Kwanini Katibu Mkuu wa CCM amekosa kabisa ushawishi Kwa jamiii? Je, CCM wana mgomo baridi dhidi yake?

Wamebaki kujipaka mkorogo kama zumaridi
 
Hivi Katibu Mkuu wa CCM anaitwa nani ?
 
Mvuto ni mashindano ya urembo?Watu makini wanaangalia anasimamia vizuri sera ya Chama chake?Anatimiza wajibu wake?
Sisi tunaomfahamu hatuna shaka nae tunajua uwezo wake.
Wengi wamezoea mipasho.Kasikilize taarabu.
Ninakubaliana na wewe, lakini ana kazi ngumu sana inayomkabili mbele yake, na sijui kama atafanikiwa. Chama kimekwishagota sana. Atajitahidi sana kukinyoosha, lakini sidhani kuwa ataweza.

Mbaya zaidi, hata Mwenyekiti wake hana haiba ya kumsaidia kukirekebisha chama.

Chongolo anayo kazi ngumu sana inayomkabili wakati huu, na hapo itakaposhindikana ni yeye atakayepewa lawama zote.

Hiki ni kipindi kigumu sana kwa CCM, kufuatana na rekodi yake mbaya ya miaka mingi.

Hata ule upepo tu unaovuma katika maeneo yetu haya, ni sababu tosha ya kumpa kazi ngumu. Kuna baadhi ya watu sasa wanajiuliza kwa nini kila mara iwe CCM..., hii pekee ni sababu muhimu kwa baadhi ya watu, na upinzani wakijua jinsi ya kutumia sababu dhaifu kama hizo, zikichagizwa na ubovu wa CCM, ni sababu tosha kabisa ya kumnyima usingizi Chongolo.

Mimi namshauri kwa kuanzia, aache kufukuzana na CHADEMA. Kuna kazi tosha ndani ya chama chake. Aanzie huko.
 
Hakuna mwenye mvuto CCM. Huyo Katibu Mkuu ndiyo kabisaaa, afadhali wampe paka mic tutaingia kuangalia masharubu. Chama kimechokwa kama enzi zileee za Msoga!!!
 
Ccm inajua wapiga kura wako wapi! Kwa kukusaidia wapiga kura wa CCM wengi Wana vitochi na wengine hawana simu kabisa, ila ndo wapanga foleni wazuli kwenye uchaguzi, iwe jua iwe mvua!!
 
Masaa ya kuongea na vyombo vya habari nayo wayaangalie. Mida ya kutafuta shilingi unaitisha press
 
Mvuto ni mashindano ya urembo?Watu makini wanaangalia anasimamia vizuri sera ya Chama chake?Anatimiza wajibu wake?
Sisi tunaomfahamu hatuna shaka nae tunajua uwezo wake.
Wengi wamezoea mipasho.Kasikilize taarabu.
Dah....Bora uwachane tu....hawajui Ile miaka 6 tulivyoishi kwa tabu....wenyewe tulijizoelea Hakuna tofauti ya Mali za chama na mali zetu binafsi....chama Ni wanachama....na wanachama ndiyo sisi....Sasa Kuna ubaya gani wa Mimi kupewa fremu 1 pale Mkwajuni niichukue kodi nilale na wajukuu? Mbona Ulaya nasikia kuna watu wanalipwa bila kufanya kazi....iweje sisi watuite mafisadi?......hebu watuache tupumue.........
Ule msemo wa "charity begins at home" ni wa kipuuzi haufai kwenye maadili yetu....
Endelea kuwachana bro...maana hawajui hata maana ya nembo ya chama...mie namalizia keivanti......maana ukiwaendekeza hawa kesho watadai Maza Ni zaifu 🤭
 
Huyu hana tofauti na Mukama. Mara zote uzoefu unaonesha wenye asili ya Pwani wame-perform zaidi (kwa viwango vya CCM) kuliko waswaga ng'ombe.
Since mfumo wa vyama vingi umeanza, kuna katibu mkuu aliyemzidi Alhaji Kinana na mzee yule wa Njombe enzi ya Mkapa? Kinana ni Muarusha na yule mzee wa Njombe ni Mbena; hapo vipi mkuu? Labda kama huna historia ya hiko chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…