KERO Kwanini katika mfumo wa Sekretarieti ya ajira ikitangazwa kazi ya astashahada mwenye shahada anaambiwa hana sifa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mendezi1512

New Member
Joined
Oct 3, 2026
Posts
1
Reaction score
1
Kuna changamoto katika mfumo wa ajira.

Baadhi ya watu wamesoma kozi tofauti katika ngazi ya cheti na diploma, lakini nafasi za kazi zinapotangazwa kulingana na kozi walizosoma katika ngazi ya cheti, mfumo unawakatalia kuomba kwa madai kuwa hawana sifa zinazohitajika.

Nashauri mfumo uruhusu mtu kuomba nafasi za kazi kulingana na elimu alizosomea katika ngazi za chini, bila kujali ana kiwango cha juu zaidi cha elimu katika kozi tofauti. Hata hivyo, hili lisihusishe wale wenye cheti na diploma katika kozi husika. Asante
 
Utakuwa unamuonea dogo wa cheti au diploma. Maana wewe unaexposure kumzidi. Lengo ni kushindanisha watu ambao wako level moja.

Ni sawa na kuweka mechi kati ya Real Madrid na Ihefu. Hakuna fairness hapo.
 
Sijui n roho mbaya ama tatizo ni nn kwa sisi Wabongo aisee 🙌

Unaona kabisa anahitajika mtu wa cheti, ila ww wa degree unaona wivu unataka mfumo uwekwe ili nawe upate hiyo nafasi.

Wabongo kmmae zetu 🙌
 
Labda ungesema Spain vs Ihefu ndo ungekuwa sahihi kwenye huu mfano wako

Madrid vs Ihefu ni ishu inayowezekana kwa 100%

Kama utakuwa unafatilia laliga Kuna timu iliwahi kupanda chap mpaka kufikia kucheza laliga, thamani ya timu na hata uwanja ilikuwa n vigumu kucheza mechi mpaka wakaanza kuchangiwa.

Fatilia Utajua hilo.
 
Watu kama Hawa ndio wanataka wakina mwigulu na samia wasiwe mafisadi

Na hawo wazee wa usajiri walivyokuwa wanonko wameunganisha mfumo wao na TCU ili watu kama hawa waficha degree watulizwe.
 
Kuna changamoto katika mfumo wa ajira.

Baadhi ya watu wamesoma kozi tofauti katika ngazi ya cheti na diploma, lakini nafasi za kazi zinapotangazwa kulingana na kozi walizosoma katika ngazi ya cheti, mfumo unawakatalia kuomba kwa madai kuwa hawana sifa zinazohitajika.

Nashauri mfumo uruhusu mtu kuomba nafasi za kazi kulingana na elimu alizosomea katika ngazi za chini, bila kujali ana kiwango cha juu zaidi cha elimu katika kozi tofauti. Hata hivyo, hili lisihusishe wale wenye cheti na diploma katika kozi husika. Asante
Ikiwa hvy, huyo wa cheti au diploma watapata kazi lini?

Kwa hii roho mbaya yako, utaendelea kusota na karatasi lako la degree mpaka kiama.

Tujifunze kuappreciate Wenzetu wanaofanikiwa Hata kama tumewazidi.
 
Labda ungesema Spain vs Ihefu ndo ungekuwa sahihi kwenye huu mfano wako

Madrid vs Ihefu ni ishu inayowezekana kwa 100%

Kama utakuwa unafatilia laliga Kuna timu iliwahi kupanda chap mpaka kufikia kucheza laliga, thamani ya timu na hata uwanja ilikuwa n vigumu kucheza mechi mpaka wakaanza kuchangiwa.

Fatilia Utajua hilo.
Inawezekana ndio lakini, usawa haupo. Mshindi anakua anajulikana. Hicho ndio wanaavoid
 
Hakuna usawa, kwamba zinakuwa sio timu za mpira au?

Kwa mtu anayefatilia mpira ataona umeandika kitu usichokijua.

Uefa, Munich anakutana Na timu ambayo thamani ya timu mzima na makocha haizidi hata $10m na Munich anapigika vzr tuu, Fatilia mechi ya uefa ya Munich aliyopigika msimu huu.
 
Kuna changamoto katika mfumo wa ajira.

Baadhi ya watu wamesoma kozi tofauti katika ngazi ya cheti na diploma, lakini nafasi za kazi zinapotangazwa kulingana na kozi walizosoma katika ngazi ya cheti, mfumo unawakatalia kuomba kwa madai kuwa hawana sifa zinazohitajika.

Nashauri mfumo uruhusu mtu kuomba nafasi za kazi kulingana na elimu alizosomea katika ngazi za chini, bila kujali ana kiwango cha juu zaidi cha elimu katika kozi tofauti. Hata hivyo, hili lisihusishe wale wenye cheti na diploma katika kozi husika. Asante
Hiyo walishakataa katakata
 
Hakuna usawa, kwamba zinakuwa sio timu za mpira au?

Kwa mtu anayefatilia mpira ataona umeandika kitu usichokijua.

Uefa, Munich anakutana Na timu ambayo thamani ya timu mzima na makocha haizidi hata $10m na Munich anapigika vzr tuu, Fatilia mechi ya uefa ya Munich aliyopigika msimu huu.
Level ziko tofaiti mkuu. It was for education purpose mkuu.
 
Kama unaona vyeti vyako vya degree na dip vitakuzingua achana navyo jaza cheti cha certificate kisha utabadilishiwa ukiingia kazini

Tofauti na hapo acha tamaa boresha uwezo wako pambania degree yako hadi ikupe kazi
 
Ukiwa na elimu ya degrees + ujobless + Unaona wa chini yako wanapata kazi, automatically lazima uwe na roho mbaya na chuki dhidi ya huyo mtu wa chini yako.

Wabongo sisi jau kummke 🙌
Nimeshangaa sana... Hii ni aina ya watu ambao yupo radhi apate hasara ilimradi tuu amkomoe mwingine..
 
Back
Top Bottom