Kwanini Iran imeshindwa kumlinda mshirika wake Hezbollah na Hamas?

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
242
Reaction score
676
Mkuu wa Hezbollah, Hassan Nasrallah amepotezwa

Kiongozi huyu mwenye ushawishi mkubwa (charsmatic leader) ameiongoza Hezbollah kwa miaka 33 yaani kutoka 1992 hadi 2024. Alikuwa nyota kuu ya Hezbollah, Hamas, Iran na vikosi vyote vya kishia duniani. Pia alikuwa ni kipenzi kikubwa cha Ayatollah Khomein, alimwita mtu na nusu. Lakini kwa Israeli, Nasrallah alikuwa ni gaidi na mtu aliyewindwa sana. Kuna muda Israeli na Hezbollah ziliacha mivutano hasa baada ya vita vya 2006 vilivyoingiliwa na UN na kuomba majeshi ya Israeli yatoke Lebanon. Tokea hapo Hezbollah ilijiimarisha sana na kuwa kundi la kijeshi kubwa sana katika makundi yote mashariki ya kati. Likawa kundi lenye nguvu kuliko hata serikali ya Lebanon likiwa na wanajeshi 100,000. Kuna muda Hezbollah walitunishiana misuli na serikali ya Beirut na kuishinda. Hezbollah kwa sehemu kubwa ilisaidia serikali ya Siria inayoongozwa na Bashar al Assad isianguke mikononi mwa vikundi vya kisuni vilivyokuwa vinadhaminiwa na Saudia Arabia na Marekani. Hivyo Hezbollah ya Nasrallah ilikuwa ni taa na tumaini kwa wapiganaji wa kishia na wote ambao wanachukizwa na Israeli.

Mtafaruku mkubwa

Lakini kuanzia October 7, Hezbollah iliunga mkono shambulio la Hamas kwa Israeli lililoua zaidi ya watu elfu. Na haikuishia hapo Nasrallah akatangaza kuiunga Hamas, hivyo akaanza kujibu mashambulizi kwa niaba ya Hamas dhidi ya Israeli. Tokea hapo serikali ya Netanyahu ikaanza mikakati ya kulivunja kundi la Hezbollah. Ikawa inajibu mashambulizi kwa kuua viongozi wandamizi wa Hezbollah na Hamas kwa kufuatwa pale walipo. Tokea hapo Nasrallah akaanza kujificha kwenye mahandaki makubwa.

Hezbollah ilikuwa inapenyesha wanajeshi wake kwa kivuli cha Hamas kuishambulia Israeli. Pamoja na hilo Nasrallah kupitia Ibrahimu Qubais, kamanda mkuu wa kikosi cha makombora cha Hezbollah wakawa wanatupa mvua ya makombora huko Israeli ambayo kwa idadi iliyotolewa na jeshi la Israeli yapata 8000. Na hawa wote wameuawa kwa kupishana siku moja. Israeli baada ya kuivunja nguvu ya Gaza na Hamas, mwezi huu waligeukia upande wa kaskazini ili kupigana na Hezbollah. Wakiwa na hasira dhidi ya makombora ya Hezbollah yaliyoharibu makazi ya miji ya kaskazini mwa Israeli na kuua. Netanyahu alitangaza vita na kundi hili akiahidi kung'oa mizizi yake, na akatoa taarifa hadi UN akisema hatasikiliza chochote hadi atimize kusudi lake la kuwaondolea mbali maadui wote wa Israeli.

Nasrallah baada ya kuona kiongozi mmoja baada ya mwingine anauawa na IDF, akaamua kukimbilia kwenye ngome kuu ya Hezbollah inayoaminika. Lakini inteligensi ya Israeli ikawa inamfuatilia kwa karibu. Na juzi alipoonekana anaingia katika handaki kubwa ambalo ndio makao makuu ya Hezbollah jijini Beiruti. IDF hawakupoteza muda, kwa kasi walimfuata kwa bomu linaloitwa bunker buster bomb lilirushwa na ndege vita. Bomu hili lilitengenezwa maalum kwa kuvunja mahandaki yenye urefu wa kuanzia mita 30 na lenye uwezo hadi wa kutokeza tetemeko la ardhi lenye kipimo cha uzito cha 3.9. Hivyo likipigwa si rahisi adui akatoka salama. Na ndio maana baada ya sinema hiyo, Israeli bila hofu ilitangaza kwa kujiamini kwamba Nasrallah ni marehemu. Hezbollah ilikanusha lakini muda umekuwa majibu. Maana Nasrallah hapatikani wala mwili wake. Na handaki hilo walikuwemo viongozi wengine wa Hezbollah pamoja na mkuu wa kikosi cha Revolution guard cha Iran. Wote wameuawa.

Iran imeumia sana pamoja na ulimwengu wa kishia kwa tukio hilo lililomwondoa hero wao. Iraq imetangaza maombolezo ya siku tatu. Na Ayatollah Khomenei ametangaza maombolezo pia, pamoja na hilo amevitaka vikosi vyote vya kijeshi vya kishia kuwa nyuma ya Hezbollah dhidi ya Israeli. Na ameonya kutokea vita vikubwa mashariki ya kati. Israeli imejibu ipo tayari kwa lolote. Na juzi Netanyahu alisema hivi juu ya Iran:

"hakuna mahali nchini Iran" ambapo "mkono mrefu" wa Israeli hauwezi kufikia, na "hiyo kwa Mashariki ya Kati yote".

Baada ya kauli hiyo, Nasrallah na mkuu wa kikosi cha Revolution guard wa Iran, wakauawa. Hezbollah wamejibu kifo cha bosi wao kwa kurusha rundo la makombora kaskazini mwa Israeli leo. Na Israeli imejibu kwa kufanya shambulio lingine jijini Beiruti na miji mingine na kuua mamia. Sasa wanajipanga kuingia ndani ya Lebanon kijeshi ili kukabiliana na majeshi ya Hezbollah, hivyo wametangaza raia wa Lebanon waondoke katika miji hiyo. Sasa Walebanoni takribani 50,000 wamekimbilia Siria kuepuka vita.

Hadi sasa wakuu 18 muhimu wa Hezbollah akiwemo Hassan Nasrallah wameuawa na jeshi la Israeli. Ni hasara kubwa sana ambayo ni ya kihistoria. Israeli inatumia mbinu hii: mpige mchungaji na kondoo watatawanyika.

Je, Hezbollah wataweza kuhimili kishindo cha Israeli yenye tekinolojia kubwa na intelijensia ya kutosha? Na je Israeli itaweza kulitokomeza kundi hili machachari? Na je Iran wataweza timiza maneno yao ya kuisaidia Hezbollah kijeshi?

Tusubiri.

1727548825112.jpg
 
Haijawahi kuishi na wavaa kobazi ni wanafki sana tena sana

USSR
 
Huruma yangu ni kwa raia wa Lebanon. Hii vita haiwahusu kabisa.
 
Wewe unaenda mbali sana kwani mungu wao aliweza?
 
Je Hezbollah wataweza kuhimili kishindo cha Israeli yenye tekinolojia kubwa na intelijensia ya kutosha? Na je Israeli itaweza kulitokomeza kundi hili machachari? Na je Iran wataweza timiza maneno yao ya kuisaidia Hezbollah kijeshi?

Tusubiri.
Iran wana long term strategy ya stability ili wapate nuclear bomb wakati Nasra yeye alitaka full vita na Israel, so ni better kumuondoa aje kiongozi mwingine atakasitisha migogoro na Israel. Same hata kwa yule wa Hamas, he was idiot kufikiri anasaidia. Na angalia those factions za hamas na hezbolla zilianza kuwa na nguvu dawa ni Iran kuzipunguzia nguvu. Same kwa Houthi nao very soon watapelekewa fire
 
Vita ni tukio baya sana! Thamani ya utu na uhai hupotea kirahisi sana uwanja wa machafuko,waisrael ni katili sana , lebanon itageuka magofu kama gaza.
 
Mkuu wa Hezbollah, Hassan Nasrallah amepotezwa

Kiongozi huyu mwenye ushawishi mkubwa (charsmatic leader) ameiongoza Hezbollah kwa miaka 33 yaani kutoka 1992 hadi 2024. Alikuwa nyota kuu ya Hezbollah, Hamas, Iran na vikosi vyote vya kishia duniani. Pia alikuwa ni kipenzi kikubwa cha Ayatollah Khomein, alimwita mtu na nusu. Lakini kwa Israeli, Nasrallah alikuwa ni gaidi na mtu aliyewindwa sana. Kuna muda Israeli na Hezbollah ziliacha mivutano hasa baada ya vita vya 2006 vilivyoingiliwa na UN na kuomba majeshi ya Israeli yatoke Lebanon. Tokea hapo Hezbollah ilijiimarisha sana na kuwa kundi la kijeshi kubwa sana katika makundi yote mashariki ya kati. Likawa kundi lenye nguvu kuliko hata serikali ya Lebanon likiwa na wanajeshi 100,000. Kuna muda Hezbollah walitunishiana misuli na serikali ya Beirut na kuishinda. Hezbollah kwa sehemu kubwa ilisaidia serikali ya Siria inayoongozwa na Bashar al Assad isianguke mikononi mwa vikundi vya kisuni vilivyokuwa vinadhaminiwa na Saudia Arabia na Marekani. Hivyo Hezbollah ya Nasrallah ilikuwa ni taa na tumaini kwa wapiganaji wa kishia na wote ambao wanachukizwa na Israeli.

Mtafaruku mkubwa

Lakini kuanzia October 7, Hezbollah iliunga mkono shambulio la Hamas kwa Israeli lililoua zaidi ya watu elfu. Na haikuishia hapo Nasrallah akatangaza kuiunga Hamas, hivyo akaanza kujibu mashambulizi kwa niaba ya Hamas dhidi ya Israeli. Tokea hapo serikali ya Netanyahu ikaanza mikakati ya kulivunja kundi la Hezbollah. Ikawa inajibu mashambulizi kwa kuua viongozi wandamizi wa Hezbollah na Hamas kwa kufuatwa pale walipo. Tokea hapo Nasrallah akaanza kujificha kwenye mahandaki makubwa.

Hezbollah ilikuwa inapenyesha wanajeshi wake kwa kivuli cha Hamas kuishambulia Israeli. Pamoja na hilo Nasrallah kupitia Ibrahimu Qubais, kamanda mkuu wa kikosi cha makombora cha Hezbollah wakawa wanatupa mvua ya makombora huko Israeli ambayo kwa idadi iliyotolewa na jeshi la Israeli yapata 8000. Na hawa wote wameuawa kwa kupishana siku moja. Israeli baada ya kuivunja nguvu ya Gaza na Hamas, mwezi huu waligeukia upande wa kaskazini ili kupigana na Hezbollah. Wakiwa na hasira dhidi ya makombora ya Hezbollah yaliyoharibu makazi ya miji ya kaskazini mwa Israeli na kuua. Netanyahu alitangaza vita na kundi hili akiahidi kung'oa mizizi yake, na akatoa taarifa hadi UN akisema hatasikiliza chochote hadi atimize kusudi lake la kuwaondolea mbali maadui wote wa Israeli.

Nasrallah baada ya kuona kiongozi mmoja baada ya mwingine anauawa na IDF, akaamua kukimbilia kwenye ngome kuu ya Hezbollah inayoaminika. Lakini inteligensi ya Israeli ikawa inamfuatilia kwa karibu. Na juzi alipoonekana anaingia katika handaki kubwa ambalo ndio makao makuu ya Hezbollah jijini Beiruti. IDF hawakupoteza muda, kwa kasi walimfuata kwa bomu linaloitwa bunker buster bomb lilirushwa na ndege vita. Bomu hili lilitengenezwa maalum kwa kuvunja mahandaki yenye urefu wa kuanzia mita 30 na lenye uwezo hadi wa kutokeza tetemeko la ardhi lenye kipimo cha uzito cha 3.9. Hivyo likipigwa si rahisi adui akatoka salama. Na ndio maana baada ya sinema hiyo, Israeli bila hofu ilitangaza kwa kujiamini kwamba Nasrallah ni marehemu. Hezbollah ilikanusha lakini muda umekuwa majibu. Maana Nasrallah hapatikani wala mwili wake. Na handaki hilo walikuwemo viongozi wengine wa Hezbollah pamoja na mkuu wa kikosi cha Revolution guard cha Iran. Wote wameuawa.

Iran imeumia sana pamoja na ulimwengu wa kishia kwa tukio hilo lililomwondoa hero wao. Iraq imetangaza maombolezo ya siku tatu. Na Ayatollah Khomenei ametangaza maombolezo pia, pamoja na hilo amevitaka vikosi vyote vya kijeshi vya kishia kuwa nyuma ya Hezbollah dhidi ya Israeli. Na ameonya kutokea vita vikubwa mashariki ya kati. Israeli imejibu ipo tayari kwa lolote. Na juzi Netanyahu alisema hivi juu ya Iran:

"hakuna mahali nchini Iran" ambapo "mkono mrefu" wa Israeli hauwezi kufikia, na "hiyo kwa Mashariki ya Kati yote".

Baada ya kauli hiyo, Nasrallah na mkuu wa kikosi cha Revolution guard wa Iran, wakauawa. Hezbollah wamejibu kifo cha bosi wao kwa kurusha rundo la makombora kaskazini mwa Israeli leo. Na Israeli imejibu kwa kufanya shambulio lingine jijini Beiruti na miji mingine na kuua mamia. Sasa wanajipanga kuingia ndani ya Lebanon kijeshi ili kukabiliana na majeshi ya Hezbollah, hivyo wametangaza raia wa Lebanon waondoke katika miji hiyo. Sasa Walebanoni takribani 50,000 wamekimbilia Siria kuepuka vita.

Hadi sasa wakuu 18 muhimu wa Hezbollah akiwemo Hassan Nasrallah wameuawa na jeshi la Israeli. Ni hasara kubwa sana ambayo ni ya kihistoria. Israeli inatumia mbinu hii: mpige mchungaji na kondoo watatawanyika.

Je Hezbollah wataweza kuhimili kishindo cha Israeli yenye tekinolojia kubwa na intelijensia ya kutosha? Na je Israeli itaweza kulitokomeza kundi hili machachari? Na je Iran wataweza timiza maneno yao ya kuisaidia Hezbollah kijeshi?

Tusubiri.
UKITUPIGA TUTAKUPIGA
#CHUMA NETANYAHU#
 
Back
Top Bottom