Kwanini JK (Kanali nusu mstaafu) hana ushawishi kwa Kagame (Jenerali Mstaafu)

Kwanini JK (Kanali nusu mstaafu) hana ushawishi kwa Kagame (Jenerali Mstaafu)

alisema alitoa ushauri kwa nia njema kabisa......na nia ile iko pale pale...angeibadili hapo ndio ungesema "U-Turn".......na hajawahi kuwa na U-turn kwenye hili suala......kwani hata kabla ya ule mkutano JK alishawasiliana na PK kuhusu ushauri huo.....pale Addis haikuwa mara ya kwanza PK kumsikia JK.....kwa ni suala walishaliongelea baina yao.........notwithstanding, JK alishtushwa na kejeli na matusi yanayoelekezwa kwake yeye na nchi yetu kwa ujumla tena kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu ikiwemo yeye mwenyewe PK........

Well, kama ulisoma post yangu ya mwanzo kabisa niliandika kuwa JK hakutoa ushauri mbaya. Tatizo lilikuwa kuwa kabla ya kuyasema aliyosema, alishawahi kukaa informally au hata formally na Kagame na kumpa huo ushauri?

Niliandika kuwa kama alishawahii kukaa nae na kumshauri hivyo lakini Kagame akaukataa huo ushauri, then it was fine for the President kwenda kwenye terraces za kimataifa na kusema aliyoyasema. Lakini sina uhakika kama walishawahi kukutana before that.

Wewe unadai kuwa alishawahi kuwasiliana na Kagame kuhusu ushauri huo kabla ya kushauri pale Addid Ababa. Kwamba kabla ya kusema aliyoyasema, JK alikuwa tayari ameshaongea na Kagame. If so, lini wapi, and what was the outcome? Hizo habari za JK kukutana na kumshauri Kagame kabla ya pale Addis Ababa umezipata wapi?

........ni ukweli usiopingika we need Rwandans and they need us.......kwa akili ya kawaida unafikiri ni rahisi hawa watu wawili kukutana.......isipokuwa ni busara tu ndio itakayowezesha hawa watu wawili wakutane kupitia now Mwenyekiti wa EAC.......sioni ubaya wa kuomba kupatanishwa....ili tuheshimiane.......

Well, Rais Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani. Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala, Uganda. Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Sasa wale wanaganga vita itakuwa imekula kwao. Na wale waliokuwa wanaandika hapa jamnvini kwa kufuata mkumbo watakuwa wamejifunza kitu.

Photos: President Kagame and President Kikwete hold talks on the sidelines of the ICGLR Summit- Kampala, 5 September 2013.

9676683911_4bb4b2c005_z.jpg


9679917620_3f83a214d0_z.jpg


9676681299_b3707d20a5_z.jpg


9677639469_ab87d0f36c_z.jpg
 
Mkuu EMT mazungumzo both kwa njia ya simu na kutembeleana kwa hawa viongozi Mrais tena hawa wa East, Central and Southern Africa yanafanyika sana.....tena wakati mwingine ziara zao hazitangazwi.......just FYI
 
Last edited by a moderator:
Hawa marais Bwana, angalia wanavyocheka, na huenda walikunywa chai na kutaniana.
 
Mkuu EMT mazungumzo both kwa njia ya simu na kutembeleana kwa hawa viongozi Mrais tena hawa wa East, Central and Southern Africa yanafanyika sana.....tena wakati mwingine ziara zao hazitangazwi.......just FYI

Hayo mazungumzo yalikuwa ya siri?
 
Back
Top Bottom