Kwanini kabila la Watusi halipo miongoni ya makabila yanayopatikana nchini wakati limekuwepo kwa muda mrefu?

Wambulu wana tofauti gani na waeraq mzee baba/mama?

Mtoa mada...kwanini hatuna kabila la wazungu Tanzania ilihali tunaowazungu wanaoishi hapa?
 
Ukiwakuta ukawauliza wewe kabila gani watakuwaambia msukuma, mhaya, muha, au mtu wa kigoma...

Utawajua ukianza kupiga nao stori moja mbili tatu hawa hawaijui Tanzania kiundani. Nilikutana na mwana mmoja akaniambia kwao Bukoba ni mhaya ila kiuhalisia Utanzania ulikuwa haupo ndani yake...tabia zetu twazijua....hauwezi kuficha asili yako hata iweje. Basi baada ya muda anajisahau na kuitaja nchi yake.

Ila wamepitia mengi nchi zao zimepitia hali ngumu saana.
 
Mtoa mada kuna makundi kadhaa ya hawa unaowaita watutsi Tanzania ila kwa sababu ya muonekano wao ni rahisi kuwachanganya wote kwa pamoja.
1.Kuna wakimbizi wa kitutsi walioloea Tanzania baada ya vita vya 1994 na migogoro ya miaka ya kabla ya hapo.Hawa wana hata ndugu huko Rwanda na hawa wanazungumza Kinyarwanda kama lugha yao na wapo sana Ngara,Karagwe,Kigoma,Katavi na Tabora.
2.Kuna watu wanaitwa Wahima.Wanashahibiana ki mwonekano na Watutsi wa Rwanda hawa hapa Tanganyika wameingia kabla ya uhuru wakiwa kama wafugaji na watawala ukienda kwa upande wa Uganda wanaitwa Bahororo sasa hawa wapo hasa kanda ya ziwa walichanganyikana na jamii za huko kiasi cha kuwa adopted ki lugha ukienda Geita na Sengerema wanajiita Wazinza au Walongo au ukienda Karagwe watajiita Wanyambo na hawana lugha yoyote wanayoijua tofauti na hizo.
Sasa shida ni moja tu katika hizi jamii.Zimetengenezwa nadharia za ufahari wa kimaumbile na kijamii zinazowafanya kujiregard kama viumbe wa kipekee na mara nyingi zinazungumziwa na watu wasiokuwa wa jamii hizi.Kwa mazingira haya inakuwa ngumu kutambulika kama kabila rasmi sababu kabila haliwi kwa sababu za kimaumbile bali lugha.
 
Naona umekuja kutetea hahahaha jina lako linaonesha wewe ni wa Nyarubanda, Kigoma
 
Mleta mada ni ngumu kupata jibu humu jukwaani kwakua watu wanajibishana bila kwenda kwenye hoja ya msingi , kifupi sasa Tz tuna makabila 123 + ( ongeza wahutu na watusi) na syo tena 120
Saurce: hotuba ya Rais Magufuli huko Ngara akiwa na mgeni wake Rais wa Burundi

Nenda youtube kwa ukumbusho zaidi
 
Watusi asili yao Rwanda huenda waliopo huku ni wale wakimbiz kwahyo hawana makazi maalumu yaan chimbuko lao kwa tz kama tunavosema wachaga kwao moshi
 
Wanabaki na kabila zao Kama ni wahutu wanabakia wahutu na Kama ni watusi wanabakia na utusi wao wakiulizwa wewe kabila gani anasema mimi mhutu au mtusi hawahitaji kujificha
Hakuna kabila la Watusi wala wahutu, Bali kuna Wanyarwanda na Warundi basi.
Hakuna kabila lisilokuwa na lugha yao, hao wote wanaongea lugha moja tu.
 
Kuna hotuba moja ya Nyerere kuhusu Rwanda alisema Watutsi si kabila.

Alitaja vigezo vya kabila kuwa ni kuwa na nchi (ardhi ya kabila hilo) kuwa na lugha ya kabila na kuwa na uongozi kama chief wa kiasili wa kabila.

Alisema Watutsi na Wahutu ni watu wale wale tu, wamegawanywa na wakoloni.

Hakuna lugha ya Watutsi. Wanaongea Kinyarwanda sawa na Wahutu.

Hawana sehemu yao maalum. Wote wanakaa pamoja na Wahutu Rwanda.
 
Waswahili? Hawa wanapatikana wapi
 
Naaam julius alisema vizuri.

Btw na yeye ni wa huko huko.
 
Nijuavyo mimi ni makabila ‘zaidi’ ya 120, ila sio yote nayafahamu (sio mimi tu). Nitumie fursa hii kuomba mwenye LIST kamili ya MAKABILA yote ya TZ atuwekee hapa.
Haya hapa
Uhindi.
 
Hawa walifika sehemu nyingi, wakiwa Musoma wanaitwa wanaki, simiyu nyantuzu, bukoba hima, Uganda nyankole ngara wasubi. Hawa wakati mwingine hawana lugha kamili,
 
Mtusi.

Hata Mbowe. Linganisha hotuba na sura ya Mbowe na Mkuu wa kwanza wa nchi
ha ha ha
Nyerere hata Lowasa ni mtoto wa Nyerere angalia mvi kichwani kichwa Cha Lowasa na Nyerere na sura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…