Kwanini kabila la Watusi halipo miongoni ya makabila yanayopatikana nchini wakati limekuwepo kwa muda mrefu?

Kwanini kabila la Watusi halipo miongoni ya makabila yanayopatikana nchini wakati limekuwepo kwa muda mrefu?

Tanganyika na hatimaye Tanzania hatujawahi kuwa na hilo kabila kama sehemu ya jamii yetu,hao unaowasema ni wahamiaji walikuja huku baada ya mauwaji ya kimbari ya kwanza kutokea dhidi ya watusi (1959-1962) ambapo takribani watusi 10,000 waliuwawa na wengi wao kukimbilia uhamishoni na wengine kuwa wakimbizi kwenye nchi za afrika mashariki ikiwamo Tanzania,kenya na uganda,
Then mauwaji ya kimbari ya pili yale ya mwaka 1994 ambayo takribani watusi laki 8 waliuwawa yalisababisha wimbi kubwa sana la wakimbizi wa kitusi kuja nchini mwetu ndio hao tunao mpaka leo,sio asili yao Tanzania na hawana asili ya kibantu,Asili yao wanatoka kwenye eneo la pembe ya africa (somalia,eritrea na ethiophia) hata ukiwaangalia wanashabihiana na watu wa hayo maeneo kwa mila,sura na maumbile
Katika makabila 120 yanayopatikana Tanzania ni ya kibantu ni machache sana ambayo hayana asili ya kibantu kama wamasai,wabarabaic,waeraq,wasandawe,wahadzabe,wambulu nk
Wambulu wana tofauti gani na waeraq mzee baba/mama?

Mtoa mada...kwanini hatuna kabila la wazungu Tanzania ilihali tunaowazungu wanaoishi hapa?
 
Ukiwakuta ukawauliza wewe kabila gani watakuwaambia msukuma, mhaya, muha, au mtu wa kigoma...

Utawajua ukianza kupiga nao stori moja mbili tatu hawa hawaijui Tanzania kiundani. Nilikutana na mwana mmoja akaniambia kwao Bukoba ni mhaya ila kiuhalisia Utanzania ulikuwa haupo ndani yake...tabia zetu twazijua....hauwezi kuficha asili yako hata iweje. Basi baada ya muda anajisahau na kuitaja nchi yake.

Ila wamepitia mengi nchi zao zimepitia hali ngumu saana.
 
Mtoa mada kuna makundi kadhaa ya hawa unaowaita watutsi Tanzania ila kwa sababu ya muonekano wao ni rahisi kuwachanganya wote kwa pamoja.
1.Kuna wakimbizi wa kitutsi walioloea Tanzania baada ya vita vya 1994 na migogoro ya miaka ya kabla ya hapo.Hawa wana hata ndugu huko Rwanda na hawa wanazungumza Kinyarwanda kama lugha yao na wapo sana Ngara,Karagwe,Kigoma,Katavi na Tabora.
2.Kuna watu wanaitwa Wahima.Wanashahibiana ki mwonekano na Watutsi wa Rwanda hawa hapa Tanganyika wameingia kabla ya uhuru wakiwa kama wafugaji na watawala ukienda kwa upande wa Uganda wanaitwa Bahororo sasa hawa wapo hasa kanda ya ziwa walichanganyikana na jamii za huko kiasi cha kuwa adopted ki lugha ukienda Geita na Sengerema wanajiita Wazinza au Walongo au ukienda Karagwe watajiita Wanyambo na hawana lugha yoyote wanayoijua tofauti na hizo.
Sasa shida ni moja tu katika hizi jamii.Zimetengenezwa nadharia za ufahari wa kimaumbile na kijamii zinazowafanya kujiregard kama viumbe wa kipekee na mara nyingi zinazungumziwa na watu wasiokuwa wa jamii hizi.Kwa mazingira haya inakuwa ngumu kutambulika kama kabila rasmi sababu kabila haliwi kwa sababu za kimaumbile bali lugha.
 
Watutsi inasemekana siyo kabila, ila ni jamii ya watu walipofika kusini mwa Afrika. Walijizolea umaarufu wa kuwa watu wema, wakaaminiwa, wakashiriki utawala na wakawa watawala.

Neno Mtutsi, wanasema linamaanisha mtu mwema. Siyo kabila. Wana kabila zao lakini walizipoteza, ndiyo maana hakuna lugha ya Kitutsi ila kuna watu wamepewa icon ya Ututsi.

Wakiwa na kabila fulani, huchukua mila hizo na hujiita wa kabila hilo. Wakiwa Kigoma ni Waha tu. Wakiwa Buhaya ni Wahaya, Uganda ni Wanankole, Usukumani watajiita Wasukuma.
Naona umekuja kutetea hahahaha jina lako linaonesha wewe ni wa Nyarubanda, Kigoma
 
Mleta mada ni ngumu kupata jibu humu jukwaani kwakua watu wanajibishana bila kwenda kwenye hoja ya msingi , kifupi sasa Tz tuna makabila 123 + ( ongeza wahutu na watusi) na syo tena 120
Saurce: hotuba ya Rais Magufuli huko Ngara akiwa na mgeni wake Rais wa Burundi

Nenda youtube kwa ukumbusho zaidi
 
Watusi asili yao Rwanda huenda waliopo huku ni wale wakimbiz kwahyo hawana makazi maalumu yaan chimbuko lao kwa tz kama tunavosema wachaga kwao moshi
 
Wanabaki na kabila zao Kama ni wahutu wanabakia wahutu na Kama ni watusi wanabakia na utusi wao wakiulizwa wewe kabila gani anasema mimi mhutu au mtusi hawahitaji kujificha
Hakuna kabila la Watusi wala wahutu, Bali kuna Wanyarwanda na Warundi basi.
Hakuna kabila lisilokuwa na lugha yao, hao wote wanaongea lugha moja tu.
 
Watusi ni moja kabila moja kubwa hapa nchini kwetu ambalo linapatikana haswa baadhi ya maeneo hapa nchini kama vile Tabora, Mpanda, Kigoma, Geita, Kagera, Karagwe, Bukoba na Kahama.

Ukifika maeneo ya Utusini katika hii mikoa, tamaduni nyingi za Kitusi zinafahamika kuanzia uvaaji, ufugaji na watu wanaofahamika. Lakini, je ni kwanini kabila hili halimo miongoni mwa makabila 120 yanayopatikana hapa nchini? Ukiangalia hili kabila ni la muda mrefu sana tangu karne ya 21 na pia kuna watemi wengi wa Kitusi .

Lakini twende mbele turudi nyuma, ni kwanini Watusi siyo miongoni mwa makabila yanayopatikana hapa nchini?

Wataalam wa historia nisaidieni.
Kuna hotuba moja ya Nyerere kuhusu Rwanda alisema Watutsi si kabila.

Alitaja vigezo vya kabila kuwa ni kuwa na nchi (ardhi ya kabila hilo) kuwa na lugha ya kabila na kuwa na uongozi kama chief wa kiasili wa kabila.

Alisema Watutsi na Wahutu ni watu wale wale tu, wamegawanywa na wakoloni.

Hakuna lugha ya Watutsi. Wanaongea Kinyarwanda sawa na Wahutu.

Hawana sehemu yao maalum. Wote wanakaa pamoja na Wahutu Rwanda.
 
Waswahili? Hawa wanapatikana wapi
Orodha ya makabila ya Tanzania
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Hii orodha ya makabila ya Tanzania inaweza kuwa na matatizo kwenye majina kadhaa, kwa sababu mbalimbali.
Orodha hii inatokana na orodha ya lugha za Tanzania inayopatikana katika Ethnologue, pamoja na tovuti nyingine.
Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja tu, badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya.
Juu ya hiyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vina mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani.
Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi tu, hasa kutokana na vita katika nchi za jirani. Vilevile ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Uarabuni au Uhindi.
Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
Waakiek
Waarusha
Waassa
Wabarabaig (pia wanaitwa Wamang'ati)
Wabembe
Wabena
Wabende
Wabondei
Wabungu (au Wawungu)
Waburunge
Wachagga
Wadatoga
Wadhaiso
Wadigo
Wadoe
Wafipa
Wagogo
Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
Wagweno
Waha
Wahadzabe (pia wanaitwa Wahadza na Watindiga)
Wahangaza
Wahaya
Wahehe
Waikizu
Waikoma
Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
Waisanzu
Wajiji
Wajita
Wakabwa
Wakaguru
Wakahe
Wakami
Wakara (pia wanaitwa Waregi)
Wakerewe
Wakimbu
Wakinga
Wakisankasa
Wakisi
Wakonongo
Wakuria
Wakutu
Wakw'adza
Wakwavi
Wakwaya
Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
Wakwifa
Walambya
Waluguru
Waluo
Wamaasai
Wamachinga
Wamagoma
Wamakonde
Wamakua (au Wamakhuwa)
Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
Wamalila
Wamambwe
Wamanda
Wamatengo
Wamatumbi
Wamaviha
Wambugwe
Wambunga
Wamosiro
Wampoto
Wamwanga
Wamwera
Wandali
Wandamba
Wandendeule
Wandengereko
Wandonde
Wangasa
Wangindo
Wangoni
Wangulu
Wangurimi (au Wangoreme)
Wanilamba (au Wanyiramba)
Wanindi
Wanyakyusa
Wanyambo
Wanyamwanga
Wanyamwezi
Wanyanyembe
Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
Wanyiha
Wapangwa
Wapare (pia wanaitwa Wasu)
Wapimbwe
Wapogolo
Warangi (au Walangi)
Warufiji
Warungi
Warungu (au Walungu)
Warungwa
Warwa
Wasafwa
Wasagara
Wasandawe
Wasangu (Tanzania)
Wasegeju
Washambaa
Washubi
Wasizaki
Wasuba
Wasukuma
Wasumbwa
Waswahili
Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
Watongwe
Watumbuka
Wavidunda
Wavinza
Wawanda
Wawanji
Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
Wayao
Wazanaki
Wazaramo
Wazigula
Wazinza
Wazyoba
 
Kuna hotuba moja ya Nyerere kuhusu Rwanda alisema Watutsi si kabila.

Alitaja vigezo vya kabila kuwa ni kuwa na nchi (ardhi ya kabila hilo) kuwa na lugha ya kabila na kuwa na uongozi kama chief wa kiasili wa kabila.

Alisema Watutsi na Wahutu ni watu wale wale tu, wamegawanywa na wakoloni.

Hakuna lugha ya Watutsi. Wanaongea Kinyarwanda sawa na Wahutu.

Hawana sehemu yao maalum. Wote wanakaa pamoja na Wahutu Rwanda.
Naaam julius alisema vizuri.

Btw na yeye ni wa huko huko.
 
Nijuavyo mimi ni makabila ‘zaidi’ ya 120, ila sio yote nayafahamu (sio mimi tu). Nitumie fursa hii kuomba mwenye LIST kamili ya MAKABILA yote ya TZ atuwekee hapa.
Haya hapa
Uhindi.
 
Mimi namuunga mkono. Hakuna kabila la watusi ila ni clan. Warwanda wataitwa watutsi, bukoba wahinda na wahima. Lugha walilirithi kadri walivyowanamigrate wakawa wana adopt mila za pale. Tofauti yao na makabila mengine,wenyewe walipigana wakatawala makabila ya kibantu. Wenyewe hata muonekano wao ni tofauti. Warefu, siyo wasemaji saana na ni watemi.
Hawa walifika sehemu nyingi, wakiwa Musoma wanaitwa wanaki, simiyu nyantuzu, bukoba hima, Uganda nyankole ngara wasubi. Hawa wakati mwingine hawana lugha kamili,
 
Mtusi.

Hata Mbowe. Linganisha hotuba na sura ya Mbowe na Mkuu wa kwanza wa nchi
ha ha ha
Nyerere hata Lowasa ni mtoto wa Nyerere angalia mvi kichwani kichwa Cha Lowasa na Nyerere na sura
 
Back
Top Bottom