Kwanini JamiiForums hamtaki kuanzisha AI yenu?

Ungeanza kuelezea tatizo unaloliona halafu lijadiliwe kwa undani ili kulitafutia suluhisho, wewe umeanza na suluhisho (Akili Mnemba) bila kuleta tatizo linaloeleweka...AI is not a panacea !
 
Nipe Elimu ni mambo gani hayo ingesaidia Mkuu
Kwa mfano GPT 3 iligharimu karibia dola milion 4, lakini hiyo ni broad na ipo kwa lugha na upana wote. Hii ya JF itakuwa ya upana mdogo na hata lugha yaweza kuwa chache zile maarufu. Mfano sasaivi ukitaka kujua kuhusu Gentlemen_ hauwezi kupata, nikitaka kujua ni thread yako ipi ilikuwa na likes nyingi pia siwezi jua. Uwepo wa AI utarahisisha ile query ya kusearch mpaka kichwa kiume.
 
Duuuh mimi nipo nyuma kweli hayo mambo ya AI naishia kuyasoma tu Jf. Sijui hata matumizi yake
 
Watu wa JF wanapenda Sana "Anonymity" na ndiyo maana wengi wao wamefunga profile Yao.

Sasa watu hiyo unayosema inasabibsha kichwa kuuma ndiyo wanaita U -JF wenyewe😄
 
Gpu moja tu ya kutrain AI inauzwa kama milioni 70, sio project za kitoto hizi zinataka mpunga mrefu.

Hao deepseek wanaosifika kutengeneza AI ya bei rahisi wametumia Gpu 50,000 ambayo ni Ma Trilioni ya hela hayo.
 
JF ina Sera zake, ukitak kujua ishu za mtu (kama hapo ulipoelezea) Privacy itakuw ndogo. Ndio maana ktk baadhi ya profiles kuna limit huwez view threads au contents (Restrictions).

Maybe useme watumie API na other automation mechanisms kwa ajili yao wao kama wao ktk shughuli za uendeshaji.
 
Gpu moja tu ya kutrain AI inauzwa kama milioni 70, sio project za kitoto hizi zinataka mpunga mrefu.

Hao deepseek wanaosifika kutengeneza AI ya bei rahisi wametumia Gpu 50,000 ambayo ni Ma Trilioni ya hela hayo.
Kwa mtazamo wako Kaka, kati ya DeepSeek na ChatGPT, ipi unaona ni bora zaidi na kwa nini?
 
Ufafanuzi please
AI itakuwa inafanya kazi gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…