Kwanini kada nyingine unadharau walimu je ni sababu ya mshahara mdogo au ni nini...??

Kwanini kada nyingine unadharau walimu je ni sababu ya mshahara mdogo au ni nini...??

System ya kuchukua hata watu waliofeli wakasome ualimu mwisho wa siku inaonekana ni profession ya watu wasiojiweza kielimu, watu wanachukulia tumefeli ndo maana ni walimu.
wengi ni magumashi tu elimu zao hazieleweki hata vyeti vya form four hawana ila ni walimu, siku msako ukipita ndo watajua kumbe walimu hakuna.
sijui kwa sababu ya kupata kazi kimagumashi ndo maana hata haki zetu hatuzijui, sijui ndo nidhamu ya ki ualimu mi sielewi,
tunafanyishwa vikazi hata bila malipo wakati inatakiwa tulipwe ukiuliza eti ni oder kutoka juu, juu mbinguni au?
mishahara midogo, mazingira ya kazi ovyo n.k n.k
idara ya elimu ubabaishaji mwingi tofauti na kada zingine ndo maana mambo ni ovyo
 
Walimu wenyewe siku hizi sisi tupo kidigitali tu
hata maadili ya kazi hatuna, tupo tu ili tupate mishahara
Aaaah hovyo tu
 
Kwa sababu walim MMEKUBALI kudharauliwa.Kuendelea kukubali kunyonywa na TSD,CWT,kukubali Mishahara duni na kutokua na bodi ya ualimu(sio walimu) ili kudhibiti ubora wa fani ya ualimu kama ilivyo kwa mainjinia na mmadaktari ni KUKUBALI KUDHARAULIWA.
 
Hivi nursing na uhasibu kwa level ya form four na ualimu wapi wanachukuliwa wenye marks chafu? Chunguza utaona kimbilio la walio feli ni uhasibu na nursing, walimu wanachukuliwa wenye 4 ya 26 na 28 wakati nursing hadi 30 ilimradi awe na D ya Bios, pia CBE pale Dodoma wanadahiliwa hadi wenye Zero za mwanzo yani 4 negative!
 
Hata wewe unaesema hvyo ulifundishwa na walimu hoa hao unaosema ni felia.Je kama wao wamefeli na hawajui walifanyalo wale wanaofaulu vipaji wanafundishwa na walimu gani? Acha dharau kufeli mtihani haimaanishi hauna akili.
 
tatzo ni mshahara tu kuwa mdogo.hv anaefaham aniambie ualim na nursing wap kuna afadhali,?? wengine tumependa kaz kutoka moyoni,kama matokeo yangu o-Level na a-level yanaridhisha kwann nijiundermine mwenyewe,Nimependa teaching toka moyoni
 
Kwani waalimu mnalipwa sh. Ngap? Ili tujue mshahara wenu kweli mdogo!!
 
mi naona kuwa msahara mdogo we angalia mwalimu mwenye shahada analipwa na anapitwa na daktari au injinia mwenye diploma!
 
Kwangu mimi mshahara wangu wa ualimu unanitosha,kwa sababu kwa mwezi nafundisha mara mbili tu!siku zingine nafanya inshu zangu tu na hakuna wa kuniuliza.Kuna watu wakiona wanajua ni Afisa TRA huo mkwanja wake.Tehtehtehteh siiachi hii kazi mpaka nakufa na mtachonga sana na ikibidi mprint na Tshirt mvae,kuwa waalimu tunalipwa mishahara midogo.Tunajua kuna wengine mna mishahara kama sisi ila kuna dili za wizi ndo zinawatoa sasa sisi mnataka tuibe chaki?.
 
Hivi nursing na uhasibu kwa level ya form four na ualimu wapi wanachukuliwa wenye marks chafu? Chunguza utaona kimbilio la walio feli ni uhasibu na nursing, walimu wanachukuliwa wenye 4 ya 26 na 28 wakati nursing hadi 30 ilimradi awe na D ya Bios, pia CBE pale Dodoma wanadahiliwa hadi wenye Zero za mwanzo yani 4 negative!

Waambie maana watu wanadhani kila aliyekuwa mwalimu bac alifeli, wengine tulikimbilia ualimu ili tupate ajira za harakaharaka then tutafute michongo mingine, kila mtu ana plan zake katika maisha, na kwa baadhi huo ualimu ni sehemu ya kupitia tu!
 
Tatizo kubwa la kudharaulika walimu wamekuwa ni waoga na wenye kugoma mabadiliko toka moyoni pia majungu ni mengi mno.
 
System ya kuchukua hata watu waliofeli wakasome ualimu mwisho wa siku inaonekana ni profession ya watu wasiojiweza kielimu, watu wanachukulia tumefeli ndo maana ni walimu.
wengi ni magumashi tu elimu zao hazieleweki hata vyeti vya form four hawana ila ni walimu, siku msako ukipita ndo watajua kumbe walimu hakuna.
sijui kwa sababu ya kupata kazi kimagumashi ndo maana hata haki zetu hatuzijui, sijui ndo nidhamu ya ki ualimu mi sielewi,
tunafanyishwa vikazi hata bila malipo wakati inatakiwa tulipwe ukiuliza eti ni oder kutoka juu, juu mbinguni au?
mishahara midogo, mazingira ya kazi ovyo n.k n.k
idara ya elimu ubabaishaji mwingi tofauti na kada zingine ndo maana mambo ni ovyo

Kasumba ya kwamba walim wamefeli haina mashiko,kuna kozi nying watu wanajoin na marks za chin sana,journalism,accounts,procurement na baadh ya kozi za afya,vyeti vya magumash vipo kila sehemu jeshin,polis had bungen mbona hao hawadharauliwi?nadhan tatzo ni walim kutojiamin,kujikubali na kuwa na msimamo wa kusimamia haki zao,ukijidharau kila mtu nae atakudharau
 
mi naona kuwa msahara mdogo we angalia mwalimu mwenye shahada analipwa na anapitwa na daktari au injinia mwenye diploma!

Una uhakika mkuu? Ebu toa figure hapa tulinganishe!! Unaongelea mshahara au posh?!
 
Back
Top Bottom