Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Biblia imeshasema wana wa Mungu ni wale wote wanaofanya mapenzi ya Mungu na hata alipozaliwa seth ndio tunaambiwa WALIANZA KULIITA JINA LA BWANA na hivyo wana wa Mungu walikuwa wana wa seth alafu wa Cain ndio hao wanadamu

Hivyo basi kivipi tena Henoko asimamie hoja kuwa wana wa Mungu ndio wale malaika waliozaa na wanadamu???

Henoko anasema hao malaika walikuwa wanaweza kupaa hadi kwenye jua sasa kivp gharika liwaue ilihali wanaweza kwenda hata mwezini????

Mie nataka kujifunza zaidi hivyo sina nature ya kubisha ningependa unisaidie kwanini kicontradict na biblia nzima alafu wewe uone kinatakiwa kitumike na wakristo
 
Vigezo ni kuwa lazima viandikwe kwa KUONGOZWA na roho mtakatifu

Cha pili kuwe na mtiririko wa kuendana na vitabu vingine

Hao waliokusanya biblia waliweka vigezo kwenye kikao cha Constantinople miaka ya 384 AD na wasomi wakikristo wa enzi hizo walikutana wakaweka vigezo sasa kivp useme hawakuongozwa na roho mtakatifu??

Vitabu vilivyoachwa kubwa ni sababu hiyo ama havikubaliani na maandiko ya manabii wengine ama vinakinzana mfano henoko alisema wana wa Mungu ni malaika ilihali marko anasema ni wale wanaofuata mapenzi ya Bwana sasa huoni wangejichanganya

Otherwise hamkatazwi kuvisoma ilihali vingi havina mfanano na vya kwenye biblia..... Ukiweza soma kitabu FIRST BOOK OF ADAM AND EVE utagundua nachokisema kina mengi mazuri ila kimekinzana kiduchu tu kma neno moja ndio maana kikaachwa

All in all vilivyopo vinatosha ndio maana hata Yesu alisema kama kila kitu kingeandikwa biblia isingetosha
 
mkuu Utingo kun kitu nimekinot kwenye coment yako kupitia mistar ulioitoa kumbe kuna pia kitabu cha yashari? sikuwahi kusoma wala kudhania hili, na hata nikiuliza kwa kiongozi wangu wa kiroho nadhani hatanipa jibu, unaweza kutupa mwanga kidogo mkuu?
Yashari kinapatikana wapi
 
baby wangu kumbe unamjua Mungu eeh ngoja nitafute kitabu cha tomaso halafu kitakuwa cha kweli maana huyu tomaso alikuwa mwanafunzi wa yesu so ina maana aliyoandika ni ya kweli maana aliyaona unlike kina mathayo .luka marko wale walisimuliwa tu
Watu mnajua kufuatilia hatar tupu!
 
Hapa kuna jambo la kutafakar!
 
Mkuu una copy ya kiswahili mie ninayo ya kiingereza ila radha inapotea kwenye translation
 
Mkuu una copy ya kiswahili mie ninayo ya kiingereza ila radha inapotea kwenye translation
Dah hapana mkuu sina version ya kiswahili ingawa kinachanganya ila ukikisoma kwa umakini utapata muktadha mzima wa alichokiongelea humo
 

Mkuu siafazali bibilia maana wanasema kuruani waliichakachua kipindi cha kaliphate ya mawaiya (kama sijakosea jona) na wakachoma vitabu vingine vyote.

Dini zote hata za waafika kama dini ya kinjekitile zilikua ni mbinu ya kutawala kama sera ya viwanda
 
Tatizo letu tunapenda kudandia gari kwa mbele, kabla ya kusoma vizuri Biblia tulipaswa kwanza kujifunza ni Nani aliandika, wakati gan na kwa lengo gan na vitu gan viliathiri maandishi yao. Vitabu vingi vya agano la kale havikuandikwa na manabii Kama inavyoonekana kwenye Biblia na Wala havikuandikwa kipind manabii hao wakiishi ila manabii wamepewa heshima Kama waandishi.

Kingine Cha kujua ni kwamba mkusanyiko wa vitabu wa vitabu vya kwenye Biblia ulifanywa na waroma hivyo upo uwezekano wa wao kukataa kitabu kwasababu yao binafsi ila wakatoa sababu nyingne.
 
Binafsi kuhusu kitabu cha Henoko kuondolewa kwake sababu kuu ni mtiririko (Sequence) kwa sababu ukikisoma ni kama kinabidi kiwe katikazi ya Maelezo ya kitabu cha mwanzo ilhali Mwanzo yenyewe inajitosheleza!
 
Mkuu naona unazidi kuchanganya watu....umeanza vizuri ila ulipoingiza waroma umeharibu kila kitu sasa kma unadai waroma ndio walivipunguza na kukataa vingine iweje sasa biblia ya wakatoliki iwe na vitabu 72 ilihali ya waprotestant ambayo wewe unatumia iwe na vitabu 66?? Nani aliyepunguza hapo???
 
Wana wa Mungu limetokea kama mara 61 kweny Biblia likiwa kama Wana wa Mungu au Mwana wa Mungu: Mwanzo 6;2,Mwanzo 6;4,Ayubu 1;6,Ayubu 2:1, Zaburi 29:1, Hosea 1:10, Mathayo 4:3, Mathayo 4:6, Mathayo 5:9, Mathayo 8:29, Mathayo 14:33, Mathayo 16:16, Mathayo 26:63, Mathayo 27:40, Mathayo 27:43, Mathayo 27:54, Marko 1:1,Marko 3:11, Marko 5:7, Marko 15:39, Luka 1:35,Luka 4:3,Luka 4:9, Luka 4:41, Luka 8:28, Luka 20:36, Luka 22:70,Yohana 1:34, Yohana 1:49, Yohana 5:25, Yohana 9:35, Yohana 10:36, Yohana 11:4, Yohana 11:27, Yohana 19:7, Yohan 20:31, Matendo ya Mitume 8:37, Matendo ya Mitume 9:20, Warumi 1:$, Warumi 8:14, Warumi 8:19, Warumi 9:26, Wakorintho 1:19, Wagalatia 2:20 Wagalatia 3:26, Waefeso 4:13, Wafilipi 2:15, Waebrania4:14, Waebrania 6:6, Waebrania 7:3,Waebrania 10:29, 1 Yohana 3:1, 1 Yohana 3:2, 1 Yohana 3:8, 1 Yohana 4:15, 1 Yohana 5:5, 1 Yohana5:10, 1 Yohana 5:13, 1Yohana 5:20, na Ufunuo wa Yohana 2:18.
Ukisommistari hiyo yote katika Muktadha wake utagundua kuwa hakuna contradiction ila contradiction inaonekana kuwapo/kuwepo katika kuelewa.Muktadha wa wana wa Mungu unajengeka katika Makundi matatu/vifungu vitatu.Fungu la kwanza uko katika Agano la kale na Ufunuo wa Yohana,fungu la pili katika injili (yaani Mathayo Luka Marko na Yohana) na fungu la tatu linajitokeza katika Matendo ya mitume Warumi naNyaraka za paulo.
Ukisoma maelezo yaliyoko katika Agano utagundua Mandhari(Setting ya hawa wana wa Mungu ni Mbinguni-Yaani wana hawa wa Mungu asili yao ni Uungu tunaweza kusema hawa ndio wana wa Mungu halisi kwa kuwa Tangu kuumbwa kwa ulimwengu walikuwepo ukisoma kitabu cha Henoko yaani hawa ndio kina Gabriel upande mmoja na kina Shemyatsa na kundi lake upande wa pili.Kwa hiyo wana wa Mungu asili yao ni mbinguni.
Ukija kwenye Injili Tunaona hapa anazungumziwa Yesu kama -mwana wa Mungu -huyu naye asili yake ni mbinguni kwa hiyo naye ni mwana wa Mungu.
Sasa swali linakuja inakuwaje
Biblia imeshasema wana wa Mungu ni wale wote wanaofanya mapenzi ya Mungu..............................................................................................
Kwa hiyo Mwanzoni wana wa Mungu asili yao ilikuwa mbinguni,baadhi wakaasi kwa kujichafua na binadamu,original plan ya Mungu ikawa imeharibika mpaka ikabidi Yesu/Yahusha(Ben of Adam) aje duniani (You know the story)kuja kurekebisha ku-salvage kwa(sacrifice) kumwaga damu yake msalabani .Kwa hiyo Baada ya kifo cha yesu Watu wote wanaojiunganisha na Yeye yule aliyekubali kufa Msalabani wanapata uwezo kuwa wana wa Mungu ndio maana neno linasema Wale wote wanaofanya mapenzi ya Mungu which means sio kila mtu.Yohana 1:12,Warumi 1:4,Wagalatia 2:20 etc etc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…