Watetezi wake Huwa wanakuja na ushahidi kuonyesha amenukuliwa vibaya.
Hii SI mara ya kwanza. Najiuliza. Anafanya kusudi?
Ana akili kubwa kiasi kwamba sisi walala hoi na waandishi makanjanja huwa hawamuelewi?
Ana mkakati wa kuifanya Dunia kuwa conscious na ushoga ili waone ni kitu Cha kawaida?
Huwa roho mtakatifu anamshukia ananena mambo ambayo linatakiwa jopo la kuyatafsiri kabla hayajafikia waumini na wafuasi wa ukatoliki Zaidi ya Bilioni ulimwenguni kote.
Ambao huwa mnaelewa mtusaidie sisi wakosefu.
Mwangalie Mungu na maagizo yake achana na papa .
Yule ni mtu kama watu wengine tofauti ni kuwa amesoma sana na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa juu kabisa wa Kanisa la Warumi kusimamia Mila na tamaduni za kirumi Duniani. Yule ni msimamizi wa Dola la Kirumi Duniani. Ndio maana makao makuu ya kanisa Katoliki yapo Kwa warumi. Na umeshaambiwa ni Roman Catholic Church. Ni kanisa la Warumi.
Wanaoongozwa na waliomchagua Papa wanamuelewa Kiongozi wao. Hata akijiumauma kuwa kwenye msimamo wa ushoga ni kwamba yeye sio Mungu Wala Mtume Wala Nabii Bali ni Kiongozi wa Kanisa ili kanisa liwe na mfumo usioyumbishwa yumbishwa.
Suala la Ushoga ni suala la Wazungu masalia wa Sodoma na Gomora . Na Papa ni mzungu hawezi kupingana na Mila zao . Waliopinga na kuweka SHERIA Kali za kimaadili walikua ni Wayahudi na Waarabu na jamii za Mashariki ya mbali. Sharia za maadili ni tishio sana Kwa wazungu.
Ungeongelea kuoa wake wengi papa angeonyesha msimamo wake thabiti wa Kupinga ndoa za mitaala.
Au ungezungumzia suala la Kukeketa Wanawake angesimama kidete kuwasuta wakurya na wasomali.
Lakini suala la Mila za Wazungu kuoa wanaume Kwa wanaume Hilo anazunguka zunguka Kwa kauli tata.
Chukizo limesimama mahali pa takatifu.
Mpango wa Mungu Kwa wanadamu ndio utakaoshinda.
Mwanakondoo ameshinda ,tumfuate.