Kwanini katiba za Afrika hatakama ni mpya ni ngumu kuwanyonga au kuwafunga mafisadi

Dennis Robert Shughuru

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2024
Posts
5,559
Reaction score
8,747
Nchi nyingi za Afrika zimekuja na katiba mpya ila imekua ni ngumu sana kwa hizo katiba kutamka waziwazi kuwashughulikia mafisadi ama kwa kuwafunga au kuwanyonga

Ni ngumu sana kwa nchi ya Afrika kusikia high profile politician ambaye ni fisadi kufungwa au kunyongwa kwanini inakua hivi

  1. Sababu kubwa kwanini inakua hivi cha kwanza jambo la kufahamu ni kwamba anayetengeneza katiba ni yule ambaye yupo madarakani sasa viongozi wengi walioko madarakani sio waadilifu sasa kama kiongozi sio mwadilifu unategemeaje atengeneze katiba ambayo itambana yeye jibu ni hapana hawezi
  2. Sababu ya pili ni viongoizi wengi wa afrika wameshashiriki ufisadi kwa njia moja au nyingine kwenye maisha yao ya siasa na uongozi kwa hiyo ni ngumu sana inapotokea wanapata nafasi ya kutengeneza katiba au kuweka amendment kuweka kipengele cha kuwabana mafisadi sababu hata wao walishafanya ufisadi kwa hiyo kuweka adhabu kali kwa mafisad ni kujiweka kwenye kitanzi
  3. Sababu nyingine ni waliowazunguka inawezekana kiongoizi akawa ana nia nzuri ila waliowazunguka wakawa wanafanya ufisadi wa kufa mtu na unakuta hawa waliowazunguka kwa njia moja au nyingine walimuweka madarakani kwa hiyo inapotokea nafasi ya kutengeneza katiba mpya au kufanya Marekebisho kamwe hawawezi kuweka adhabu kali kwa mafisadi inakua ni katiba mpya jina ila content ya zaman

Mfano kenya walitengeneza katiba mpya ila still ufisadi na ukabila bado upo sana sababu waliotengeneza katiba ya kenya ya mwaka 2010 ni walewale establishment politicians usitegemee waweke sheria ngumu za ufisadi kwa sababu wame-thrive kupitia ufisadi na wanatumia tribe card kushinda uchaguzi kamwe hawawezi weka vipengele vigumu kwenye katiba vitakavyowabana

Sasa ili nchi za afrika tupate katiba bora wanaotakiwa kutengeneza katiba hawatakiwi kuwa hawa waliopo madarakani sababu kamwe hawawezi kukuletea katiba nzuri sababu ikija katiba nzuri wao ndo watakuwa washtumiwa wa kwanza mtu kama Ibrahim traore ambaye hana mizizi serikalini ndo anatakiwa atengeneze katiba nzuri tena pale tu anapoingia madarakani kabla hata ya kuzoea madaraka lakin na yeye akishazoea madaraka ni ngumu sana kukupa katiba mpya nzuri
 
Ni sawa na kutegemea samia suluhu Hassan kukupa katiba bora sana sana watakuja na katiba mbovu sana zaidi ya hii
 
Hata ambao hawako madarakani hawawezi kuweka hivyo vipengere maana wanajua au wanatamani siku moja kuwa viongozi serikalini na wana tamaa ya kupora mali za umma. Kama alivyosema makonda unapiga kelele kwa sababu hauko jikoni. Hapa kwa kweli ni mtego sana katika uandikaji wa hizi katiba mpya. Au kuwe na sheria kwamba wale wote walioshirika katika tume au bunge la kuandika katika wasiruhusiwe kushika nafasi za kisiasi kwa miaka 50 zijazo au maisha yao yote.
 
Kama nchi nyingine waliweza kuwa na katiba ambazo zitashughulikia wabadhirifu hata sisi tunaweza ni basi kwenye siasa zetu kuna dhana ilikuwa siasa ni mchezo mchafu kwa hiyo wanaoshiriki siasa ni wale wanaoamini siasa ni mchezo mchafu

Sasa mtu anayeamini siasa ni mchezo mchafu anawezaje kukuletea katiba mpya nzuri hii ndo changamoto iliyopo huku afrika
 
Nchi nyingine za ulaya sio Afrika. Ila kipengele cha kuwazuia kugombea au kuteuliwa nafasi za kisiasa inaweza kusaidia
 
Back
Top Bottom