Kwanini kila mtu anaikimbia rangi nyeusi? Kuna siri gani?

Kwanini kila mtu anaikimbia rangi nyeusi? Kuna siri gani?

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Leo nimesikia kuwa na Wamisri wamegomea movie inayomzungumzia Cleopatra kama mwanamke mweusi.

Kuna mifano mingi tu ya kusema hapa ni jinsi gani weusi unachukiwa, tunachukiwa. Tatizo nini haswa? Kuna siri gani? Ni huu huu ukosefu wetu wa maarifa au kuna jingine?
 
Leo nimesikia kuwa na wamisri wamegomea movie inayomzungumzia cleopatra kama mwanamke mweusi.

Kuna mifano mingi tu ya kusema hapa ni jinsi gani weusi unachukiwa, tunachukiwa. Tatizo nini haswaa? Kuna siri gani? Ni huu huu ukosefu wetu wa maarifa au kuna jingine?
Mbona mi napendwa sana na weusi wangu hadi I feel proud with ma color!!
 
We mwenyewe hutambui tofauti kubwa kati yetu na watu weupe??
 
Leo nimesikia kuwa na wamisri wamegomea movie inayomzungumzia cleopatra kama mwanamke mweusi.

Kuna mifano mingi tu ya kusema hapa ni jinsi gani weusi unachukiwa, tunachukiwa. Tatizo nini haswaa? Kuna siri gani? Ni huu huu ukosefu wetu wa maarifa au kuna jingine?
Cleopatra ana madudu mengi kuna ile ambayo alicheza mzungu yaliyofanyika mule, amecheza Elizabeth Taylor na Joseph Makwenzi ni whites kabisa wakaangalie ile hii ya black watuachie mablack tujipongeze, mboni hata Yesu yupo mweusi alieigiza hatukusikia kelele zozote mtoeni huyo Yesu mweusi hatumtaki
 
Leo nimesikia kuwa na wamisri wamegomea movie inayomzungumzia cleopatra kama mwanamke mweusi.

Kuna mifano mingi tu ya kusema hapa ni jinsi gani weusi unachukiwa, tunachukiwa. Tatizo nini haswaa? Kuna siri gani? Ni huu huu ukosefu wetu wa maarifa au kuna jingine?
Hao wote hupendelea kuvaa suti nyeusi
 
zamani tulipokuwa watoto wadogo tuliyaogopa sana magari meusi. Tukiyaona tulikuwa tunakimbia mbali kwa hofu
Gari jeusi linatisha na likipigwa tinted nyeusi ndio kabisa, Tena kuna haya wanayaitaje sijui yaan ukiliona mbele ngao mnyama sio mnyama
 
Lazima wachukie, just imagine kupewa sifa za kinafiki ama kupotosha ukweli kisa kuwafuraisha watu..

Kama muonekano wa Mtu fulan ulikuwa wa aina gani kwanini leo hii watu waubadirishe? Je inawezekana kubadiri uhusika wa mtu na Utu wake? Kama haiwezekan kwann hao watu wa Filam+historia wamekuwa wakipenda kubadiri mionekano ya watu kuwa ni aina fulan kumbe sivyo hivyo?.

Hakuna anaepinga kwa nia mbaya bali ukweli ubaki ukweli kama huyo cleopatra alikuwa mweupe acha uhalisia wake uwe hivyo, hizo tabia za kubadiri mionekano ya watu imeletwa na wazungu+waarabu kwa manufaa yao ya kukuza na kuzipa nguvu Race zao(white supremacy) na inajulikana wamefanya ushenzi huo hata ktk maandiko ya vitabu vya kiimani.

Rangi nyeusi ndio Rangi KUU na yenye UTISHO kuliko rangi yoyote, pia rangi nyeusi kwakuwa ndio asili ya Uungu na uumbaji hivyo haiwezekan kwa vyovyote vile kuifake ama kuitengeneza bali inajitengeneza yenyewe ndiomaana hakuna mpka leo aliyeweza kutengeneza Kiza/giza wala kuunda mwanga wenye kiza/giza wala kuunda giza feki, haiwezekan na wala kumbadiri mtu mweupe kuwa mweusi haiwezekan kwakuwa Asili inanguvu na haiwezi kubadirishwa kwa vyovyote vile[emoji23][emoji23]ila inawezekana mweusi kuonekana mweupe nae mweusi huyo si kumbadiri bali kwa kummulika weusi wake usionekane kwa kutumia viambatasumu(chemicals) kwa binadamu ama kutumia mwanga wa rangi ktk Giza kulifanya lisionekane.

Iko ivyo watu weupe wazungu+waarabu na race za jinsi yao wanajua kuhusu huu ukwel ndiomaana wanajaribu kufanya rangi hii idharaulike.

Walianza kwa uzushi wa kuishusha thamani kupitia ukolon na ubaguz wa rangi, wakaja ktk maandiko kufanya ubaguzi ionekane hata viumbe wa kiroho ni weupe na mashetani ni weusi, kumbe kiuhalisia MALAIKA NA VIUMBE WA MBINGUNI ni Weusi kama alvyo mtu mweusi, bali Mashetan na mapepo ndio wenye rangi ya laana yaani rangi isiyo na UTU(UUNGU) rangi nyeupe, ndiomaana hata viumbe wa giza wote huja ktk mionekano yao ya weupe, majini weupe, malaika wa uongo wanaowatokea manabii wenu wa uongo nao ni weupe, hakuna jini mweusi na hayupo tembea popote uliza kwa yeyote hata kwa waganga wa kienyeji majini+mapepo mionekano yao ni mtu wa race ya Mwarabu+mzungu kwakuwa ndio asili zao na sio weusi je kwann leo hii hawa watu wamekanusha hii kweli na kuwaaminisha mashetan ni weusi na malaika ni weupe?.

Sababu kuu ni kuwafanya watu weusi waidharau asili yao.

Baada ya wakolon kuja walisafisha nakala zote za kihistoria zilizowahusu waafrika nakala ambazo zilikuwa za maandiko ya kiroho, technolojia na mambo mbalimbali ambayo leo hii wameyabadiri na kuyafanya yaonekane wao ndio waanzilishi.

Afrika ndio Paradise ya kimwili hapa dunian ndiomaana Vurugu haziishi kwa watu weupe kugombea resources kupitia machafuko na vibaraka wao wa kisiasa.

Fungueni akili jmn someni muijue asili yenu.
 
Gari jeusi linatisha na likipigwa tinted nyeusi ndio kabisa, Tena kuna haya wanayaitaje sijui yaan ukiliona mbele ngao mnyama sio mnyama
Huo ndio utisho wenyewe maana hata zaman mtu mweusi alikuwa akiabudiwa kama MUNGU wa dunia kwakuwa na ule UTISHO wa asili ulikuwepo ndani ya watu weusi.

Miungu hawa wa dunia yaan watu weusi ndio waliojenga pyramids na ndege za ajabu hapo zaman kabla hata ya izi technolojia feki za leo hazipo, bila kusahau technolojia za anga, matibabu, mahesabu lkn baada ya hawa watu weusi walipoanza kuzisaliti nguvu za Asili za Uungu wao ndipo wakaanza kupoteza ushawishi dunian na nguvu zao hatimae watu weupe(machotara wa aliens) wakapata nafasi ya kuitawala Africa hapo waliitawala baada ya maelfu ya miaka waliyokuwa wakijaribu kuivamia lkn wanashindwa, leo hii wamepata chance ya kututawala usidhani wataitumia vibaya hii chance,

wazungu wanatujua zaidi ya tunavyojijua maana wamecheza na historia zetu na za babu zetu kwa maelfu ya miaka na leo hii vizazi vyao vinaendeleza mchezo huo huo wa kutushikiria maana wanajuwa historia na walichoachiwa na babu zao mission ya kuitawala afrika daima huku sisi tukienda kama misukule hatujui tunaishi vipi dunian, hatujui historia yetu, hatujui mwanzo wetu, hatuna mchango wowote tena hapa dunian leo hii zaid ya kula, kulala, kusapoti ajenda zao na kuuwana sisi kwa sisi, acha tutwangane mpaka tutakapopata akili.
 
Cleopatra alikuwa mzungu wa Ugiriki. Wacha tu wachukie kwa upotoshaji unaofanyika
 
Cleopatra hakuwa mweusi, mtu wazazi wake walikuwa Wagiriki wa Macedonia kutoka uzao wa Ptolemy anakuwaje mweusi. Ujue Netflix wanakosea historia sana kwenye movies zao kisa kufurahisha watu The first temptation of Jesus waliigiza Yesu ni shoga na Maria anavuta bangi, kwenye movie ya Vikings wanaonyesha Malkia mmoja mweusi.

Egypt wana haki ya kuwafungulia mashtaka. Hawa siku nyingine wataigiza Mtume Muhammad akiwa Myahudi
 
Back
Top Bottom