Kwanini Kagame anachukiwa sana humu JF?

Kwanini Kagame anachukiwa sana humu JF?

Mtu gani amegombana na majirani zake wote hebu nitajie nchi ambayo haijagombana na kagame, sasa hivi anagombana na Africa kusini
Lazima anagombana nao kwa sababu maalumu ,

Hata Israel inagombana na inchi zinazoizunguka , hiyo ni kawaida tu
 
Kiswahili tumejifunza ukubwani , tumekulia kijijini huko ambapo tulikuwa tunaongea kiluga Cya kabira letu , ukionekana unaongea kiswahili watu wanakuokopa Sana
Nenda kwenyu huko bwana katetee huu ujinga,hata hapa unachapia tena.nasema hivi!wewe ni mtutsi hujifichi
 
Nenda kwenyu huko bwana katetee huu ujinga,hata hapa unachapia tena.nasema hivi!wewe ni mtutsi hujifichi
Ningekuwa mtutsi ningefurahi Sana , maana ni kabira ninalolipenda Sana
 
*cya kabira*
huyu ni mnyarwanda pure halafu sijui kwa nini wanyarwanda kiswahili kinawashinda hata wakikaa Tanzania .Ni tofauti kabisa na warundi,mrundi akikaa kwenye miji ya tz hamalizi mwaka bila kujua kiswahili kizuri kama unabisha nenda pale buyenzi Bujumbura kasikilize warundi wanavyokinyoosha kiswahili cha pwani kabisa
 
Kuna ambae wanamchukia sema wanashindwa kumlenga yeye waliyenae karibu wanabaki kumsema Kagame aliye mbali na wanajua hata wakimsema vipi haitakaa itokee akaja kuwakamata!!
 
MAHORO, hili jina tu linatosha kutoa utambulisho wako Mkuu!! Kwahiyo sishangai haya uliyoandika hapa mkuu! Halafu ubora wa elimu haupimwi kwa kugawia watoto laptop mkuu, tafakari.
 
Nimepitia threads nyingi Sana na comments za watu zinazomhusu Paul kagàme, nimesikitika Sana kwa njisi ambavyo watu hawamupendi kagàme , ninaomba tufanye uchunguzi na comments bila chuki binafsi

Angalieni , katika inchi za Afrika au duniani kote , Ni raisi gani amefanikiwa katika kuiletea maendeleo inchi yake ?

Amewaunganisha wanyarwanda wote , makabira ya Rwanda yote ni wamoja na wanampenda Sana kagàme , hiii Ni kupitia kampeni yake iliyoitwa SOTE NI WANYARWANDA.. na Sasa umoja na mshikamano vinaonekana

Amaefanikisha kumaliza rushwa katika inchi yake , ambapo inchi nyingine zimeshindwa kabisa ..

Elimu Ni Bora kuliko inchi yoyote , mfano kila mtoto ana laptop yake , pia kuonesha ubora wake wa elimu , Tanzania imeazima wataalamu wa IT kutoka rwanda

Anatengeneza ndege zisizotumia rubani maalufu Kama DRONES , na ndizo zinatumika kusambaza madawa inchini

Amewagawia wanyarwanda Ngombe na kuwajengea nyumba nzuri

Ameitangaza rwanda kupitia timu ya kubwa ya England ya ARSENAL kupitia VISIT RWANDA, Leo kila mtu duniani anaulizia RWANDA , watalii wanaongezeka kila kukicha ((nitawaletea takwimu )

Kwakweli Mimi siyo mnyarwanda ila nimependa uongozi wa huyu mjeshi , Ni uongozi unaotakiwa kuigwa na watawala wengine , na tukipata kiongozi wa hivi hata akitawala milele ni sawa tu ..

Angalia Burundi , imepitia matatizo sawa na RWANDA , lakin kimaendeleo na usalama bado iko nyuma Sana , hii Ni kwasababu ya kiongozi mubovu

Nawaomba watanzania wenzangu , tuache chuki binafsi juu ya Paul Kagàme , acha achape kazi kwa ajili ya watu wake ,

Anawaoenda watu wake na watu wake wanampenda Sana , Ni wachahe Sana mainterahamwe ndio hawampendi ,

Kiongozi Bora hawezi kukaa kimya akiona watu wake wanauawa , Ni kiongozi mpumbavu Sana anayeweza kuona watu wake wananyanyaswa na akakaa kimya ..!!

KAGAME ni kiongozi wa watu , na ingewezekana tungefanya awe rais wa Afrika ,

Acheni chuki za kipuuzi
Umesahau hii hapa , AMEUWA NA KUFUNGA KILA MNYARWANDA ANAYEMPINGA .
 
Back
Top Bottom