Kwanini Kenya ni maarufu kuliko nchi nyingi za Afrika

Kwanini Kenya ni maarufu kuliko nchi nyingi za Afrika

japo nigeria ndo tech hub kubwa africa, ila inasemekana maendeleo ya tech yalianza kenya

m-pesa imeanza kutumika kenya africa nzima

serikali ya ke ndo ya kwanza duniani kutumia mobile money(hiyo m-pesa) kuuza goverment bonds

kenya kuna kikundi cha wataalam wa IT kikubwa tokea early 2010s huko, wametengeneza na wanatengeneza tech startups nyingi(japo nyingi zinakufa, zinakosa funding)
Kenya kwenye huo upande wa IT wako mbali mno. Kwa mfano hapa TZ ukikuta vijana wanaoweza kucheza na Adobe Photoshop, Corel draw na app zingine za graphics basi huweka mabega juu wakati Kenya hayo mambo hata secretary tu ofisini anafanya kwa mshahara mdogo.
 
Kenya is renowned in Africa for its diverse landscapes, including the iconic Maasai Mara National Reserve and Mount Kenya. It's also recognized for its rich wildlife, featuring the "Big Five" – lions, elephants, rhinos, leopards, and buffaloes. Additionally, Kenya is known for its vibrant culture, Swahili language, and as a hub for safari tourism. The country's capital, Nairobi, serves as a major economic and political center in East Africa.
True🤣🤣🤣🤣
 
Chanzo cha umaarufu in a good way
1. Tourism
2. Cultural Heritage-The vibrant and colorful Maasai
3. Sporting Achievements-Kenyan athletes
4. Innovation and Technology-MPESA, Nairobi-the capital city is known as the "Silicon Savannah"
5. Film-Lupita Nyongo.

Chanzo cha umaarufu in a bad way
1. Corruption
2. Political Instability
3. Security Concerns-close to Somali border
4. Inequality and Poverty
5. Tribalism
6. Nepotism
7. One of the world's top (ten slum HQ).
8. Terror hot bed
 
Kenya kwenye huo upande wa IT wako mbali mno. Kwa mfano hapa TZ ukikuta vijana wanaoweza kucheza na Adobe Photoshop, Corel draw na app zingine za graphics basi huweka mabega juu wakati Kenya hayo mambo hata secretary tu ofisini anafanya kwa mshahara mdogo.
Hizo si ni normal applications. Kwani ndiyo IT hiyo?
 
kiufupi ukiiondoa nchi chache za afrika magharibi especially nigeria Kenya ina world class celebrities wengi kuliko nchi yeyote africa, kenya ina dominate olympics kwenye marathon miaka mingi G. O. A. Ts hawa watu wanashiriki rugby world cups na walishakua na rais wa marekani kiufupi mijamaa inakelele sana uko duniani na wenzao wapopo sisi tupotupo tu kama mang'ombe
 
Kenya ilikuwa ni koloni la Waingereza ambalo walitaka kulifanya sehemu ya kuhamia.

Kama Australia ya Afrika.

Hivyo walianza kujipanga kuweka mambo kuhamia kabisa.

Tofauti na sehemu kama Tanganyika ambako hakukuwa koloni, ila Trusteeship /Mandate tu.

Hili likisababisha uchumi wa Kenya uwekwe imara kimfumo kama sehemu Waingereza walipotaka kuhamia. Tofauti na Tanganyika.

Pia, Wakenya walivyopata uhuru hawakujiingiza kwenye experiments za Ujamaa, walikwenda kwenye ubepari moja kwa moja. Imesaidia uchumi wao kuwa consistent.

Wakenya walianza kufunguka na kusafiri dunia nzima kutafuta fursa zamani kulinganisha na Tanzania.

Uchumi wa kibepari umewafanya Wakenya kuwa hustlers zaidi. Wakati watu wa Tanzania wamefungiwa kutoka nje na serikali ya kijamaa, mtu wa Tanzania kutafuta fursa kwenda nje ikionekana kukisa uzalendo, Wakenya walikuwa wanatafuta fursa kwenda nje.

Wakenya hawana jeuri kwenye kutafuta hela, ukija mzungu unawapa hela hata miguu watakulamba.

Ndiyo maana Mkenya akishajua kitu kitaongeza uchumi hana siasa nyingi. Ndiyo maana Kenya wameruhusu dual citizenship, sisi tunaleta figisu za kisiasa.

Watanzania maskini jeuri, wanaweza kufa kwa njaa, wakaambiwa hapa kuna hela jifunzeni Kiingereza tu mfanye kazi za Customer Service muwe wanyenyekevu tu, wakakataa.

Angalia vipaji vya riadha vile vile vilivyopo Kenya Tanzania vipo, ila mafanikio ya riadha Kenya ni tofautibkabisa na Tanzania.

Tanzania figisu za kisiasa nyingi sana. Kenya wenzetu wanapeana fursa na michongo.
true...
 
6. Nepotism
7. One of the world's top (ten slum HQ).
8. Terror hot bed
Wewe umetoka na bile yako ya Nairobi vs Dar ukaleta huku. Angalia watanzania wenzako wasiokuwa na uzalendo bandia (blind patriotism) wanavyochangia humu. Take this bile away. Hapa tunaongea pasi na uzalendo
 
Watu kama akili zenu ni kuwaza kukimbizana na mwenge mtakuwaje maarufu wakati ni wazi kwamba hamna akili.

Hata muamke mkute sukari kilo shilingi elfu kumi lakini bado tu mtamshangilia mama na kumvika majoho ya uchifu. Wakenya sio wajinga hivyo.
 
Back
Top Bottom