Kwanini kila pakiboreshwa wateja wanakimbia?

Wateja walizoea style yako ya zamani,sasa umebadilisha ukaleta mpya ikawa ngumu kwa wao kuisoma.
 
Mkuuu suala la Chakula ni ladha ya msosi. Wakati ukiwa kwenye maboresho wateja wako wameshapata sehemu nyingine ya kula ambako Mapishi tayari wameyazoea huenda pia wanapata tips za dagaa, chachandu na mboga za majani bure hivyo hawana haja ya kurudi kwako wamevumbua chimbo lingine. Inshort nenda kasome mchezo wafanyacho wapinzani wako wewe uboreshe zaidi.
 
Hiyo ipo sana ukiboresha mahali watu wanaogopa wanadhani ni pa bei mbaya.
Hata magenge ya vibanda yanauza kuliko mtu mwenye fremu
 
Weka tangazo la bei za chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu kilichokutokea na mimi kimewahi kunitokea! Nilikua na ka bar kwenye kona fulani ina ka giza giza na imekaa shaghalabagala. Basi waendesha bodaboda, bajaji na vijana vijana wengi wa mtaani walikua wanapenda sana kuja mida ya jioni kupiga ulabu na nyama choma pale.
Nikaona nipaboreshe nikaita mafundi wakapatengeneza vizuri, safisha kila mahali piga rangi, funga taa nzuri mpaka barabarani, weka ma flat screen, music safi, n.k pakawa bomba mbayaa na bei sikupandisha.
Tangu nipaboreshe sikuwahi kuona tena mteja yoyote kukanyaga pale! Sio bodaboda, wala wateja wa kawaida wote wakakata miguu hadi mwisho ikabidi nipafunge tu.
 
Poleni
 
Tuambie Ni maboresho gani umeyafanya ili tukushauri huwenda umeleta wahudumu was vimini na eneo Hilo SI wapenzi wa kuangaia mapaja ya kilamtu USITEGEMEE KUPATA WATEJA MKUU!
 
Umenena vyema sana ndg. Waliowengi wanaogopa sehemu smart sana hata kukaa tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumezoea kula kipindupinduini hata chipsi huku Dar wanaita chipsi vumbi...usafi sio utamaduni kwa wengi wetu
 
usije ukalogwa ukafanya marekebisho kwenye biashara ambayo imeshachanganya....lazima wateja wataingiwa na hofu..halalfu watatokomea
 
Naomba nije inbobo kuna madini nahitaji toka kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…