akaja duniani kupitia bikira maria, akahubiri, akateswa, akafa, akafufuka siku ya tatu, akapaa mbinguni, atakuja kuwahukumu wazima na wafu siku ya kiama.
-Ana mamlaka ya duniani na mbinguni.
Hajafa hadi leo na yupo anatawala mbinguni na duniani.
-Ni mwana wa Mungu.
-Anauweza wote, ni muumbaji wa vitu vyote.
-Ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho.
-Amri alizotuagiza kuzifanya ndio za mwisho hakuna amri na maagizo mengine mapya.
-Alikuwepo kabla ya ulimwengu kuwapo.
-Injiri yoyote itakayoonekana ikipingana na Injiri yake basi ni feki na aliyeileta amelaaniwa.
-Atakuja kutufufua siku ya Mwisho na kutupeleka kwake mbinguni sisi tunaomwamini na kufuata maagizo yake kama agizo la UBATIZO.
-Mashetani, ma Ibilisi, ma Jini, Mapepo, na wafuasi wao ni jamii ya giza na yamelaaniwa yanasubiri kutupwa jehanam siku ya kiyama, hakuna JINI JEMA.
-Yesu Kristo Ndiye Masihi, Mungu Mkuu na Mwokozi wa watu wote.
[emoji115]
Hayo maelezo hapo juu ni baadhi ya maneno ambayo Injiri zote za kwenye biblia zinayasisitiza kwa uzito kubwa.
Tofauti ipo kwa,
Injiri ya kwenye kitabu cha Muhammadi (Qurani) na ya kitabu cha Barnaba, hayo mambo hayapo kabisa.
Injiri ya Qurani na Barnaba kwa pamoja zinasema
[emoji116]
-Muhammadi ndiye Nabii wa kumfuata kwa sasa.
-Yesu ni mtume tu kama Muhammadi.
-Yesu Kristo hakuwahi kuteswa, kusulubiwa wala kufa msalabani wala kufufuka.
-Yesu sio Mungu wala Mwana wa Mungu.
-Mungu hawezi kuwa na mwana kwakuwa hana mke.
-Uislamu ni Dini, na asiye mwislamu hawezi kufika mbinguni kwakuwa ni kafiri.
-Maagizo aliyo agiza mtume Muhammadi ndiyo ya msingi kufuatwa na watu wote.
-Mtume Muhamadi ndiye mtume wa mwisho, hakutatokea mtume mwingine mwenye kitabu na maagizo mengine.
[emoji115]
Hayo ni baadhi ya maagizo yanayosisitizwa sana, kwenye kitabu cha Qurani na kitabu cha Injiri ya Barnaba.
.....................................................
Hivyo msibishane hadi kutoana ngeu wewe Masudi Mshahala na wenzako.
Mjue kuwa,
Wakristo tuna Injiri yetu iliyopo kwenye Biblia.
Na ninyi Waislamu muna Injiri yenu iliyopo kwenye kitabu cha Qurani na kwenye kitabu cha Barnaba.
Tusilazimishane wala kuvutana kila mtu aifuate Injiri yake anayoiamini na mtume wake.
Tuonane siku ya KIYAMA.
Siku hiyo tutajua mbichi na mbivu .
Wasalaam.