Kwanini Job Ndugai Wanalazimisha tumuite Hayati lakini Augustino Ramadhani wanataka tumuite Marehemu?

Tulipokosea pakubwa kama taifa ni pale tulipoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma
 
Hayati figganigga
 
Unafuatilia mambo ya hovyo tu we bwege. Filikunjombe bwana mdogo mbunge ameifanyia nini nchi zaidi ya ubunge wa Ludewa. Hilo la Augustinho Ramadhani kwanza unabwabwaja tu huna ht uhakika au umezusha tu km kawaida yako. Ni kawaida akili ndogo kufuatilia petty issues
 
Kaka kudos kwako kwa kutambua mchango wa the late Augustino Ramadhani. A man of integrity.
1. Military – Brigadier General in the TPDF.
2. Judiciary – Chief Justice of Tanzania.
3. Church – Bishop of Zanzibar in the Anglican Church.

Alikua amenyooka sana ase.
 
Wanajipendekeza kwake ili siku wakienda akawapokee wakidhani nako atakuwa supika
 
Na hoja yako ni ipi? Au matusi ndiyo lugha yako tu%?
 
Basi Mimi kwa Heshima Nimekumbuka Hayati Bibi yangu!
 
Basi ****** ni marehemu tu
 
Sikuwa najua kuwa hayati ina hadhi kuliko marehemu.
Kwa hiyo tuanze kusema “ Marehemu Hayati…” Kwa pamoja au “ Hayati Marehemu”…
Watu wa KHL na BAKITA njooni mtoe muongozo… hivi ni nini cha heshima zaidi mtu kuitwa Marehemu au Hayati ? Faida na Hasara zake ni zipi mtu akiitwa hivyo ilihali yupo anaoza huko kaburini?
 
Ni kama job amebebwa sana as there's something hiding.
But uitwe jina lolote haitabadili kuwa you are no more.
 
Angenyooka asingekataa mgombea binafsi kwenye full bench acha ujinga.

Mbaya zaidi bila aibu akaja kuchukuwa fomu kugombea Urais kupitia Ccm, hii nini maana yake?
 
Kwani hayati na marehemu wana tofauti gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…