Watu wanapenda kudanganyana. Halafu wengi ukiangalia ni ushabiki tu. Hakuna hata hoja ya maana wanayojenga au kuonesha.
Wee tangu lini mtoto aanze darasa la kwanza mpaka anamaliza level hiyo bila kupimwa kama alielewa yale aliyokuwa amefundishwa?? Na kipimo cha kuelewa duniani kote ni mtihani ama uwe wa kuandika au wa kuzungumza.
Mpaka mmoja anadiriki kudanganya kwamba ulaya hakuna mitihani wakati si kweli. Huyu
mbarika atafute kitu kinaitwa ects ajionee kama kweli ulaya hakuna mitihani.
Mitihani haikosi, hata mataifa ya Asian Tiger tunayoyaonea tamaa, wana mitihani. Ambayo lengo lake ni kupima uelewa wa wanafunzi. Kuboresha elimu ili ionekane ina tija zaidi kwa jamii, ni kuangalia kama yale yanayofundishwa na namna wanavyofundishwa yana saidia katika kuleta maendeleo chanya ya jamii na nchi kwa ujumla. Kwa hiyo tuangalie elimu kwa ujumla wake, na si kuangalia kipengele kidogo sana cha mitihani.