Hivi kwanini KENYA ni maarufu kuliko nchi nyingi sana
Katika bara letu la AFRICA?
Yani ni vitu gani.....vinaifanya KENYA..ijulikane sana
Kuliko nchi nyingine nyingi za ukanda huu wa AFRICA?
Sahau kuhusu the issue of WILDLIFE.
WHY KENYA?
Kenya ilikuwa ni koloni la Waingereza ambalo walitaka kulifanya sehemu ya kuhamia.
Kama Australia ya Afrika.
Hivyo walianza kujipanga kuweka mambo kuhamia kabisa.
Tofauti na sehemu kama Tanganyika ambako hakukuwa koloni, ila Trusteeship /Mandate tu.
Hili likisababisha uchumi wa Kenya uwekwe imara kimfumo kama sehemu Waingereza walipotaka kuhamia. Tofauti na Tanganyika.
Pia, Wakenya walivyopata uhuru hawakujiingiza kwenye experiments za Ujamaa, walikwenda kwenye ubepari moja kwa moja. Imesaidia uchumi wao kuwa consistent.
Wakenya walianza kufunguka na kusafiri dunia nzima kutafuta fursa zamani kulinganisha na Tanzania.
Uchumi wa kibepari umewafanya Wakenya kuwa hustlers zaidi. Wakati watu wa Tanzania wamefungiwa kutoka nje na serikali ya kijamaa, mtu wa Tanzania kutafuta fursa kwenda nje ikionekana kukisa uzalendo, Wakenya walikuwa wanatafuta fursa kwenda nje.
Wakenya hawana jeuri kwenye kutafuta hela, ukija mzungu unawapa hela hata miguu watakulamba.
Ndiyo maana Mkenya akishajua kitu kitaongeza uchumi hana siasa nyingi. Ndiyo maana Kenya wameruhusu dual citizenship, sisi tunaleta figisu za kisiasa.
Watanzania maskini jeuri, wanaweza kufa kwa njaa, wakaambiwa hapa kuna hela jifunzeni Kiingereza tu mfanye kazi za Customer Service muwe wanyenyekevu tu, wakakataa.
Angalia vipaji vya riadha vile vile vilivyopo Kenya Tanzania vipo, ila mafanikio ya riadha Kenya ni tofautibkabisa na Tanzania.
Tanzania figisu za kisiasa nyingi sana. Kenya wenzetu wanapeana fursa na michongo.