Kwanini jua, Mwezi, Nyota, vinaelea angani?

Kwanini jua, Mwezi, Nyota, vinaelea angani?

Mkuu aretasludovickHilo jina lina wafaa sana.
Maana Mpumbavu ni Mtu anayejifanya Mjuaji kumbe Hajui chochote.
Ukiwambia ulimwengu Haukuumbwa wataanza kuuliza Maswali yasiyo na Mantiki yoyote.

Lakini ukiwauliza wao,Huyo Mungu aliumbwa na nani?watakwambia Hakuumbwa.

Sasa kama unaamini kuwa kitu kinaweza kuwepo Bila kuumbwa,kwanini unapinga sayansi inaposema kuwa Ulimwengu Haukuumbwa?
All theists suffer From Special pleading.Lol

Sikiliza watakavyotokwa na povu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,swali Gani unataka Ujibiwe?
Uliuliza kuhusu Chanzo cha Big-Bang nikakijibu Hakuna.
Ukauliza tena,umejuaje kuwa Hakukuwa na Kitu kabla ya BB?.Hili ni swali la kipuuzi.

Hakuna kitu kinachoweza kuexist Nje ya Space and time
Na Space&time vyote vilikuwa Ndani ya Singurality/BB point.so Hakukuwa na kitu nje.
Aisee,labda nukushauri jambo huenda nikakusaidia maana kureason tu umeshindwa...

Nakushauri tu mkuu endelea kujifunza sana kuhusu maisha haya na kila kilichomo humu kwa kutafuta vyanzo vingi kadiri uwezavyo huenda ukapata mwanga maana hii ni hatari sana...

Kama ulikuwa unajaribu kupinga ili uelewe basi nasikitika kusema kuwa hata namna ya kupinga umekwama maana kuna mambo mengi sana hujayajua bado na unapaswa kuyajua uyafanye kama msingi ii ukijibiwa uweze kuelewa...

Kila la kheri....
 
Na nitaendelea kukuita Mpumbavu Unless uje upande Wangu.
Leo unatuuliza Mungu ni kitu gani?kwahiyo ulikuwa Unaamini kitu Usichokijua?

You're Moron For really.

Teh teh teh.
Kuja upande wako, haimaanishi upande wako umekuwa sahihi,

Elewa mantiki ya swali,

Nikikuuliza Mungu ni kitu gani wewe.na kwa kutumia sayansi ukashindwa kumuelezea.maana yake si kwamba haexist ila umeshindwa kumuelezea kwa kutumia sayansi.

Ni sahihi sasa na mimi kukuita mpumbavu maana umeshindwa???
 
Hapo ndo ujue kwamba hata baadhi ya mengine ambayo tunadhani tunayajua leo baadaye tunaweza kuja kugundua kuwa yalikuwa si ya kweli.
Ni sahihi, ndiyo maana mtu yeyote mwenye afya bora ya akili yuko tayari kukubali kosa pale inapogundulika na ushahidi wa kuridhisha kwamba kile alichokuwa akikifahamu ni tofauti na ukweli halisi. Nakumbuka zamani ilifundishwa kuwa ulimi una sehem mbalimbali kwa ajili ya kuhisi ladha tofautitofauti, Popo haoni kwa macho. Hivi shulei tulifundishwa milango mingapi ya fahamu kweli?!! Kwa kadri teknolojia inavyokuwa binaadamu anagundua zaidi na zaidi na kujisahihisha na kuboresha kuelewa wake wa mwanzo.
 
Teh teh teh.
Kuja upande wako, haimaanishi upande wako umekuwa sahihi,

Elewa mantiki ya swali,

Nikikuuliza Mungu ni kitu gani wewe.na kwa kutumia sayansi ukashindwa kumuelezea.maana yake si kwamba haexist ila umeshindwa kumuelezea kwa kutumia sayansi.

Ni sahihi sasa na mimi kukuita mpumbavu maana umeshindwa???

mungu ni kitu chochote unachokiamini na kukiabudu kwa kuamini kina uwezo na mamlaka juu yako
 
mungu ni kitu chochote unachokiamini na kukiabudu kwa kuamini kina uwezo na mamlaka juu yako

Usiseme kitu chochote labda kama unamaanisha miungu,

Mungu hawezi kuwa kitu chochote, Mungu ni mmoja pekee ninayemuabudu na kumuamini kuwa ana mamlaka juu yangu.
 
Kila kitu ulichotaja hapo juu kinaelea angali sababu kila kitu kinamvuta mwenzake, chenye mass(kg) kubwa kinavuta zaidi chenye mass(kg) ndogo. Sasa utauliza kwa nini vinavutana lakini havigongani, sababu ni nyingi, sayari zote zinavutwa na jua, lakini zinazunguka jua kwa spidi kubwa kwa hiyo zinacounterbalance, mwezi unazunguka dunia kwa speed kubwa ambayo inatosha pia ku-counterbalance nguvu inayouvuta karibu.

Kama haija-make sense inakuaje kitu kikizunguka kwa kasi kinacounter balance em angalia hii picha hapa chini
attachment.php

Hilo gari likishuka kwa spidi kubwa, litaweza kuzunguka hiyo round kwa ndani bila kuanguka na likapitiliza hadi upande wa pili, lakini likishuka kwa spidi ndogo basi halitoweza kuzunguka litaanguka. Concept kama hiyo.

Kuhusu kuona nyota na mwezi wakati wa usiku peke yake ni kitu simple tu, dunia inajizungusha kwenye mhimili wake, upande ambao unakua hautazamani na jua moja kwa moja ndo inakua usiku, kwa kua mwanga wa jua haufiki basi nyota na mwezi utaviona. Hata mchana hua nyota zinatoa mwanga lakini huzioni mchana sababu mwanga wa jua ni mkali kuliko unaotoka kwenye nyota.. Chukua tochi mchana, mwambia mtu asimame 50M kutoka kwako, ile tochi mwanga wake hutouona sababu mwanga wa jua umezidi, ila usiku utauona.. Hili jambo hata mtoto mdogo anaweza kukuelezea.

Nimeipenda umeiweka vizuri mtu kukuelewa,ingawa si kweli kwamba swali hili hata mtoto angeweza kulijibu,wewe umeona ni swali rahisi kwasababu umesoma vizuri hayo mambo na ukumbuke kuwa si watu wote wamesomea elimu hii.
 
Wakuu kuna mada fupi hapa,

Eti kwanini Jua, Mwezi, Nyota na Sayari zinaelea angani? Kwanini hazianguki chini? Pia kwanini nyota na mwezi huonekana wakati wa usiku tu?

Mkuu kama unapenda kujua kuhusu anga kwa ujumla nakushauri cheki discovery wana vipindi vizuri kama how the universe works,
 
Usiseme kitu chochote labda kama unamaanisha miungu,

Mungu hawezi kuwa kitu chochote, Mungu ni mmoja pekee ninayemuabudu na kumuamini kuwa ana mamlaka juu yangu.

mkorinto hivi unaijua tofauti ya umoja na uwingi?
 
Last edited by a moderator:
Nimeipenda umeiweka vizuri mtu kukuelewa,ingawa si kweli kwamba swali hili hata mtoto angeweza kulijibu,wewe umeona ni swali rahisi kwasababu umesoma vizuri hayo mambo na ukumbuke kuwa si watu wote wamesomea elimu hii.

Mkuu sisemei swali la kwanza, naongelea swali kwa nini mchana nyota na mwezi hazionekani, hiyo ni very easy logic
 
Back
Top Bottom