huenda ni kwa sababu izi na zingine wazijuazo/nisizozijua
-Katika sura ya 222 Barnaba anaeleza kuwa Yesu Kristo hakusulubiwa, aliondolewa na Malaika, kisha Yuda alisulubiwa badala yake.
-Katika sura ya 44 Barnaba anaeleza kuwa Ibrahimu alimtoa Ishmaeli awe sadaka katika madhabahu, na anamwita Mungu wa Ibrahimu, Ishmaeli na Yakobo.
-Barnaba anamweka mtume Muhammadi kama mbadala wa Yesu kristo, angalia sura ya 44, 45, 9, 112, 39 na nyinginezo ktk kitabu hicho
Barnaba katika biblia (
sijajua ni toleo la ngapi)
-Kuonyesha jinsi Mungu alivyowachagua Barnaba na Sauli kwa mara ya kwanza kuihubiri Injili za
mbali, wakianzia na Kipro. Ingawa Wayahudi wengi waliiamini Injili na kubatizwa, lakini wengi wao
walikuwa ndiyo maadui wa Kweli.Kwa hiyo wanafunzi walisafiri nchi za mbali na wakatanyika kwenda
sehemu mbalimbali ulimwenguni na Injili ya Neno la Mungu ikihubiriwa kwa Wayahudi na kwa watu
wa Mataifa.(Matendo ya Mitume 11:19-26; 13:1-13)
-Upande wa Kaskazini wa Yudea, katika nchi ya Shamu (Syria) palikuwa na Antiokia, mji ambao
ulikuwa mkubwa sana na maarufu. Wanafunzi waliotoka nchi za mbali walikuja katika mji huu na
wakahubiri watu wengi katika mji huu na watu wengi sana wakaongoka kwa kuiamini Kweli. Eklesia
kubwa ikaanzishwa na ''watu wengi wakaongezeka kwa upande wa Bwana''. Eklesia ya
Yerusalemu ikamtuma Barnaba ili awaimarishe na kuwatia moyo waamini wapya ambao wengi wao
walikuwa ni watu wa Mataifa. Sauli wakati huo alikuwa amerudi Tarso, mji wa nyumbani kwao, naye
Barnaba akasafiri umbali upatao kama km 200 kutoka Antiokia kumtafuta Sauli na kumleta hadi
eklesia ya Antiokia. Wakafanya kazi ya kufundisha watu muda wa mwaka mzima (Matendo ya
Mitume 11:24-26). Antiokia (katika Syria au Shamu) ulikuwa ni mji ambao mkuu katika kuhubiri Injili.
Licha ya Barnaba na Sauli kuhubiri, lakini walikuwepo wengine pale ambao ni walimu na manabii na
wakati sasa ulifika Injili ihubiriwe zaidi kwa watu wa Mataifa (Matendo ya Mitume 11:24-25). Na ikuwa
ni hapa Antiokia ambapo ''wanafunzi waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza'' (Matendo ya
Mitume 11:26) ikiwa na maana ya “wafuasi wa Kristo''.
-Siku moja, ndugu hawa walipokuwa pamoja wakimwabudu Mungu, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia” (mstari 2). Kwa hiyo pamoja na maombi ya ndugu wa Antiokia ye kuwatia moyo, Barnaba na Sauli wakatengwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya safari nyingi na ndefu katika kumtumikia Kristo. (Matendo ya Mitume13:1-3)
-WANAKWENDA KISIWA CHA KIPRO (mstari 4-8 )
Walipoondoka Antiokia, wakaenda Seleukia, ambayo ndiyo bandari iliyokuwa karibu sana,
wakasafiri na Meli kwenda Kipro ambacho ni kisiwa kikubwa upande wa Mashariki wa bahari ya
Mediteraniani. Barnaba alikuwa mzaliwa ni Kipro (Matendo Mitume 4:36) na sasa alitakiwa kupeleka
ujumbe wa Injili aliousikia na kuuamini katika nchi yake. Na pia katika safari alimchukua Yohana
Marko, mpwa wake ili awasaidie katika kazi hii maalumu. Ikawa meli ilipofika bandari ya Salami, hawa
ndugu wakawa wa kwanza kuingia katika sinagogi na wakahubiri pale. Kisha wakatembea kwa miguu
mpaka Pafo mji mkuu wa Kipro. Liwali wa Kirumi Sergio Paulo, akataka kusikia Neno la Mungu
kutoka kwao. Alikuwa ni mtu mwenye akili sana na alikuwa amevutiwa sna na ujumbe ambao aliusikia
ndugu hawa watatu walipokuwa wanahubiri. Lakini alikuwa na Myahudi aliyeitwa Bar Yesu (na
alijulikana kwa jina la Elima, mchawi au mtu afanyaye ushirikina), ambaye alikuwa ni nabii wa uongo.
Elima alibishana na Barnaba na Sauli, maana aliweza kuona kuwa Liwali alipenda sana Injili na yeye
akataka kumgeuza nia ili asiikubali ile imani na hivyo asiendelee kuisikiliza Injili.
ELIMA ANAADHIBIWA (mstari 9-12)
Ikawa Elima alipozidi kulipinga Neno la Kweli, ndipo Sauli, hali akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia
macho, “Tazama mkono wa Bwana uko juu yako; nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa
muda” (mstari 11). Maana alikuwa adui wa haki yote, mpotoshaji, ambaye hakutaka Liwali aipokee
Kweli. Na sasa yeye mwenyewe anakuwa kipofu ghafla na anaomba watu wamwongoze kwa
kumshika mkono. Mungu alikuwa anamfundisha somo. Naye Liwali akastaajabu sana. Mwujiza huu
wa kumpofusha Elima ulisababisha Liwali aamini mambo yale aliyokuwa ameanza kuamini.
SASA SAULI ANAITWA PAULO (mstari 9)
Utaona kuwa kuanzia wakati huu, katika maandiko ya Luka aliyoyaandika katika Kitabu cha
Matendo ya Mitume, Sauli anaitwa Paulo, ikiwa na maana ya “mdogo”. Anajulikana kuwa ni “Mtume
kwa watu wa Mataifa”, kwa sababu kazi yake kubwa ilifanyikia kwa watu wa Mataifa.
WIKIPEDIA
--
Mtume Barnaba' (jina la awali Yosefu wa Kupro) alikuwa Myahudi wa kabila la Lawi wa karne ya 1 BK.
Anajulikana hasa kwa jina la Barnaba (kwa Kiaramu בר נביא, bar naḇyā, yaani 'mwana wa nabii'. Lakini Luka mwinjili (kitabu cha Matendo ya Mitume 4:36) alilitafsiri kwa Kigiriki υἱός παρακλήσεως, huios paraklēseōs, yaani "mwana wa faraja" au "mwana wa himizo".
--
Mapokeo yanasema aliuawa kwa ajili ya imani yake huko Salamis, Kupro, mwaka 61.
Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, Waanglikana na Walutheri wanamheshimu kama mtakatifu tarehe 11 Juni.
Wataalamu wengine wanamtaja kama mtunzi wa Waraka kwa Waebrania, na Klemens wa Aleksandria alimtaja kama mwandishi wa Waraka wa Barnaba, lakini hakuna hakika.
--Katika kitabu hicho cha Agano Jipya (Biblia ya Kikristo) tunapata habari kuwa aliongokea mapema Ukristo, akauza shamba lake na kuwakabidhi Mitume wa Yesu mapato yake ili wawasaidie maskini. Labda kwa sababu hiyo Mitume walimuita Barnaba (Mdo 4:36-37).
Kisha kuheshimiwa hivyo katika Kanisa la awali huko Yerusalemu, alimtambulisha na kumdhamini Mtume Paulo muda mfupi baada ya huyo kuongoka huko Damasko (Mdo 9:26Katika kitabu hicho cha Agano Jipya (Biblia ya Kikristo) tunapata habari kuwa aliongokea mapema Ukristo, akauza shamba lake na kuwakabidhi Mitume wa Yesu mapato yake ili wawasaidie maskini. Labda kwa sababu hiyo Mitume walimuita Barnaba (Mdo 4:36-37). -28).
Watu wa mataifa walipoanza kuingizwa moja kwa moja katika Ukristo mjini Antiokia, alitumwa huko kwa niaba ya Kanisa mama, akawa kiongozi mkuu wa jumuia hiyo mpya (Mdo 11:19-30; 13:1).
Baadaye Roho Mtakatifu alidai yeye na Paulo wapelekwe kufanya umisionari sehemu nyingine, wakaondoka pamoja na binamu yake, Yohane Marko, kuelekea kwanza kisiwani Kupro, halafu bara, katika maeneo ya Uturuki Kusini wa leo (Mdo 13:2-14:28).
Kazi yao ilipopata upinzani kwa sababu ya kutodai Wapagani wakiongoka washike Torati yote, walikwenda pamoja Yerusalemu (mwaka 49 hivi, kwa mtaguso wa Mitume, ambao uliamua kuhusu suala hilo (Mdo 15:1-35).
Baada ya kutengana na Paulo, Barnaba alifunga tena safari kwenda Kupro pamoja na Marko (Mdo 15:36-39) kati ya miaka 50 na 53.
Baada ya hapo hatuna tena habari ya hakika juu yake, ila Mtume Paulo alimtaja kama mfano wa mtu asiye na mke kwa ajili ya uinjilishaji (1Kor 9:16-22).