Kwanini Job Ndugai Wanalazimisha tumuite Hayati lakini Augustino Ramadhani wanataka tumuite Marehemu?

AI generated. Wote wameshakufa hata ukimwita hayati au marehemu hawatarudi tena duniani.
 
JPM tulimwita mwendazake, wakabisha weee lakini ikawa imetoka hiyo.

Huyu ni marehemu.
 
Sikuwa najua kuwa hayati ina hadhi kuliko marehemu.
Wewe ni wa wapi ambaye hujui utofauti kati ya hayati na marehemu? Siku hizi hamfundishwi Kiswahili? Kapuku kama wewe ukifariki ni marehemu lakini kwa mtu aliyekuwa na mchango mkubwa hapa duniani ni hayati. Ndugai hana sifa ya kuitwa hayati, huyo ni marehemu tu!
 
Achaneni AI inawaharibu! Ona sasa hata hiki tulichofundishwa darasa la "4 B" tayari umekimbilia AI!
 
Ndigai ni marehemu.

Anakumbukwa kwa mabaya yake kuliko mazuri yule ( wale covid 19 walilipwa kwa pesa zetu) alimualika Cecil mwambe bungeni akiwa amefukuzwa na chama chake.

Wakati siyo MILELE
Marehemu ni mtu anayerehemewa na Mungu,hayati ni mtu aliye hai,kama unamchukia ndugai, tafuta jina jingine la kumuita na si marehemu
 
Achaneni AI inawaharibu! Ona sasa hata hiki tulichofundishwa darasa la "4 B" tayari umekimbilia AI!
Marehemu (al marhuum) ni mtu anayerehemewa na Mungu,hayati(al hayyat) aliye hai,hili ni jina mojawapo la Allah, kwamba yu hai milele
 
Chadema bhana πŸ˜‚ bila kupingapinga hamuoni amani
Watu wajinga tu ndio hufuata chochote wanachoambiwa ili isionekane wanapingapinga. Hivyo ujue si kila mtu ni mjinga kama ww.
 
Mkuu huwezi pingana na technology, lasivyo na wewe uache kutumia simu kuwasalimia baba na mama ,uwe unafunga safari ya kwenda huko,na tena usitumie gari uende Kwa mguu
πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏπŸ™ŒπŸΏ
 
hakuna shida, shida ni kuwa AI haiwezi kukufanya ukatumia commonsense
Sio ukweli mkuu,kama ndivyo hata wewe sayansi na technology imekufanya uwe mzembe,siku hizi unatumia madawa ya viwandani kujitibu badala ya Kutumia mitishamba,unatumia simu kusalimiana na ndugu zako walio mbali badala ya kwenda kuwasalimia ana kwa ana,unatumia usafiri wa gari na ndege pia treni kitu ambacho kimekufanya uwe mzembe kwani ulipaswa kwenda kwa miguu.

Huwezi shindana na technolijia hata kidogo
 
mimi sijasema kuwezi kutumia technology ya sasa, nimesema haiwezi kukufanya ukatumia commonsense - fahamu hivyo.

Maana yake ni kwamba AI itakupa majibu lakini wewe ndiyo utumie akili ya vippi yale majibu yanaweza kukufaidisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…