chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Mwenge ni protocal ya Rais, nilitarajia Mkuu wa Mkoa wa Arusha leo akabidhi mwenge kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Kulikoni Arusha!?
Hata mgomo wa wafanyabiashara Namanga, kwa nini Mkuu wa Mkoa wa Arusha hajaenda kuushughulikia?
=======
Mbio za Mwenge wa Uhuru leo July 26th, 2024 zimeingia katika Mkoa wa Mara na kupokelewa rasmi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bwana Musa Musaile Musa.
Akitoa taarifa kwa Kiongozi wa Kitaifa wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Godfrey Eliakimu Mzava, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amesema kuwa mwaka huu Mbio za Mwenge wa Uhuru zitapita katika miradi ya maendeleo 72 yenye thamani ya shilingi 24,961,723,115.48 `iliyotekelezwa kwa michango ya wananchi, Halmashauri, Serikali Kuu na wahisani.
“Miradi itakayotembelewa ipo katika sekta za elimu, kilimo, ujenzi, maji, afya, mifugo, mazingira, ustawi wa Jamii, viwanda na biashara na shughuli za vijana” amesema Mhe. Mtambi.
Mhe. Mtambi amesema ukiwa katika Mkoa wa Mara Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Wilaya sita na Halmashauri tisa katika umbali wa kilomita 1,037.80.
Kanali Mtambi amesema ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni kuhusu utunzaji wa mazingira na uchaguzi wa Serikali za Mitaa chini ya kauli mbiu: Tunza Mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu.
Akizungumzia ratiba ya Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kanali Mtambi amesema Mwenge unatarajiwa kukimbizwa kuanzia Serengeti tarehe 26/ 7/ 2024, Tarime DC tarehe 27/7/2024, Tarime TC tarehe 28/7/2024, Rorya 29/7/2024 na Manispaa ya Musoma tarehe 30/7/2024.
Mwenge utakimbizwa Musoma DC tarehe 31/7/2024, Butiama tarehe 1/8/2024, Bunda DC tarehe 2/8/2024, Bunda TC tarehe 3/8/2024 na tarehe 4/8/ 2024 Mwenge utakabidhiwa katika Mkoa wa Simiyu kuendelea na mbio zake.
Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara amewakaribisha viongozi, watendaji na wananchi wote kushiriki katika maadhimisho ya miaka 60 ya Mwenge wa Mwitongo yatakayofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwitongo tarehe 1 Agosti, 2024.
Mwenge wa Mwitongo ni mwenge wa Kabila la Wazanaki ambao upo Nyumbani kwa Baba wa Taifa na unawashwa kila mwaka Mbio za Mwenge wa Uhuru zikiwa katika Mkoa wa Mara tangu mbio hizo zilipoanzishwa mwaka 1964.
Mhe. Mtambi amesema mwaka huu ni mwaka maalum kwa Mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo unaadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, miaka 60 ya Muungano wa Tanzania na Miaka 60 ya Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Baada ya mapokezi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bibi Anjelina Marko.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambapo ukiwa huko utapita katika miradi tisa yenye thamani ya shilingi 6,274,190, 935.39
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bwana Musa Musaile Musa katika Kijiji cha Robanda Wilaya ya Serengeti na baadae kuukabidhi kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti Bibi Angelina Marko kuendelea na mbio zake.