Kwanini JK (Kanali nusu mstaafu) hana ushawishi kwa Kagame (Jenerali Mstaafu)



Ulichoongea/ulichoandika kina mashiko......LAKINI haiondoi ukweli na substance ya USAHURI aliopewa President Kagame.......kwa jinsi ulivoaandika...sisi kama wanadamu basi tutegemee Malaika tu ndio waje watushauri......!!



Mkuu........chuki na hila za President Kagame kwa Taifa letu zinajulikana muda mrefu......Kagame amekuwa "haambiliki"...ukifuatilia mahusiano yetu na Rwanda kwa Takriban miaka sita hivi kwa karibu utatambua nini huyu jamaa amekuwa akifanya........kama ni u-snitch....basi huyu jamaa ni kafuzu mafunzo kutoka KENYA........

Wakenya siku zote wamekuwa against na maendeleo ya Taifa letu na wanafanya hivyo mchana kweupe....tena Wakenya ndio ma-snitch viongozi hapa EAC......eti wanajifanya wanataka shirikisho.........sihitaji kukueleza mengi kuhusu jinsi gani wakenya wanvyolihujumu Taifa letu........sasa wamepata kijana Kagame....wanatumia u-snitch wao ili Kagame asitumie Bandari yetu........now they are together.........

Kenya na Rwanda ni wabinafsi sana na wana dharau sana....wanafikir wamepata intelijensia ya kutosha ya kutusambaratisha.......yeah inawezekana kwa kiwango fulani....lakini......"yo" wasijidanganye...we know them better than they think they know us........ndio maana hii EAC wengine wanchukulia kama vehicle fulani hivi kiuchumi........if you know what I mean......kumbuka Mzee Jomo aliwaambia Wakikuyu...msije mkathubutu kuwaachia Wajaluo wakashika nchi hii.....this also applies to Rwanda.......we know the history even deeper in their vikaos..........
 

Mkuu....nilikuwa Kigali na pembezoni mwake for about 18 months two years baada ya mauaji ya Kimbari.......being a Tanzanian wengi niliokuwa nafanya shughuli nao i.e. wahutu na watutsi.....wana hisia za chuki kali sana miongoni mwao........Paul Kagame has been trying to show outsiders kuwa he is for real to bring amani in Rwanda......but just check this out......"Just a simple and humble USHAURI" ona alivyo-react!!.......I like Kagame kwenye utendaji kazi kwa maendeleo ya nchi....lakini kwa hili la kutafuta suluhu/amani....I don't like him at all......ni Mwanajeshi kweli kweli..... si mchezo.......

.......sikuwashangaa wale mawaziri wake na senior officers wake walivyokuja na matusi not only kwa JK bali hata kwa Watanzania.....mengine hayasemwi na vyombo vya habari (i.e.. edited news......hizi dharau na chuki ndio order of the day kwenye vikao vyao vingi)......maana mtafaruku wake ni mkubwa......lakini watu wa mipakani wanafahamu ndio maana kuna tension kule......hivi sasa......CDF Mwamunyange meant what he said that day....because he had to......achilia mbali ya kuambia aseme na JK..........

...kamwambie leo Mkikuyu akubali kuongozwa na Mjaluo......uone reaction yake.......leo President Uhuru anatake side!.....
 
Angelijibiwa vivyo hivyo. Alichopaswa JK kufanya ni kupeleka maoni yake EAC na wala siyo kumwaga mtama kwenye kuku wengi........

I doubt it na kinachonifanya niwe na doubt na hilo is the timing of these events.

Siko interested na kujadili ushenzi au usafi wa Kagame au kuhusiana na ushauri alioutoa JK, whether ulikua sahihi au ulifuata proper channels et al, ila kwanini PK alimjibu JK kwa kejeli na dharau kubwa?

Anapata wapi hicho kiburi, anajiamini na nini mpaka kumwambia 'I will hit you', mbona anapewa ushauri kama huo wa JK na watu au taasisi mbalimbali lakini hawajibu hovyohovyo kama alivyomjibu Rais wetu?

Ila je ni PK tu katika ukanda wetu aliyegain confidence kwamba, NOW naweza kusema au kufanya chochote bila kujali kitakua na impact gani kwenye mahusiano na Tanzania.

Kwa nini Malawi wameanza chokochoko zao wakati huu?
kwa nini Kenya, Uganda zimeamua kujenga uhusiano wa karibu zaidi wa kiuchumi na Rwanda na sio Tanzania, kwa maana nyingine kwa nini wameitenga Tanzania?
Je ndani ya Tanzania hali ikoje, majibu unayo.

My opinion on the matter ni kuwa PK na wote wanaotake aim at Tanzania wanapata nguvu kutokana na siasa za ndani za nchi yetu, uongozi na siasa mbovu na madudu yote yanayotokea nchini ndio yanawapa nguvu kina Kagame kumkejeli JK bila wasiwasi.

Kama JK alishaitwa Rais dhaifu ndani ya bunge, ni nini kitamfanya Kagame apokee ushauri wa Rais dhaifu ambaye mambo ya nyumbani kwake yamemshinda, atasema nini kuhusiana na nyumba ya jirani?

Like I said, Respect is earned not given.
 

Ndiyo maana nilisema kwenye post tangu hapo juu kuwa tatizo hili suala linajadiliwa na watu wengi too emotionally, subjectively, and sometimes, irrationally.

Mourinho kahoji vizuri hapo juu. "
Kama JK alishaitwa Rais dhaifu ndani ya bunge, ni nini kitamfanya Kagame apokee ushauri wa Rais dhaifu ambaye mambo ya nyumbani kwake yamemshinda, atasema nini kuhusiana na nyumba ya jirani?"

Kila wakati watu wengi hapa JF wanalalama kuwa Rais wao ni "dhaifu", kwamba ameshindwa kuongoza nchi, nk. Lakini watu hao hao wako mstari wa mbele kudai kuwa rais wa nchi nyingine angekubali tuu ushauri uliotolewa na Rais wao wanayemwitwa "dhaifu".

Hivi Rais anaweza kuwa "dhaifu" katika masuala ya ndani ya nchi yake lakini asiwe "dhaifu" kwenye masuala ya nje ya nchi?

Kama wananchi wake wanasema Rais wao ni "dhaifu", ni Rais gani wa nchi nyingine atakayekubali ushauri wa Rais anayedaikuwa ni "dhaifu"?

Kuna jamaaa nilikuwa naongea nae jana kuhusiana na hili suala akaja na point kuwa kutokana na Rais kuelemewa nchini, kutokana na kupungua kwa legitimacy yake mbele ya wananchi wengi, kutokana na wananchi wengi kumchoka, kutokana na wananchi wengi kugawanyika kivyama, nk, basi suala la Kagame linaweza kutumiwa kurudisha heshima ya JK na serikali yake.

Why? Kwa sababu katika watu ambao ni wanafiki, wasahaulifu na wanaopenda kuendekeza ushabiki for the sake of it, Watanzania wanaongoza. Watu wengi wanaelekea kusahau masuala ya msingi ya ndani ya nchi, badala yake wamejikita kwenye bifu za JK na Kagame.
 

Utasemaje kama mtu akisema kuwa JK anatumia suala la Kagame kuhamisha Watanzania kujadili masuala nyeti ya ndani ya nchi?

Pia ni sawa kwa Rais wa nchi nyingine kukubali ushauri uliotolewa na Rais ambaye wananchi wake wanamwita ni "dhaifu"?

Kwa nini wananchi wamwite Rais wao ni "dhaifu", halafu Rais huyo huyo asitoe ushauri "dhaifu" kwa Rais wa nchi nyingine?

Kama tunakubaliana kuwa ushauri alioutoa Rais Kikwete ulikuwa siyo "dhaifu", basi tukubaliane kuwa Rais wetu siyo "dhaifu".
 
Mkuu kwenye siasa sio lazima A iwe B na B si lazima iwe A, lakini A ni B, na A ni A na B ni B na B ni A. Maana yangu ni kuwa siasa si sawa na hisabati ambayo 1+1=2, siasa haina kanuni. Inawezekana kuwa JK ni dhaifu wa mambo ya ndani, kwa kuwa hakuwa na experience hata kidogo ya mambo hayo wakati anaingia madarakani, na kwa kuwa hakuingia madarakani kwa njia ya kistaarabu. Na hata hivyo ukiwa mdhaifu kwenye masomo ya lugha, huenda si mdhaifu kwenye masomo ya hesabu au jiografia. Ukiangalia kwenye jukwaa la siasa za kimataifa perfomance yake si mbaya, kwa kuwa walau alijifunza mengi kwa miaka 10 ya uwaziri wa mambo ya nje.

Ningethibisha kuwa JK ni dhaifu kama angesema tuichape Malawi, lakini alitoa kauli ya u-stateman na si ya kihuni, au angeshauri Rwanda iendelee kuwaua FDLR nchini DRC, na yeye asingekuwa tofauti na hao FDLR na M23.

Mkuu kingine ni vizuri tukumbuke kuwa hapa Tanzania tunamwita JK kama tunavyopenda kwa kuwa tuna uhuru huo. Kagame ni very strong ndani, na ameonesha utendaji wa hali ya juu ambao hata watanzania tuna admire, lakini no doubt nje Kagame ni complete failure. Amekosana na M7, JK, JK wa DRC, Laurent Kabila, na wengine wengi tu kimsingi hana jirani wa maana, ila yeye tu ndio wa maana kuliko wote. In fact anaijenga vizuri Rwanda kwa ndani, lakini anaibomoa vibaya sana kwa nje, na anahatarisha uhamasa wa watusi (wa Rwanda na nje ya Rwanda) kwa kuingiza zaidi hisia za uhutu na utusi ndani ya mioyo ya wanyarwanda, na kuwafanya watu wengine wasio wahutu waanze kuwachukia watusi.
 
wakuu michango yenu imesababisha nibadilishe msimamo wangu, kweli kauli ya JK hakupaswa kuitoa, naunga mkono hoja.
 
Reactions: SMU

Sikubaliani na analysis yako ya masomo na kiongozi. Kiongozi mkuu wa taifa anachaguliwa kwa kuangalia vigezo vya ndani na nje ya nchi. Lazima kiongozi awe na uwezo or at least understanding ya ku kudeal with both national and international issues.

Halafu siyo suala la Kagame tuu; yapo masuala mengine ya kimataifa ambayo Rais ameshiriki na still watu wakamwita ni "dhaifu".

Who knows, inawezekana Kagame anamdharau JK kwa sababu anaona hata baadhi ya Watanzania wanamwona ni "dhaifu" na JK anamtumia Kagame ili asionekane kama ni "dhaifu" mbele ya baadhi ya wananchi wake wanaoamini hivyo.

Tukukubali au tukatae kuwa Rais wetu ni "dhafu". Lakini hai-make sense kabisa kusema kuwa Rais ni "dhaifu" ndani ya nchi lakini si "dhaifu" nje ya nchi. What sort of President would that be?
 

Unatakiwa kuangalia suala la mgogoro ndani ya Maziwa Makuu kwa jicho lingine.....hili suala ni zaidi ya JK unayemfahamu....ukichukulia kirahisi rahisi na hizi siasa zetu za kuitana dhaifu.....hutaelewa muktadha mzima wa mgogoro uliopo........it is deeper than most of the persons might think.......
 

.....the point aliyoitoa huyo jamaa ni very weak.....hii nchi inakuwa kidemokrasia...ideologies za vyama mbali mbali zinakuwa siku hadi siku....na watu/vikundi mbali mbali vinaanza kuamka na kuelewa maana ya demokrasia....watu wengine mnaita mgawanyiko.......lakini kukua huku hakuwezi kumzuia Rais wa nchi kufanya lile linalotakiwa kufanya in that capacity..........Huyo jamaa atakuwa dhaifu kimawazo/kifikira......I'm sorry!......

...Kama Tanzania, msimamo wetu kuhusu amani unaeleweka.......usuluhishi wa suala la Rwanda na waasi wake lilianza na JKN (RIP)....Mandela (naye yuko hoi).. nk nk...ni kitu gani cha ajabu alichokisema JK ambacho Mwl JKN au Mandela wasingesema.........Mandela alipoingia tu madarakani akaanza na reconciliation....mara nyingi hapa tunasema JKN (RIP) naye alikuwa dhaifu na sera zake za kiuchumi.........kwa hiyo naye alikuwa anatafuta nini kule kwenye reconciliation ya Rwanda!.......hivi katika watu wote hapa East Africa....hivi leo ndio Watanzania tuwe wa kwanza kuamsha ugomvi na Rwanda!!...CAN YOU BELIEVE THAT??....ooh PLEASE.......of all the people....TANZANIA!.....do you know what we went through during and after genocide........yaani Paul Kagame leo anatuita Watanzania 'genociders"....eti kwa kuwa tumemwambia a-reconcile!!??

......ni wakati umefika sasa PK aache arrogance/revenge attacks (amabzo zinaumiza na hata wasiokuwemo).....na utawala wa kibaguzi unaoendeleza chuki miongoni mwa wananchi wake.....na a-reconcile.......Yes, wale jamaa (genociders) walikimbilia DRC......na yeye PK aliivamia DRC mwaka 1996 ili kuwasaka na kuwaua genociders.......doing the same shit, (i.e. including DRC people who suffered)......killing thousands of civilians

Kagame na Museveni ni vijana/wanafunzi wetu....kama PK anafikiri arrogance yake ataileta Tanzania anajidanganya



.....waite Watanzania kitu kingine lakini sio unafiki........Watanzania si wanafiki.....
 

Kwa hiyo unataka kusema mgogoro ndani ya maziwa makuu unasababishwa na Kagame na Museveni?

Au hoja yako ni ipi Mkuu katika hilo?
 

Unaweza kudhibitisha kuwa Kagame amekosana na Museveni na hana jirani wa maana?

Hivi kwa nini kabla ya sisi kutoka na kuanza kutafuta udhaifu wa Kagame hatutaki kujichunguza wenyewe kwanza?

Je sisi ni wasafi? Je JK ni msafi, haui, je waandishi wa habari na wanaharakati hawauwawi nchini kwetu? Hawateswi kwa kunyofolewa meno na kucha? Majirani zetu wanasema nini kuhusu sisi? Wakenya wanatusemaje? Waganda na Wanyarwanda je?

Kwa nini watanzania tunapenda kujifanya ni wasafi, ni kisiwa cha amani wakati uhalisia hauko hivyo?

Kama Mkuu EMT alivyosema, tunajuaje hii serikali iliyoshindwa kabisa kuendesha nchi inautumia huu mzozo ili kuhamisha akili za watu na wasahau mabomu ya Arusha, mauaji ya kina Daudi Mwangosi, utekaji nyara wa kina Ulimboka na wengine, mauaji ya viongozi wa dini, mambo ya Muungano ambao ni wazi watu wa upande mmoja hawautaki kabisaa.
 
Reactions: EMT

Demokrasia gani inayokua wakati tunaona kuna nguvu za wazi kucounter check ukuaji wa demokrasia?

Mabomu Arusha, mauaji ya kina Mwangosi, mauaji yaliyoshindwa ya kina Ulimboka, usiri wa mikataba (tena ya hovyo) ambayo viongozi wetu wanaingia na wawekezaji wa nje, waziri mkuu kuruhusu Police kupiga wananchi na madudu mengine chungumbovu na mnayajua.

Huu ndio unaita ukuaji wa demokrasia? Labla kuna version nyingine ya demokrasia

Namuunga mkono EMT kuwa watanzania walio wengi ni WANAFIKI WAKUBWA. Mshindwe kuandamana kwa mauaji ya hadharani ya kina Mwangosi halafu yakuume sana mauaji ya Wanyarwanda na Wakongo, huu kama sio unafiki ni nini?
 
Kwa hiyo unataka kusema mgogoro ndani ya maziwa makuu unasababishwa na Kagame na Museveni?

Au hoja yako ni ipi Mkuu katika hilo?


.......hahahah.......interesting....
 

Labda uniambie jinsi unavyomfahamu JK zaidi ya mimi ninavyomfahamu.

Unaposema "ukichukulia kirahisi rahisi na hizi siasa zetu za kuitana dhaifu" kwa hiyo unakubali kuwa JK siyo "dhaifu" then?

Kama wewe unaujua zaidi muktadha mzima wa mgogoro uliopo ni utuambie mapema. Inawezekana labda ninahoji based on my ignorance ya huo mgogoro.
 

Mkuu you need to know that JK si mfalme. Ukiangalia kipindi chake cha kwanza cha utawala mambo yalikuwa ovyo sana, lakini term ya pili baada ya wakubwa wengine kumwambia anapeleka nchi kubaya, na kumuelekeza namna ya kuiendesha mambo yanabadilika. Kama JK would have been bad as some people wants us to believe, he would not be presiding the country today, angekuwa amebadilishwa. He has his weaknesses, but that does not make him weak in all fronts.
 
.....hii nchi inakuwa kidemokrasia...
Una maana gani kwa kusema demokrasia inakua? Kwa sababu tuna utitiri wa vyama vya siasa ambavyo havina hata mwelekeo? Au ni kwa sababu ya watu kupigwa na mabomu kwenye mikutano ya kisiasa? Ni creteria gani hasa unatumia kuonyesha kukua kwa demokrasia hapa nchini? Kwa sababu watu wanakamatwa na polisi wakiwa hai na mwisho kutolewa kituoni wakiwa wamekufa tayari kupelekwa mochwari? Au ni kwa sababu ya Waziri Mkuu kusema tupigwe tuu kwa sababu serikali imetuchoka? Au tumekuwa demokrasia iliyokua kiasi cha kulindwa na jeshi kule Mtwara? Au labda demokrasia imekua fasta baada ya Tendwa kustaafu?

ideologies za vyama mbali mbali zinakuwa siku hadi siku....
You must be joking! Aren't you? Vyama vipi hivyo? Kwanza, unaweza kuniambia jinsi ideology ya CCM inavyokuwa siku hadi siku? Vipi ile ya CUF ambayo wamejikuta wakiiruka wao wenyewe. Ndiyo kuonyesha ukuaji wake?

na watu/vikundi mbali mbali vinaanza kuamka na kuelewa maana ya demokrasia....watu wengine mnaita mgawanyiko

Vikundi gani hivyo unavyozungumzia? Green Guard? Red Brigade?

..lakini kukua huku [kwa demokrasia] hakuwezi kumzuia Rais wa nchi kufanya lile linalotakiwa kufanya in that capacity..........
Like what? Sijakuelewa una maana gani hapa.


Mkuu kama ulisoma post yangu ya mwanzo kabisa kwenye hii thread, nimeandika kuwa s
idhani kama ushauri alioutoa ni mbaya. Inawezekana kabisa kuwa substantively, ushauri wa Rais kwa Rwanda hauna tatizo. Lakini kabla ya kuyasema hayo hadharani, alishawahi kukaa informally au hata formally na Kagame na kumpa huo ushauri? Kama alishawahii kukaa nae na kumshauri hivyo lakini Kagame akaukataa huo ushauri, basi ilikuwa sawa kwa JK kwenda kwenye uwanja wa kimataifa na kusema aliyoyasema? Lakini kama hawajawahi kukutana na kushauriana na Kagame juu ya hilo jambo, basi hapo huoni kama kulikuwa na uwezekano wa Kagame kuguna?

Vipi kama ilikuwa ni Kagame alihutumbia kwenye mikutano ya kimataifa kuwa Tanzania inabidi wasikilize watu wa Mtwara, ifannye uchunguzi wa kina kuhusiana na matukio ya kuuawa na kuteswa kwa watu hapa nchini bila kwanza kuonge na JK, unadhani response ya JK ingekuwaje?

Wakati akina Nyerere na Mandela wakisuluhisha huko, walikuwa wanafanyaje? Walikuwa wanakaa na pande zote mbili na kujadiliana nao au walikuwa wanaenda kwenye majukwaa ya kimataifa na kusema wanalodhani kuwa ni sahihi bila kuwahusisha kwanza pande husika?


To the contrary, michango ya wachangiaji wengi hapa JF wanaonyesha kutaka vita. Pitia kwenye threads zinazojadili suala hili na soma michango ya watu and you won't be surprised. Ndiyo maana nilisema mwanzo hili suala linajadiliwa too emotionally na subjectively bila hata kufikiria implications za kuingia kwenye migogoro kama hii.

yaani Paul Kagame leo anatuita Watanzania 'genociders"....eti kwa kuwa tumemwambia a-reconcile!!??

Kama wewe Mtanzania siyo "genocider" na unajulikana ni mtu wa amani na huna ugomvi na mtu kwa nini kinakuuma kama ukiitwa genocider? Yaani kwa sababu amekuita genocider basi unataka kumpiga ili kumwonyesha kuwa wewe siyo genocider? Mie mtu akiiniita mshamba wakati najijua siyo mshamba wala sitapoteza muda nae. I have got a lot of things to do in my own home.​


......ni wakati umefika sasa PK aache arrogance/revenge attacks (amabzo zinaumiza na hata wasiokuwemo).....na utawala wa kibaguzi unaoendeleza chuki miongoni mwa wananchi wake.....na a-reconcile.......

That is none of our business. In fact, na sisi tuna matatizo kedekede ya ku-address. Tuna udini unaozidi kukua kila siku. Tuna ndugu zetu wameuawa na wengine kuteswa katika mazingira ya ajabu. Tuna matatizo mengine ya kushamiri kwa madawa ya kulevya. Hali ya maisha inazidi kuzorota, juzi tuu tumeletewa picha za kutisha kuhusu hali ilivyo Muhimbili. Mwaka huu tumekuwa na matokeo mabaya sana ya elimu. Kodi za mawasiliano zimepanda maradufu. Mtwara bado hali haijatulia. Tushughulikie kwanza haya, then tukiwa na muda wa ziasa tunaweza kusadia wengine.

Yes, wale jamaa (genociders) walikimbilia DRC......na yeye PK aliivamia DRC mwaka 1996 ili kuwasaka na kuwaua genociders.......doing the same shit, (i.e. including DRC people who suffered)......killing thousands of civilians

Wakati anawaua mwaka huo wa 1996, Tanzania ilifanya nini? Sina tatizo na Tanzania kusaidia katika vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchi nyingine, but we must do so in a responsible way kwa kuhakikisha kuwa hatuwaweki wanajeshi wetu katika mazingira ya hatari. In fact, ni moja ya majukumu yetu kulinda na kutetea regional and international peace and security. We signed the UN Charter to maintain peace and security.

Please I am not here to defend Kagame and I don't think why I should even try to defend him. Hata hivyo, this does not give me a reason to support the other side. Unless kuna information au mambo ambayo yamefanyika na siyajui bado naamini kuwa JK should have addressed the matter much better than he did.

Kagame na Museveni ni vijana/wanafunzi wetu....kama PK anafikiri arrogance yake ataileta Tanzania anajidanganya

Hizi ndizo arguments ambazo hazina substance yoyote. Hivi angekuwa ni Mkapa, Mganda nae angekuwa sahihi kusema kuwa Mkapa ni kijana/mwanafunzi wetu kwa hiyo kama anafikiri arrogance yake ataileta Uganda anajidanganya? Ukiwa kama Mtanzania ungekubaliana na hoja kama hiyo?

.....waite Watanzania kitu kingine lakini sio unafiki........Watanzania si wanafiki.....

Narudia tena Watanzania wengi ni wanafiki. Hilo liko wazi na wala usitake kujidanganya. Hata watawala wetu wanalijua hili na ndiyo maana Pinda alisema kuwa wanaopinga kodi za simkadi ni wanafiki. Watanzania wengi ni wanafiki, kwa mfano, wanasema kila mara kuwa wanachukia ushoga na hawatakubali ushoga kuhalalishwa lakini, ukipita kitaa mashoga wako kila kona. Kama huo sio unafiki ni nini?

Watanzania wengi ni wanafiki, wanapenda kujadili hoja nyepesi nyepesi (angalia hata threads zinazochangiwa zaidi kule jukwaa la siasa), wengi ni wavivu wa kufikiri pia.Kazi yetu wengi ni kupiga domo sana huku wachache wakila nchi. Rasilimali za nchi wanafaidi watu wachache. Juzi hapa walipogoma madaktari na walimu wengi wetu tuliwatupia madongo, lakini ndiyo tunaongoza kwa kulalamika kuwa elimu imeshuka, Muhimumbi watu wanakufa kama kuku, etc. Unafiki mtupu.

Nchi ina hali mbaya, ardhi inaporwa, madini yanamalizwa, wanyama nao wanahamishwa tena kwa ndege, wengine wanauawa na kuchomolewa meno yao, mfumuko wa bei ndiyo usisime, biashara ya madawa ya kulevya ndiyo hivyo tena, kila kitu kimekaa tenge, lakini sie ndo kwaaaaanza tuko na bize na Kagame. What is so special with Kagame?
 
Mkuu you need to know that JK si mfalme.

Neither did I say ni mfalme. Hata kama angekuwa mfalme kwani mfalme hafanyi makosa?

Ukiangalia kipindi chake cha kwanza cha utawala mambo yalikuwa ovyo sana, lakini term ya pili baada ya wakubwa wengine kumwambia anapeleka nchi kubaya, na kumuelekeza namna ya kuiendesha mambo yanabadilika.

Really? Kwa hiyo mambo ni much better kulinganisha na kipindi chake cha kwanza?

Labda ndo maana mpaka polisi wameambiwa watupige tuu maana serikali ya JK imetuchoka sasa.

Halafu kama Rais wa nchi anaelekezwa na wakubwa wengine kuendesha nchi then we must be in trouble.

Kama JK would have been bad as some people wants us to believe, he would not be presiding the country today, angekuwa amebadilishwa. He has his weaknesses, but that does not make him weak in all fronts.

Huu ni utani au niseme unafiki mwingine tena wa waziwazi.

Mtanzania gani wa nchi hii has the gut to overthrow the President?

Kwa sasa hata tukiwa na rais mbaya kiasi gani, mambo ya Tunisia na Misri mtayasikia kwenye bomba tuu.

Bado hatuna huo ubavu huo. Tutaishia kulalama as usual na kumwachia kila kitu Mungu.
 


....hahahah.......Mkuu nasisitiza, ukiliangalia hili suala kwa jicho la Chadema Vs CCM, au CCM Vs CUF......utakuwa huelewi hili suala zima........

Bila ya watu kupata Elimu ya maendeleo na ya kutambua haki zao na pia kuwa na uhuru wa kupata habari na elimu ya Uraia.....mapambano ya kuikomboa nchi yetu kutokana na ufisadi na ushenzi unaoendelea hayatafanikiwa..........tuna miaka takriban 21 tangia tuingie kwenye mfumo wa demokrasia ya vyama vingi........sisi bado ni wachanga kwenye huu mfumo........ tofauti na nyakati zile cha mfumo wa chama kimoja sasa hivi kuna asasi za kiharakati (vikundi....hapa sina maana ya Red/Green Brigade) zisizo za kiserikali....zipo katika kuelimisha jamii juu ya haki zao.....hivyo taratibu demokrasia yetu inakuwa.....kwani watu hivi sasa wanatambua na wanauliza.......

.......certainly baadhi ya watendaji serikalini bado wanafikir wapo kwenye ule mfumo wa zamani ndio maana unaona wanashindwa kutofautisha wajibu wao kwa wananchi waliowaajiri......mapamabano yanaendelea kwani kuna mambo kadhaa kwenye Katiba yanahitaji mageuzi/marekebisho makubwa..........so hivi vitu inabidi viende pamoja i.e. ukuaji wa demokrasia yetu na marekebisho ya Katiba.........

...vitendo vya kikatili vilivyo fanywa na vinavyoendelea kufanywa na dola yetu havikubaliki hata kidogo.....

......kuumia au kutokuumia kwa JUST kuitwa genocider its not a point.....the point is DHANA NZIMA inayobebwa behind......na vitendo vinavyoendelea.......na yes ni mwanafunzi wetu meaning we know a lot of him....na siyo ile tafsiri rahisi ya Mkapa kusoma Makerere......hivyo asijidanganye

.......Mkuu hakuna mahala binafsi nimepigia chapuo vita........na wala hiyo si nia ya Tanzania...Watanzania tutaji-defend kulinda Taifa letu na mipaka yetu pale tutakapochokozwa.......

.....Mkuu unataka uambiwe kuwa siku fulani saa fulani PK alishauriwa na JK akae na mahasimu wake......au unafikiri kila ziara za Marais zinatangazwa.......hivyo vitu mbona vinafanyika kirahisi sana....ila si lazima vyombo vya habari vifahamu kuwa Rais alikuwa na mazungumzo na Rais wa nchi fulani kwa masaa kadhaa.......ilifanyika hivyo kwa nchi nyingine barani Afrika......mfano.....kule Sudan, Kenya, DRC, Zimbabwe, Namibia nk na kwenye jukwaa la mikutano ya Kimataifa viongozi wao wakaambiwa/wakapewa ushauri na ukweli kwa uwazi.........unless kama hujui hivi vitu vinafanyika........JK kwenye hili hakukurupuka..........

Binafsi sifurahishwi na mambo mengi yanayotokea nchini na lawama nampatia JK....lakini kwenye hili suala la maziwa makuu......Kudos! to JK........
 

You must be joking!

Elimu ipi hiyo unayoiongelea hapa, shule za kata?
Kuna kipindi katika historia ya nchi yetu tumeshuhudia kuporomoka kwa kiwango cha elimu kama wakati huu( utawala wa JK)? Facts zipo wazi na mnazijua

Hakuna ukuaji wa demokrasia katika jamii ya watu wajinga popote pale chini ya jua, ukuaji wa demokrasia unaendana sambamba na ukuaji wa elimu ila hapa kwetu ni vice versa, (kwa mujibu wa maelezo yako at least)

Unajichanganya mwenyewe, mara demokrasia inakua mara ooh "vitendo vya kikatili vilivyo fanywa na vinavyoendelea kufanywa na dola yetu havikubaliki hata kidogo"

JK kafanya nini hasa kwenye huu mgogoro wa maziwa makuu mpaka apewe 'kudos'?

Au unadhani watu hawajui kuwa silaha zinazotumika katika mgogoro huu, asilimia kubwa tu zinapitia Tanzania hasahasa Mwanza?
Unakumbuka documentary ya mapanki na makala nyingine nyingi tu za watu wa UN na Human Rights zimeshapigia kelele kuhusu hilo, JK amechukua hatua gani?

Akose busara ndogo tu ya kuongea vizuri na watanzania wa Mtwara badala yake 'anawang'oa pembe', atayaweza wapi mambo yaliyowashinda kina Mandela na Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…