matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Tofauti yako na yule ambaye unaona anamfaidi Mungu na nguvu zake iko kichwani na kinywani mwako.
Wote ambao akilini mwao wanaamini katika ufinyu na uhafifu wa uwezo wa Mungu watafaidi uhafifu na ufinyu huo.
Wale wanaoamini katika na kusadiki kabisa kuwa kwao Mungu ananguvu na uweza wote kuliko kitu chochote hao ndio watakaofaidi ukuu huo.
Kazi hii inafanyika kichwani mwako.
Unachokiamini kichwani sharti ukinene mdomoni. Ukisikia mtu anasema anaamini Mungu wakati mdomoni anatamka mambo ya shetani, uchawi, kulongwa, na kushindwa hali ya maneno yako ndio itakayokuzunguka.
Warumi 10:10
Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Ni hayo tu.